Mr Mikazo
JF-Expert Member
- May 26, 2016
- 1,594
- 800
ALEXIS Sanchez bwana. Eti anataka mshahara wa pauni 400,000 kwa wiki ili aendelee kubaki Arsenal.
Hivi anajua kuwa ligi nzima ya Ujerumani ‘Bundesliga’ hakuna mchezaji anayelipwa pauni 200,000 kwa wiki. Mchezaji anayelipwa ghali pale ni Roberto Lewandowski, tena ni pauni 180,000 tu kwa wiki. Huyu Sanchez hii bange unayovuta ni ya nchi gani?
Eden Hazard, aliyebeba Premier msimu uliopita analipwa pauni 200,000 kwa wiki, lakini hajainua mdomo wake kuomba kuongezewa mshahara.
Cristiano Ronaldo kule Madrid analipwa pauni 360,000 kwa wiki. Sasa huyu Mchile wetu eti anataka pauni 400,000! Yaani tukulipe zaidi ya mchezaji bora wa dunia? Umerogwa wewe, si bure.
Neymar, licha ya uwezo wake mkubwa uwanjani na pesa nyingi anazowapa Barcelona kwa mikataba ya matangazo, bado mshahara wake ni pauni 250,000. Ni kitu gani hasa Sanchez anachomzidi Neymar hadi pauni 300,000 tulizomuahidi azione ndogo?
Arjen Robben, fundi wa kupiga ndizi pale Munich, analipwa pauni 160,000 kwa wiki. Thomas Muller, nani asiyeijua shughuli yake? Mshahara wake ni pauni 150,000 kwa wiki. Wote wako kimya.
Yule Douglas Costa analipwa pauni 100,000 kwa wiki pamoja na ufundi wake wote. Sanchez hiyo pauni 400,000 unaitaka ya nini baba?
Hivi wakati tukipunyuliwa kile ‘kichapo hevi’ cha mabao 10 na Bayern Munich, si ulikuwepo uwanjani wewe? Ulifanya nini cha maana hasa hadi ukatutisha namna hii?
Douglas Costa hasemi anataka pauni 300,000 kwa wiki, pamoja na upambanaji wake wote, ila wewe uliyefungwa 10 unadai pauni 400,000, umechanganyikiwa wewe, si bure.
Luis Suarez analipwa pauni 200,000. Luka ‘fundi’ Modric, fundi haswa. Kabeba Ligi na Uefa na bado mshahara wake ni pauni 120,000 kwa wiki.
Eti yeye yuko kimya halafu wewe uliyebeba Kombe la FA tu unatunisha misuli kutaka pauni 400,000. Kusanya virago vyako baba, timu si ya baba yako hii.
Kwa taarifa yako sasa, si Chelsea, Manchester City, Manchester United, Barcelona, Bayern Munich, PSG wala hao Madrid wanaojifanya wamechanganyikiwa na matumizi ya hela, hakuna anayeweza kukupa mshahara wa pauni 400,000 kwa wiki.
Wewe kama unataka kwenda, nenda kwa amani tu baba. Tunakushukuru kwa vibao vyako ulivyotufungia fungia japo havijatupeleka popote zaidi ya kufuzu Uropa tu.
Ni hivi baba, hiyo ndoto yako ya kutaka tukulipe pauni 400,000 kwa wiki, ifute kabisa. Hatuna hela ya kuchezea kiasi hicho. Hiyo mibange waliyokuvutisha hao kina Vidal, usituletee huku aisee.