Barua ya wazi kwa ndugu Zangu: Tuamue kupambana

Barua ya wazi kwa ndugu Zangu: Tuamue kupambana

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2013
Posts
10,931
Reaction score
24,816
Najua pengine naweza jisababishia maneno ya kebehi na dhihaka lakini sitoacha kusema kile nikifikiriacho kwenu ninyi ndugu zangu.

Waafrika tumekuwa tukifaulu katika kushindwa toka karne na karne.nguvu zetu zimekuwa ni udhaifu wetu. Na kwa kuwa tumeshindwa kujitathmini na kumtafuta wa kumsukumia udhaifu wetu kamwe hatutabadilika.

Africa hii toka tangu na tangu imekuwa na udhaifu katika mioyo.ujasiri katika nyuso na unafiki ktk ndimi.

Afrika miaka kadhaa baada ya Uhuru bado tumeonesha kutokomaa kisiasa na kiakili. Nliwahi pingana sana na mwandishi Nguli na Msomi Walter Rodney kwenye kitabu chake HOW EUROPE UNDERDEVELOPED AFRICA. nikitamani kitabu hicho kingepigwa marufuku katika vitabu vya historia ya mwafrika.

Ni kitabu kinachotoa faraja ya kushindwa kwetu kwa kupata sababi ya udhaifu na umaskini wetu miaka na miaka.kama mpaka leo nchi za kiafrika zitaendelea kulalamika na kusingizia ubeberu hiyo ni alama ya kushindwa daima.

Kama tutauana na kusingizia mataifa ya magharibi ni kudhihirisha kuwa bado hatujapata wasaa wa kutafakari akili zetu.

Ni wendawazimu kuamini kuwa kuna Taifa litakaa kuangalia maslahi ya taifa lingine pumbavuh ambalo halijataka kujitambua. Haya maisha ni ya surival for the fittest why tuamini kuwa kuna Taifa litataka kuona afrika inaendelea kuliko lenyewe?

Miaka ya kuuliwa P.Lumumba, Sankara,Kwame N etc afrika ilifanya nini kulipiza kisasi?ilijikumbatia na kuki ikiomboleza kama ilivyokuwa miaka ile wazungu na waarabu 20 wanapokuja katika vijiji kukamata mamia ya waafrika shababy kabisa kuwapelekea utumwani.

Bado miaka 50+ baada ya uhuru afrika ni maskini na kilio kile kile cha kunyonywa na mabeberu.

Waafrika tunauana tukigombea madaraka na viongozi wetu kunilimbikizia mali,kujipendelea au kupendelea tabaka flani.vinatokea vita kutokana na uvunjaji wa katiba na uchu wa madaraka then tunawalaumu wabeberu?nani katuroga?

Ina maana afrika mpaka leo hii inashindwa kutambua lipi baya na lipi zuri mpaka kugombanishwa?

Tumeamua kupambana na wazungu na waarabu kwa kusema adamu alikuwa mweusi,Yesu alikuwa mweusi,Muhamad? Sijui. Tumekuwa tukijikita katika kutafuta usawa wa kimtizamo na kusahau usawa wa Kiuchumi.

Kama Yesu alikuwa mweusi,weusi walijenga pyramids na adamu alikuwa mweusi hivyo vitu vimeisaidia nini afrika kwa sasa? Ni mataifa mangapi yana nuklia afrika?yamevumbua na kukuza teknolojia flani?

Ni aibu hao wanaoponda mabeberu wanatumia magari ya mabeberu,suit,simu,tv,saa,viatu na mambo mengi from mabeberu.huo uafrika wetu ni upi?

Tunapata wapi nguvu ya kwenda omba msaada kwa mataifa ambayo yanatusimanga?afrika imekuwa dhaifu mpaka udhaifu umekuwa afrika.

Tunapokemea kitendo cha mzungu kumua George Floyd tunasahau maelfu ya watu tunao waua huku kwetu afrika. Tunasahau kabisa kuwa askari wetu huua na kutesa waafrika wenzao. Hapo tunasimama na kuona ni sawa tunapoua watu waliotofauti nasi kimtizamo.kama ambavyo wengine wanaua walio na tofaut nao kirangi.

Vita katika afrika vimeua watu wengi. Kuliko wazungu walivyoua huko kwao.tumeuana wenyewe kwa wenyewe kwa upumbavu wetu na kusingizia wazungu.

Afrika ifikie hatua ikubali kubadilika.wakati sisi tunalia lia na kulalamika wenzetu wanasonga mbele.
 
Chochote Kinachotokea Katika Maisha Yako, Muhusika Wa Kwanza Ni Wewe.
Sasa Afrika Yetu Hii Kila Kinachotokea Tunatafuta Mahali Pa Kuelekeza Lawama Zetu. Maana Yake Hatutaki Kujiwajibikia, Tunasubiri Kuwajibikiwa.
Ni Ajabu Kusubiri Tatizo Lako Lije Kutatuliwa Na Mtu Mwingine.
 
Watawala wetu wamemfanya mzungu mbuzi wao wa kafara ili kuficha madhaifu yao na kibaya zaidi wametengeneza magenge ya kihuni kuunga mkono maneno yao yanayolenga kughiribu akili za wananchi waone kweli wazungu ni chanzo cha matatizo yao..wengine wanakuja sio muda mrefu kukupinga.
 
Back
Top Bottom