Barua ya Uchumba; sababu 30 zilizonifanya nimpose Binti Yenu

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
BARUA YA UCHUMBA; SABABU 30 ZILIZONIFANYA NIMPOSE BINTI YENU.

Kwa Mkono wa, Robert Heriel

Taikon , kijana wenu, mwana wa Tibeli, kutoka nyota ya Jibi, Kuhani katika Hekalu Jeusi.

Na, Kwa Baba na Mama Mkwe, wa Nchi ya Maziwa na Asali, inayomea miti izaayo matunda misimu yote.

Neema ya Mungu ikae juu yenu, tena baraka zake ziwafunike, ni matumaini yangu muwazima wa Afya, na Hiyo ndio Dua yangu niwaombeayo;

Ninayofuraha iliyohaja yangu tangu siku ile, nilipoonana na binti yenu; kuwaandikia barua hii ya Posa ili nimpose Binti yenu.

Nalipenda kuandika siku Ile Ile barua hii lakini Ukuu wenu ulifanya mikono yangu kutetemeka, sikuweza kuandika chochote, heshima yenu na utukufu mlionao ni mkubwa Sana kwangu kiasi cha kushindwa kuelezea.

Sio ajabu nalimtafuta mtaalamu wa kuandika ili aniandikie barua hii ikidhi ubora utakaoendana na heshima yenu; lakini sikupata licha ya kuhangaika huku na huku, ambapo niliongea na washairi, na wanafasihi wapatao sita lakini wote walinikatalia wakisema wao hawatathubutu kulegeza mirija ya kalamu zao mbele yenu.

Ikawa, nilipokosa na muda ungali ukisonga nikaona niandike mwenyewe.

Ningeenda mbele lakini sina budi kujitambulisha Kama ilivyokuwa Mila na desturi zetu Sisi Waafrika.

Naitwa Taikon Mtibeli, natoka Ukoo wa Tibeli, huko iliko nyota ya Tibeli. Kitaaluma Mimi ni Mwanafasihi, mkufunzi wa falsafa za kifasihi, kipato changu kinaweza kuwa Kama kitendawili ambacho kikitegwa hadhira haiwezi kukitegua. Umri wangu ni Alafu Lela utoe Mia kenda sabini na tatu.

Kimo changu ni urefu wa Riwaya za mapenzi zilizojawa na hisia za msisimko.
Napenda kuvaa nguo za hekaya za wahenga, ambazo zinanifanya nionekane nadhifu na kupewa heshima Kama malenga wa diwani ya Mloka.

Nilitaka kusahau, pengine dini yangu ningeisema, Mimi dini yangu ni PAUKWA na dhehebu langu ni PAKAWA.
Itoshe kusema huyo ndio Mimi Kwa uchache.

Barua hii ni ambatanisho la kujitambulisha kwenu na kumtambua binti yenu Kama mwanamke aliyeweza kuuteka mtima wangu, nachelea kusema siwezi dhibiti mapigo ya moyo wangu mbele yake.

Sifa zake hazihesabiki, uzuri wake hauelezeki ingawaje nimejaribu kuzidodosa Kwa uchache.

Wazazi wangu kupitia binti yenu, naomba kuzitaja sababu zilizonifanya niache makundi ya maelfu elfu ya wanawake Duniani na kutia nanga kwa Binti yenu. Sababu hizo nimeziandika Kama hivi;

1. Uzuri Kama Malaika
Binti yenu ni mzuri Sana, na hapa nazungumzia uzuri wa maumbile.
Uso wake mzuri Sana hata akipiga Miayo au akitoka kulala bado ni mzuri
Sababu hii itazaa vijisababu vidogo dogo Kama hivi;

2. Macho yake Kama njiwa Pori wa Serengeti.
Binti yenu macho yake sikuweza kuyafananisha na kitu chochote siku ya kwanza nilipomuona.
Lakini siku nilipoenda Mbuga ya Serengeti nikawaona njiwa wa kijivu, hakika moyo wangu ulilipuka.
Macho ya binti yenu yanamfanano ya njiwa Pori wa Serengeti. Macho ya upole yenye ukike ndani yake.

3. Nywele nzuri Kama Tausi
4. Midomo laini na minene kiasi Kama Paka wa Australia.

5. Pua nyembamba iliyochongoka Kama Mtusi
6. Meno meupe yaliyopangika
7. Mashavu laini yenye mashimo madogo Kama mashimo ya Suleiman

8. Shingo ndefu nzuri Kama Flamingo

9. Maziwa mazuri makubwa kiasi Kama nguva

10. Mikono laini yenye viganja na kucha nzuri

11. Kiuno kizuri chembamba Kama Dondola

12. Kitovu kizuri kilichoingia ndani kidogo Kama kitovu cha katuni.

13. Hipsi na matako makubwa yaliyojenga umbo namba nane.

14. Mapaja manene laini Kama Farasi.

15. Magoti laini, nyuma yakiwa na vishimo na vimichirizi vya kiuchokozi.

16. Miguu ya bia na unyayo wa wastani ambao akivaa kiatu anapendeza.

17. Kucha nzuri za miguuni ambazo akizapaka rangi anapendeza Kama Mbega

18. Masikio mazuri ya wastani akivaa hereni anavutia Kama mlimbwende wa kimataifa.

19. Sauti laini tamu, isiyochosha, Kama mwombaji WA sauti ya Kwanza peponi

20. Mwendo wake wa madaha na maringo Kama Twiga.

21. Tabia yake nzuri kama wanawake wa Sayuni

22. Akili zake za wastani zaongeza utukufu wake.

23. Vizinga vyake sio haba Ila sijali kwani kizuri chagaramiwa.

25. Elimu yake ya urembo na mapishi yazidisha sifa zake

26. Foleni ya washindani wangu kuwa kubwa wanaotaka kumchukua inanipa chachu ya kuona yeye ni wathamaani kwani kila mwanaume anamhitaji.

27. Siri ya kambi na ramani ya jeshi siwezi elezea hapa. Kwani anamkanda mweusi wa mapambano ya chumbani.

28. Maombi yake asalipo hushusha Malaika walioko mbinguni. Sio ajabu kwani huenda ni Malaika mwenzao.

29. Akinuna anazidi kuwa mzuri Kama kitu kizuri cha Kula Kama chocolate

30. Anapenda Ndugu zangu Kama ninavyowapenda ninyi Wakwe zangu.

Kufikia hapo, wazazi wangu naombeni mnikubalie niwe na binti yenu, tuunganishe undugu.

Ni taraji langu kuwa mtanikubalia kihalali.

Hata hivyo naahidi kuwa nitampenda, nitamtunza na kumthamini mtoto wenu siku zote za maisha yangu.

Nimeambatanisha na shilingi laki moja (100,000) ya kitanzania Kama kituliza koo baada ya barua hii ndefu.

Aliyeieleta barua hiyo ni Mjomba wangu, Dapshan Dube.

Wenu katika Uposaji
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa MOROGORO

Tusubiri majibu ya Barua Kama nitajibiwa au nitapigwa cha mbavu.

Nitayaweka hapahapa
 
Kwa maneno haya.. mahari umesamehewa.. beba uondoke naye...
 
Kitakachopona hapo ni laki tu! Ila barua chanachana! Mshenga tolewa nduki! Aaf namposaji bange zakuvutia matakoni umejifunzia wapi?
 
Sababu ni hii
Screenshot_20210511-230444~2.jpg
 
Na wakati wowote waweza ukageukwa
 
Kama ni kwetu unapigwa faini kwanza, afu mengine ndo yafuate kwa kuwa inaonekana umeshajuana kimwili na binti kabla hujapeleka barua kwa vidokezo hivi;

-unayajua mapaja na kitovu chake
- mkanda mweusi kitandani
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Unazingua mkuu.

Yaani kirahisi hivyo
Duh mkuu juhudi zote hizo bado unaona hajafanya chochote kiasi cha kumwambie eti kirahisi hivyo. Mpe moyo tafhari usimkatishe tamaa anaweza kujinyonga huyoo.
 
Kama ni kwetu unapigwa faini kwanza, afu mengine ndo yafuate kwa kuwa inaonekana umeshajuana kimwili na binti kabla hujapeleka barua kwa vidokezo hivi;

-unayajua mapaja na kitovu chake
- mkanda mweusi kitandani

😃😃😃

Mtaiambatanisha hiyo faini kwenye mahari.
Ilmradi binti yenu nimchukue
 
Back
Top Bottom