Barua ya wazi kwa Diamond

wiseboy.

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2014
Posts
2,932
Reaction score
4,544
Mdogo wangu Diamond, umesahau ulikotoka, mafanikio yamekufanya hadi unamdharau baba yako mzazi, hata kama alikukosea vp, huna baba mwingine zaidi yake.

Mama yangu aliwahi kuniambia kuwa, baba ni baba tu hata kama ni chizi, umaarufu, kipaji na pesa vyote vitaisha na hutaamini kamwe, kila jambo na wakati wake, leo hii unawaona waandishi wakubwa wa riwaya kama kina shigongo, kabla yao walikuwepo wengine kama kina Elvis Musiba na Ben Mtobwa, shigongo na wewe wote mtatoka kwenye game watakuja wengine nao watafunika vibaya.

Dunia ni gunia, usidhani kuwa wewe utatamalaki milele, muda si mrefu utafutika kwenye game, hao mademu zako kina wema, meninnah, penny na wengine, hakuna anayekupenda kwa dhati hata mmoja mdogo wangu, wanakupendea umaarufu wako na pesa ulizofanikiwa kupata.

Ungekuwa unasukuma mkokoteni au kupiga debe kwenye daladala kamwe usingewaona hao warembo dogo, jirekebishe haraka, ukamuombe na msamaha baba yako, pia uwe unampatia matumizi kama ufanyavyo kwa mama yako, hapo MUNGU atakubariki sana na hakika utadumu sana kwenye game
 
Naona huku unaangaika sana kama kweli unampenda na nia yako nikutaka suluhu ungekwenda kwa Mamake Diamond,na vile vile ningekua huyo Babake ningekaa kimnyaa kwani hata kunyamaza pia NENO..........
 
Ushauri huo kwanza mpe baba akaombe msamaha kwa Kumtelekeza mtoto.Huyo Mungu wa kumuadhibu Diamond kwa kosa gani?Asimuadhibu baba aloshindwa kumuonesha mapenzi mtoto.

Alafu mambo yake na Baba inatakiwa aambiwe na mama yake mzazi kwani ndi mwenye kujua baba wa mtoto.

Huyu baba nae hana tofauti na uliowataja hapo juu kwani angekua teja wa Tandale angejitokeza? Au baada ya Diamond kutoka ndo kapima DNA nakujua kuwa ni mwanae?

Ukishajiuliza hayo ukajifunze kuandika barua.
 


Baba akaombe msamaha kwa mwanae, kisa? ana pesa - I doubt!
 
Naona huku unaangaika sana kama kweli unampenda na nia yako nikutaka suluhu ungekwenda kwa Mamake Diamond,na vile vile ningekua huyo Babake ningekaa kimnyaa kwani hata kunyamaza pia NENO..........

Word..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…