Barua ya wazi kwa mheshimiwa Raisi.

Barua ya wazi kwa mheshimiwa Raisi.

Joined
May 27, 2017
Posts
39
Reaction score
27
Jemedari yeyote ambaye askari wake wa chini hawamuelewi ni vigumu kushinda vita.
Ili kushinda vita unahitaji mambo mengi,na kubwa kuliko yote ni morali,wasaidizi wako wanafanya kazi za kinafiki ,ndani ya miiyo yao kuna chuki kubwa dhidi yako na wateule wako wachache, na liliotokea Zimbabwe liwe fundisho kwako, bahati mbaya ukiwa mamlakani masikio hutiwa pamba na nguvu ulizonazo.
Baada ya mukhtasari huo hapo juu ,nataka kukusaidia juu ya azma yako ya viwanda.
1.Soko
Tanzania imekaa vizuri kijografia kuliko nchi nyingi katika ukanda huu.
Kutokana na jografia, ni lazima kuanzisha juhudi za makusudi kuifanya Tanzania kuwa soko la bidhaa tofauti tofauti kabla ya kuamua ni aina gani ya bidhaa ushugulike nayo zaidi.
Tanzania haina kiwanda hata kimoja cha kutengeneza magurudumu ya magari , kwa nini usiweke ushuru zero tariff.
kwa kuifanya tairi kuwa rahisi utavutia wanunuzi kutoka nchi zote jirani kuja kununua bidhaa hiyo hapa Tanzania.
Faida itakayo patikana ni mafuriko ya wanunuzi kuja Dar es salaam. Wanunuzi.

watakula
mchele kutoka kahama,Nyama toka shinyanga,nyanya toka Iringa,maji toka Bakhresa n.k

Watalala
ajira kwa vijana waliosomea hotel management

Taxis
kwenda na kurudi katika mizunguko yao

Bandarini
karibu wafanyakazi wote ni Watanzania na matumizi yao yatarudi kwa wenzao wa tandika na manzese.

Kwa ufupi kitendo cha kuacha kushughulika na tairi pekee ime sababisha multiple effects katika uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa jumla, je tukifanya hivyo kwa bidhaa zote ambazo tunaona hatuna uwezo wa Ku compete na mataifa makubwa yenye cheaper source of energy and more sophisticated technology?
Ni matarahio yangu utaondoa pamba masikioni ili utimize ndoto yako.
Kupanga ni kuchagua
 
Back
Top Bottom