Barua ya wazi kwa DG wa TAKUKURU

dodomacity

Member
Joined
Jan 26, 2021
Posts
7
Reaction score
10
Kamanda heshima yako,

Napenda kukufahamisha kuwa tumekutumia email ya malalamiko dhidi ya maofisa wako wanajihusisha na vitendo vya rushwa. Email hii tuliyokutumia tumetumia dgeneral@pccb.go.tz. Tumeona tukutumie ujumbe kupitia jf hapa kwani tunaamini wewe unapitia hapa lakini pia uenda hiyo email husiipate kwani inaweza fika masijala na wakaipitisha kushoto. Kuna maofisa wako wa pccb ni wachafu. Tafadhali fuatilia.

Asante na kwa lolote kuhusu ushahidi tupo tayari.
 
Naamini atashughurika nao

Sent from my TECNO KD7h using JamiiForums mobile app
 

Mkuu chana na weka uchi hapaJF hatunaga kulemba, sema wapi, lini na wamefanya nini?
 
Waweza kuwa mzalendo wa kweli,ila tu itakuwa jambo jema kama nitaarifa ya kweli isiyokuwa na manufaa binafsi au majungu ndani yake,Tanzania ni yetu wote tuijenge kwa pamoja.
 
Bado hujafanya Jambo la Tija badala yake ungewataja hao Maofisa ( Watendaji ) wala rushwa wa PCCB tungekuona una Mantiki mno kwani huenda kuna Watu hapa JamiiForums wako Jirani na PCCB DG hivyo wangerahisisha Jambo lako Kumfikia kwa haraka na hata Watendaji wa Vyombo vingine kuanza Kuwafuatilia na hata Kuwachunguza.
 
Hujawa wazi...Taarifa si Ya GT,umeiweka kama mashairi Ya Wimbo tu tena wa Taarabu
 
Ndio matatizo ya kuajiri UVCCM kwenda PCCB au TISS au Polisi hakuna weledi na rushwa kuvuka mipaka.
 
Kuna tatizo hilo pia hata uhamiaji email hawasomi na hawajibu sijuiwaliweka za nini hazifanyiwi kazi hata kidogo....ukute malalamiko halali wao wanaita majungu.....watupe email ya mama tujue moja
 
Wewe ni mzalendo wa kweli. Kikubwa usiwe umewasingizia, wanaweza kuwa maofisa wenzio unawachoma ili upate hicho cheo, maofisini kuna mambo sana hasa ufanye kazi na kabila fulani hivi, wana majungu balaa!.
 
Tunakusihi mleta mada barua yako kwa DG wa pccb iwe imebeba "uwazi na ukweli". Na siyo "uwongo na ufitini"
 

d
Mimi nimshauri Cp Hamduni afanya reshuffle kwa makamanda wa pccb wilaya maana wengi wao wanabambika kesi yaani ni shida chombo jina kubwa ila majanga mama akiunde upya
 
Wanajf naomba radhi kwa kuchelewa kujibu hoja zinazohusu post yangu kwani nilikuwa mgonjwa wa kitandani kwa wiki mbili nikiwa hoi. Kiufupi ni kwamba maofisa hawa wako hapa bukoba mjini kwenye ofisi ya pccb mkoa ambao ni KILASA MALULU, TRYPHONE MAGOGWA, MBAGA, KAPERA na mtu mmoja hivi ana kovu shavuni pia akiwemo bwana John Joseph ambaye ni mkuu wao. Tumelalamika tangu mwaka 2019 mpaka sasa hakuna majibu, lakini pia tumetuma emails kibao bila majibu na wakati mwingine tumeomba tuombwe ushahidi lakini pccb hq haijawahi kututakisha ushahidi. Email zetu wanazo lakini wako kimya.
 
Kuna tatizo hilo pia hata uhamiaji email hawasomi na hawajibu sijuiwaliweka za nini hazifanyiwi kazi hata kidogo....ukute malalamiko halali wao wanaita majungu.....watupe email ya mama tujue moja
Uhamiaji ni shida, nilituma email kama mara 4 lakini hakuna majibu, hawajibu email wanazotumiwa.
 
Haya kawataja tayari hebu msidieni basi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…