Mheshimiwa Bwana Canute,
Salaam sana na pole kwa mahangaiko na misukumsuko ya huko Kilema nakubaliana na barua yako kwamba majibu ya Mh. Mbunge wetu kuhusu tuhuma dhidi ya Diwani hayakuwatosheleza na hasa ukizingatia kwamba yeye mwenyewe katika kikao cha KDDTF cha 30 alitamka wazi kuwa matatizo makubwa yaliyoko huko vijijini ni uongozi mbovu ambao umajaa ufisadi mtupu - fedha na mali za wananchi zinatafunwa wazi wazi na viongozi ambao wako madarakani. Kwa hakika nadhani ni muda mwafaka kwa wananchi kuelezwa wazi wazi juu ya maswala haya yote yanayohusu maendeleo yao hususani masuala yanoyohusu fedha na mali za vijiji hayana budi kuwekwa bayana hadharani bila ya kificho au mizengwe yoyote ile. Dhana kwamba kiongozi hawezi kukosolewa au ni makosa kumkosoa kiongozi na kwamba kufanya hivyo ni chokochoko au fitina za kugombea madaraka mawazo kama hayo hayana nafasi katika dunia ya utandawazi na maendeleo ya sasa. Kwa mantiki hiyo basi naona suala hili linageuzwa kuwa ni vita binafsi ambavyo sivyo [kulingana taarifa ambazo umeziambatanisha barua ya awali]
Kwamba fedha zilitolewa na UNDP kwa wananchi wa Masaera kwa maendeleo yao kupitia asasi au kikundi husika na kwamba je fedha hizo zimetumika kama ilivyotakikana? Kwamba wasaini katika fedha hizo ni mtoto wa Diwani na mfanyakazi wake ni jambo lisilokubalika kisheria kwa masuala yanayohusu usimamizi wa fedha za umma je uchaguzi ulifanyika na kuwachagua hao wasaini ?
Mheshimiwa Bwana Canute bila ya kuingilia kwa undani zaidi saula hili na kulingana na sheria na taratibu za nchi yetu na katiba ya nchi - uhuru wa kutoa maoni -kama ibara namba 18 inavyojieleza
18.-(1) Bila ya kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru
kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta,
kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo
chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa
mawasiliano yake kutoingiliwa kati.
(2) Kila raia anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu
matukio mbalimbali nchini na duniani kote ambayo ni muhimu
kwa maisha na shughuli za wananchi, na pia juu ya masuala
muhimu kwa jamii.
na zaidi pia kulingana na madaraka ya Umma kama ilivyooanishwa katika katiba ya nchi yetu - ibara 145
MADARAKA YA UMMA
Serikali za Mitaa
Sheria ya 1984
Na.15 ib.50
145
.-(1) Kutakuwa na vyombo vya Serikali za Mitaa katika
kila mkoa, wilaya, mji na kijiji, katika Jamhuri ya Muungano,
ambayo vitakuwa vya aina na majina yatakayowekwa na sheria
iliyotungwa na Bunge au na Baraza la Wawakilishi.
(2) Bunge au Baraza la Wawakilishi, kadri itakavyokuwa,
litatunga sheria itakayofafanua utaratibu wa kuanzisha vyombo
vya Serikali za Mitaa; miundo na wajumbe wake, njia za mapato
na utaratibu wa utekelezaji wa shughuli za vyombo hivyo.
Kazi za Serikali
za Mitaa Sheria
ya 1984 Na.15
ib.20
146
.-(1) Madhumuni ya kuwapo Serikali ya Mitaa ni
kupeleka madaraka kwa wananchi. Na vyombo vya Serikali za
Mitaa vitakuwa na haki na mamlaka ya kushiriki kuwashirikisha
wananchi katika mipango na shughuli za utekelezaji wa
maendeleo katika sehemu zao na nchini kote kwa jumla.
(2) Bila ya kuathiri maelezo ya jumla yaliyomo katika ibara
ndogo ya (1) ya ibara hii, hiki chombo cha Serikali za Mitaa, kwa
kuzingatia masharti ya sheria iliyokianzisha, kitahusika na
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
104
shughuli zifuatazo -
(a) Kutekeleza kazi za Serikali za Mitaa katika eneo
lake;
(b) Kuhakikisha utekelezaji wa sheria na ulinzi wa
wananchi; na
(c) Kuimarisha demokrasi katika eneo lake na kuitumia
demokrasi kuharakisha maendeleo ya wananchi.
Mheshimiwa ndugu Canute nadhani kulingana na taratibu hizi ikiwa kiongozi anaonekana kupingana na katiba na matendo na mwelekeo wake hauridhishi ni vema akajiuzulu wadhifa huo. Kwa kuwa ni wazi viongozi wengi katika nchi za Kiafrika hawana tabia ya uwajibikaji ni vema juhudi za kujenga mila ya uwajibikaji kwa viongozi ikaanza kushirikishwa katika mila na desturi zetu za Kitanzania.
Kwamba ukweli haufichiki na ikiwa hayo mliyoyaeleza ni kweli basi nadhani ni vema Mwenyekiti wa kijiji pamoja serikali ya kijiji, Afisa Mtendaji wa Kata ya Kilema Kusini pamoja na wananchi mkaitisha mkutano wa wazi na ikiwezekana mkashirikisha pia uongozi wa serikali katika ngazi ya wilaya ambapo mambo yote haya mtayajadili na ikiwa Mh. Diwani atakuwa na tuhuma za kujibu basi itafaa awajibike na kama atakataa apigiwe kura ya kutokuwa na imani naye na kuondolewa madarakani kama wananchi watamkataa. Nadhani Bwana Canute umefikia muda wa kuwaweka viongozi waliochaguliwa kuwajibika kwa wale waliowachagua kwa kuanzisha taratibu za " IMPEACHMENT" hiyo ndiyo njia inayofaa badala ya kusubiri miaka mitano ya uchaguzi. Kwa waraka huu Mh. Bwana Canute KDDTF inaamini kabisa kwamba matatizo mengi ya ufukara, uhalifu na ujambazi kwa kiasi fulani unachangiwa na uongozi dhaifu na wababaishaji katika tarafa hii ni wazi kwamba KDDTF inaamini kuwa usuluhishi wa matatizo haya yote utatatuliwa au kumalizwa na wanajamii ya Kilema wenyewe kwa kuchukua juhudi mahususi za kupambana nayo katika ngazi zote kwa uwazi, ukweli na kwa haki kwa wote.
Tumsifu Yesu Kristo!
Wako katika utumishi
Dr. Joakim Michael Kifai
Katibu Mkuu_KDDTF
Dar es Salaam 6/11/2007.