Mganguzi
JF-Expert Member
- Aug 3, 2022
- 1,604
- 3,715
Ndugu Tundu,
Nakuandikia barua hii ya wazi, kwa afya na mustakabali wa taifa letu na hali ya kisiasa ilivyo sasa nakusihi uachane na wazo lako la kugombea urais tena mwaka ujao!
Na badala yake nenda bungeni ukatusaidie kuliamsha bunge letu ambalo linaonekana limekufa na ndio chanzo cha miswada mibovu kupitishwa!!
Wekeni nguvu kwanza bungeni, ikulu iacheni kwanza mtapata mgombea siku zijazo, lakini nchi itapata nafuu kubwa sana ikiwa wewe, Mnyika, Mbowe, Sugu, mkarudi bungeni.
Tatizo kubwa kwa sasa linaanzia bungeni na sio ikulu!! Labda unaweza kugombea urais lakini mwisho tukaishia kusema kura zimeibiwa tukajikuta tunakosa vyote!!
Tuweke mgombea urais kwa nia ya kujizolea viti vingi bungeni!!
Mwisho ni kuhusu mvuto wako kwa nafasi ya urais ni tofauti na 2020, kwa sasa hali ni tofauti, jaribu kutathmini kwa kina utaelewa ninachomaanisha!!
Kama Chadema inaweza imshawishi Job Ndugai agombee nafasi ya urais hapo angalau litakuwa ingizo jipya linalosisimua.
Ni hayo tu!
PIA SOMA
- Kuelekea 2025 - Lissu athibitisha kuandika barua ya kugombea Urais, asema CCM wameweka fedha katika Akaunti yake, tatizo liko wapi?