msani
JF-Expert Member
- Jun 13, 2011
- 1,801
- 1,191
Mheshimiwa Rais Hussein Mwinyi, nakuandikia hapa kwa sababu nahisi ndio sehemu pekee ujumbe unaweza kukufikia.
Sisi wafanyabiashara mara nyingi huwa tunakopa fedha benki ili kuendesha biashara zetu, na sisi kama wengine tumekuwa tunakopa mara nyingi na kufanya valuation ya mali zetu kama dhamana benki. Tulikuwa tunalipa Approval Fee ya serikali ambayo ni ni 0.02% ya thamani ya mali husika. Lakini hivi majuzi nilifanya zoezi kama hili na nikaambiwa kwamba ada hiyo sasa hivi ni 0.3% kutoka ya awali ya 0.02%.
Property yetu ina Market Value ya TZS 21 Bilioni ambapo awali nilikuwa nalipa Approval fee ya takribani TZS 4,200,000 lakini majuzi hapa nililipa takribani TZS 50M ili Mthamini mkuu wa serikali aidhinishe hizo ripoti na mambo yangu yasikwame lakini bahati mbaya mkopo wangu haukufanikiwa na benki ikabidi nihame benki na zoezi la uthamini lianze tena upya ambapo sasa natakiwa kulipa TZS 63M ili waidhinishe hii ripoti kama takwa lakisheria.
Mheshimiwa Rais, hiki ni kikwazo kwa ukuaji wa kibiashara hapa Zanzibar, hili halina afya kibiashara kabisa. Tanzania Bara tunafanya biashara kama hizi pia lakini tunalipa Approval fee ya Valuation ya 0.02% na sio hii dhulma tunayofanyiwa hapa Zanzibar.
Hii imetengeneza mwanya wa rushwa kwa ofisi hiyo ambapo watu wanalipa pesa kidogo ili kukwepa hicho walichokiweka. Imetenngenezwa mwanya wa rushwa na mkwamo wa kibiashara kwa sababu ili kupunguza hizo gharama basi inabidi kukaa na kuzungumza na kulipa kiasi Fulani ambacho hakiendi serikalini, bora ile ya 0.02% ilikuwa inafika serikalini. Hata ukifanya uchunguzi leo kwa ripoti zilizofanyiwa Approval kwenye mabenki uangalie kama kuna pesa imeingiwa sawa sawa na hizo ripoti, utakayoyakuta utshangaa.
Tunaumia sana, tunakuomba sana uingilie kati uliangalie na ikikupendeza basi ulitolee maelekezo.