Mgombea ubunge wa jimbo la Ubungo kupitia ACT-Wazalendo, akutana na upinzani mzito kutoka kwa Mkurugenzi wa Uchaguzi wa jimbo hilo, kwa kile kilichoonekana barua yake ya utambulisho kutofautiana na barua nyingine za chama hicho.
Japokuwa mkurugenzi mwisho alimkabidhi fomu, baada ya mashauriano marefu, lakini bado Mkurugenzi na Ofisi nzima wamebaki na mashaka.
Wakurugenzi wa Uchaguzi mnatumika vibaya sana. Yaani mnaleta matatizo kwa kulazimisha kasoro zisizo za lazima ili tu mpate sababu. Jizuieni uchama kwenye ofisi zetu za umma.