Barua ya Wazi kwa Bw. Macrice Daniel Mbodo Head PostMaster mteuliwa

Barua ya Wazi kwa Bw. Macrice Daniel Mbodo Head PostMaster mteuliwa

Uhakika Bro

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2022
Posts
3,644
Reaction score
4,315
Kwanza, tafadhali isome barua hii kwa niaba ya watanzania wote wanaotumaini katika ukuaji wa sekta ya posta nchini.

Tarehe: 2Sept2024

Kwa:
Bw. Macrice Daniel Mbodo
Postamasta Mkuu, Shirika la Posta Tanzania (TPC)

Mada: Pongezi na Ushauri kwa Nafasi ya Ukuu wa Posta Tanzania

Ndugu Bw. Mbodo,

Kwa niaba ya Watanzania wote, napenda kukupatia pongezi zetu za dhati kwa kuteuliwa kwako kuwa Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC). Nafasi hii ni ya heshima kubwa na pia yenye changamoto, lakini tunaamini kwa uwezo wako wa kipekee, utaweza kuleta mabadiliko chanya katika sekta hii muhimu.

Hii ni fursa adhimu kwa wewe kuleta mapinduzi ya kisasa katika Shirika la Posta. Tunaamini kuwa unaweza kubadilisha mtindo wa uendeshaji na kuhakikisha kwamba Shirika la Posta linakuwa mfumo wa damu wa nchi nzima, ambao utawezesha usambazaji wa mizigo na vifurushi kwa ufanisi wa hali ya juu. Kwa kufanya hivyo, utaweza kuunganisha wajasiriamali na wateja wao popote walipo nchini, na kuimarisha biashara ya mtandaoni kwa kutoa huduma bora na za haraka.

Usikilizaji na utendaji wako utakuwa na athari kubwa katika kuboresha huduma za posta nchini, na hivyo kuondoa utegemezi wa maelekezo ya muda maalum kama ‘nanenane effect’. Badala yake, kwa kutumia teknolojia ya kisasa na ushirikishaji wa taarifa na bidhaa masaa 24/7, utaweza kuhakikisha kuwa huduma za posta zinafikia wananchi wote kwa haraka na kwa ufanisi.

Tumeshuhudia ilivyo rahisi hivi sasa kupokea vifurushi kutoka nje ya nchi kupitia posta. Sasa tunaomba urahisi huohuo utumike katika mizigo inayozalishwa hapahapa nchini. Ifike hatua mkulima wa viazi wa Njombe na Mbeya anakusanya anayapeleka posta na yanafika Mwanza kwa gharama nafuu kabisa. Sijui kama inawezekana? Na hata tukiachana na viazi basi hata njasiriamali afunge ubuyu na sabuni kwenye kiboksi kidogo na mzigo umfikie mteja wake aliyeko mbali kwa gharama nafuu kabisa! Je nayo haiwezekani.

Ni masikitiko huduma ya usafirishaji vifurushi kutawaliwa na baadhi mashirika ya mabasi (ambayo hayajafikia uwezo wa kuwa na ofisi nchi nzima)wakati ambapo tungeweza kutumia vema miundombinu ya posta iliyopo kila wilaya na kuhakikisha ufikikaji wa jumla wa nchi na bara zima Universal access.

Tunakupongeza tena na tunakutakia mafanikio mema katika majukumu yako mapya. Tunatumaini kuwa utaendelea kuzingatia malengo haya na kuhakikisha kuwa Shirika la Posta linafikia viwango vya juu vya ubora na huduma kwa taifa letu.

Kwa pamoja tuijenge nchi yetu.

- Mdau

PIA SOMA
- Uteuzi Septemba 2, 2024: Rais Samia ateua na kuhamisha vituo vya kazi viongozi mbalimbali
 
Kumbe hiyo sehemu ya pia soma ni kazi ya maadmin..... okay kazi nzuri
 
Waziri anayetegemea posho za Vodacom,halotel,tigo atawaza uzalendo wa posta
 
Back
Top Bottom