Barua ya wazi kwa Dada yangu kipenzi

Barua ya wazi kwa Dada yangu kipenzi

Magical power

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2022
Posts
2,158
Reaction score
5,626
BARUA YA WAZI KWA DADA ANGU KIPENZI
1731101958708.jpg

Dada angu mwema, naipenda furaha yako nami sisiti kukuhusia katika yale niyafahamuyo mimi ambayo ni mambo mema kwenye maisha yako

1. DADA ANGU mwema mwanaume anayekupenda kwa dhati na anayekuwazia mema hawezi kukushawishi akulale kinyume cha maumbile. Hayupo mwanaume sahihi/bora anayekupenda sana na anayeijua thamani yako akakushawishi au akaongea ujinga huu. Hapo HAMNAMO mwanaume jiongeze hiyo ni mbuzi

2. DADA ANGU mwema hakuna mwanaume anayekupenda sana akakuambia nizalie mtoto kwanza ndipo nikuoe basi ukifanya hivyo🙌🏿😢 jiandae kuwa single mother uliyepumbazika na penzi la majaribio yaaani wewe ni MGALATIA

3. DADA ANGU mwema usipunbazike na penzi la mume wa mtu kisa anakulipia kodi ya nyumba, anakuhudumia huku akija hapo KUKUDINYA mchana na usiku anaenda kwa mke wake au mara mojamoja anakuja kulala hapo. Huku ukipambania eti aachane na mke wake akuoe wewe. Wewe ni MGALATIA kweli

FUMBA macho tukuombee wewe ni MGALATIA

4. DADA ANGU mwema, usiolewe na mtu kisa umezaa naye, amekusaidia kutatua changamoto yako, upweke au usiendelee kubaki kwenye mahusiano yaliyokufa kisa umezaa naye, mtoto haleti upendo utabaki kwenye maisha yake kama dada wa kazi.

5. DADA ANGU mwema, usikubali kutumiwa kimapenzi cha mwajiri wako (boss wako) ukajiona umeyawin maisha. Umeshapotea na utapoteza kujiamini na utakuwa adui wa wafanya kazi wenzako kwasababu utawaumiza

6. DADA ANGU mwema usiendelee kuzaa na mwanaume ambaye umeona kabisa haeleweki, anakwepa majukumu maana utakuwa na majukumu makubwa ya kulea pekee ako na ukiachika utapata shida kupata mwanaume atajayekuoa ukiwa na watoto wengi dada angu

Yawezekana umemuona haeleweki achana naye kama uko naye kwenye ndoa achana au punguza kuzaa linda thamani yako usije kujuta.
 
Back
Top Bottom