Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
- Thread starter
-
- #21
Mwanakijiji,
Inaonekana huyu kijana ana kiburi na ujeuri wa makusudi, kuwalinda wahalifu na marafiki zake, kama anashindwa kukemea chochote bongo basi Zimbabwe itakuwa ni sikio la kufa kwake.
Gm
Jenny Booth said:
The bodies of four opposition activists are reported to have been found near the Zimbabwean capital Harare this morning, as violence escalates ahead of next week's election.
The Movement for Democratic Change, Zimbabwe's main opposition party, said that four of its youth members were abducted on Tuesday. Their bodies were found discarded in different places around Chitungwiza, southeast of Harare.
The deaths come hours after Thabo Mbeki, the South African President, flew to Zimbabwe to urge Mr Mugabe to cancel next week's vote and negotiate a deal with the opposition in a bid to control the violence.
The MDC said that latest bodies brought to around 70 the total number of its
activists, their spouses and children who have been murdered by Zimbabwe's
security forces and government supporters since the first round of the
presidential election on March 29 failed to yield a conclusive result.
Nelson Chamisa, an MDC spokesman, said that the party suspected that the
latest victims had been beaten to death after being attacked at a local
councillor's residence by youth supporters of President Mugabe's Zanu-PF
party, armed with clubs and whips. "Now it's about 70 we've lost," said Mr Chamisa. "The situation in the country is getting worse. A free and fair election is impossible." The MDC says the ruling party unleashed an army-led campaign of intimidation against opposition voters after the first vote, in which its party leader Morgan Tsvangirai defeated Mr Mugabe but fell short of an outright majority.
Mr Tsvangirai has said that Zimbabwe is now run by what is essentially a "military junta".
Until the last week the violence has mainly been confined to rural areas, but the most recent attacks have taken mob action from poor townships into
prosperous suburbia. In the past week, the wives of at least three MDC officials has been murdered. Abigail Chitoro, 27, the wife of Harare's recently elected MDC mayor, was so badly beaten by the mob that dragged her and her four-year-old son from their home that even her brother-in-law struggled to identify the body. The clothes she was wearing, her distinctive haircut and the blindfold that Zanu (PF) supporters forced her to wear as they firebombed her home gave the only clue to her identity. The child was dumped alive at a police station.
The UN has blamed Mr Mugabe's supporters for most of the attacks.
Mr Mugabe, however, has blamed the MDC for the mounting violence ahead of the June 27 run-off, and has threatened to arrest opposition leaders over
it. Mr Mbeki met Mr Mugabe and Mr Tsvangirai separately in Zimbabwe yesterday to try to mediate an end to the increasingly violent crisis.
South Africa's Business Day newspaper, a respected financial daily, quoted
unnamed sources as saying that Mr Mbeki tried to set up a meeting between
the pair - their first ever - but did not receive a firm commitment from
Zimbabwe's president.
Wakuu
Matatizo yanayoikumba Zimba si kosa la Mugabe.
Mutakumbuka matatizo yameanza baada ya wazungu kufukuzwa,hivyo basi inaodhihirisha ni jinsi gani wazungu walivyo wanoko na washenzi hadi wakacreate dudu la uhakika lililozaa matatizo yooote haya muyaonayo zimbabwe.
Neno moja nalolitaka kwenu watanzania ni kutafutia njia ya kumsadia mugabe na watu wake waondokane na hali mbaya ya kiuchumi then maissue ya siasa yafute.
Hata huyo Tsava akichukua nchi bado ni kibaraka tuu wa wazungu,hakuna jipya,zaidi ya ukoloni mpya.
Na ni Mwalimu huyo huyo ambaye alizungumzia suala la "uraia" baada ya Idi Amin kuanza kuhoji uraia wa waasia wa Uganda na kuanza sera zake za kibaguzi kule. Mwalimu alizungumza siku ile August 21, 1972 pale Chuo cha Ualimu Chang'ombe, Mwalimu alisema hivi "Afrika lazima ikatae kudhalilishwa, kunyonywa, na kusukumwa sukumwa. Na kwa moyo huo huo ni lazima tukatae kuwadhalilisha, kuwanyonya, na kuwasukuma sukuma wengine. Ni lazima tutende siyo maneno tu".
Matatizo ya Zimbabwe yamesababishwa na Mugabe, period. Alianza kufanya unyama dhidi ya Matabele kwa vile walikuwa wako upande wa Joshua Nkomo. Aliwakumbatia veterans alipoona wameanza kumhoji kwa nini anawapendelea watu ambao hawakuhusika na mapambano, hususan, mke wake Grace. Si tu aliwanyang'anya mashamba bali aliwaondoa wazimbabwe weusi waliokuwa wakifanya kazi na kuishi kwenye mashamba hayo na kuwapa cronies wake ambao hawana utaalam wa kilimo. Wakati wa visingizio umekwisha. Matatizo haya ameyaleta mtu mweusi mwenzetu. Tusimuonee haya.
Nyerere alisimama kidede kumpinga Idi Amin hata pale wenzake walipompa uenyekiti wa O.A.U! laiti Idi Amin angechukua nchi wakati huu, bila shaka angeendelea kupeta!
Ni hawa viongozi wetu wakati wenzetu wanauawa huko Darfur walikuwa karibu wampe uenyekiti wa A.U. rais wa Sudan. Mpaka hapo tutakapoweza kusimama na kuwekana sawa wenyewe dunia itaendelea kutuona ni vikaragosi!
Mungu alinusuru bara letu. Mungu awanusuru wazimbabwe. Kama alivyosema Robert Nesta Marley " Afrika liberate Zimbabwe....."
Fundi, we have wrote countless of times here..the worst enemy of Africa are Africans. Huna haja ya kuanza kurevisit history. Facts are out there for everybody to see..anayekubali au anayekataa..mwache. Ila Mugabe anapigana na Ukuta! No society can suffer permanently!
MWanakiji Milosevic na Mugabe ni mambo mawili tofauti,Mie Mugane kwa upande mmoja simuungi mkono,hasa katika mambo yanayohusu kuendeleza Uchumi wa Nchi ya wazimbabwe.It is about time to the West should start declaring certain individuals in Zimbabwe armed forces as war criminals. Na kama alivyofanyiwa Slobodan Milosevic saa ya Mugabe nayo inafuatia. Huwezi kuwatenda watu wako hivyo na ukaendelea kutawala.
21 June 2008
Posted to the web 21 June 2008
A parliamentary committee yesterday endorsed the Government's tough stance on Zimbabwe, saying it fully supports the official sentiments of the members of the Southern African Development Community (Sadc). The chairman of the Parliamentary Committee for Foreign Affairs, Security
and Defence, Mr Wilson Masilingi, said they agreed with the official denunciation of the state-sponsored violence just a week before the election
run-off pitting President Robert Mugabe against MDC candidate Morgan Tsvangirai. The statement issued by the MP for Muleba at the National Assembly in Dodoma was in response to Foreign Affairs and International Co-operation minister Bernard Membe's warning in Dar es Salaam on Thursday that Tanzania was appalled by President Mugabe's style, which threatened to plunge the country into chaos.
Nominated MP Anna Abdullah said that while the Government's statement was positive, it had, however, taken too long for it to denounce the breakdown of law and order and condemn the rampant human rights abuses in Zimbabwe. Speaking to The Citizen, Mr Masilingi and Ms Abdullah said that "even though Zimbabwe is a sovereign state, Tanzania has a historical stake and can, therefore, not keep quiet as that country spirals into anarchy".
Earlier, in her contribution to the Budget debate, Ms Abdullah said: "It's good that the Government has issued a condemnation of Zimbabwe even though
this should have come earlier. Tanzania, as the current chair of the African Union, must be in the forefront in condemning what is going on in Zimbabwe."
Later, she told The Citizen that President Mugabe deserved to be condemned by his fellow African leaders for trying to cling to power by force. "Our country supported Zimbabwe's struggle for independence but it was not so that he could become the President for life," she said. Zimbabwe, she added, was neither a chieftainship nor a kingdom. "Democracy and the rule of law must be respected," she said, denouncing recent reports that quoted Mr Mugabe and his wife, Grace, threatening not to hand over power should he be defeated in run-off poll.
Mr Masilingi said he had been shocked by a report of the Sadc political committee, which confirmed gross human rights abuses and mounting insecurity against the people of Zimbabwe and election monitors. "We share the Government's concern and urge the relevant organs of the Sadc member countries follow closely all that is happening in Zimbabwe." The MP said President Mugabe must cooperate with fellow regional leaders to make sure the re-run election was free and fair. "It is in the interest of the people of Zimbabwe as well as the region to have peaceful and democratic elections," Mr Masilingi said. In an indication that gone are the days when Zimbabwe took Tanzania's support for granted, Foreign minister Membe on Thursday cast doubt on the possibility of a free and fair election on June 27.
He told journalists in Dar es Salaam: "I want to tell you what I told fellow Southern African Development Community (Sadc) members. We have got evidence that the elections will not be free and fair." He added: "Zimbabwe has been our great friend. We have stood by them since the Lancaster agreement on land issues in 1980, but on governance issues, we have started to differ with the incumbent president." Last week, President Mugabe vowed to "go to war" to prevent the Movement for Democratic Change from taking power - as the race for the presidency entered its final phase. "We are prepared to fight for our country and to go to war for it," he told a rally of cheering supporters.
Bunge Backs Tough Stand On Zimbabwe
A torture victim is given treatment for his burns in a hospital in Harare, Zimbabwe. He was set on fire by suspected Zanu PF militia
Assassins Aim at Zimbabwe Opposition
http://graphics8.nytimes.com/images/2008/06/22/world/22zimbabwe-span-600.jpg[/img[/CENTER]]
[B][SIZE="4"][COLOR="Lime"]Killer Robert Mugabe anataka kuongoza vipofu na walioungua na moto ambao hawawezi kukaa chini.[/COLOR][/SIZE][/B][/QUOTE]
Kama wakati wote suspect ndio mkosaji...pengine hatuna haja na mahakama!
I don't think if it is fair or reasonable to conclude every statement/action by Mugabe goverment is wrong and every statements by MDC and supporters is correct.... so far we know MDC is saying ZANU-PF is violently targeting its supporters and Mugabe goverment is saying MDC is behind the violence.
Mambo ya Kenya yalikua tofauti kidogo, lakini inasemekana watu zaidi ya 1,000 walikufa....lakini inashangaza kuona hakuna kilichofanyika kwa victims.
Pengine ilikua ni jinsi ya kujustify stakes and need for GNU without rerun.
Soma habari kwa undani:[url]http://www.talkzimbabwe.com/news/128/ARTICLE/2744/2008-06-20.html[/url]
Na. M. M. Mwanakijiji
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
YAH: Iongoze Afrika kupinga utawala wa kidhalimu wa Robert Mugabe
Naomba husika na kichwa hicho cha habari;
Hivi hadi nini kitokee ndipo viongozi wetu wataona kuwa kinachoendelea Zimbabwe ni aibu ya bara letu, na udhalilishaji wa utu, hadhi, na tunu ya mwafrika? Ni mpaka nini kifanyike ndipo tutaweza kuchukua msimamo wa kupinga uvunjaji mkubwa wa haki za binadamu, na kuchukua msimamo ulio dhahiri dhidi ya Robert Mugabe? Kwanini Tanzania nchi ambayo inadai katika Katiba yake kuwa "kila mtu anastahili haki ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake" ifumbie macho utu wa wana wa Zimbabwe ambao wanateswa katika mikono ya utawala wa kidhalimu wa Robert Mugabe?
Inakuwaje wanasiasa wetu na wabunge wetu wanashindwa kutoa msimamo wa kulaani kauli za kidikteta ambazo zimekuwa zikitolewa na utawala wa Robert Mugabe? Hivi kweli tunahitaji wazungu kutuonesha kuwa kinachotokea Zimbabwe hakina mfano wa haki za binadamu? HIvi kweli tunataka hadi Amnesty International na Human Rights Watch waje na kutuambia kuwa ya Mugabe ni uovu uliokithiri?
Je tumekuwa watii na wenye kuheshimu sura za watu kiasi hiki hadi tunaogopa kumwambia kuwa "tunashukuru kwa mchango wako lakini kwa hili tunakukana"? Je hakuna watu waliofanya mambo mazuri huko nyuma na katika maisha yao ya baadaye wakaharibu na historia zao zikatajwa na nyota pembeni?
Wale wanaolalamikia ukiukwaji wa haki za binadamu kule Palestine, Iraq na Afghanistani, walioandamana ujio wa Bush na ambao wakitetea haki za watu wa huko wako wapi leo hii wakati ndugu zetu wanaishi maisha ya wasiwasi na hofu kubwa chini ya mkono wenye kucha ndefu zichomazo wa Robert Mugabe?
Wakati umefika kwa viongozi wetu kuacha mazingaombwe ya diplomasia ya ukimya ambayo kimsingi ni ukimya wa kidiplomasia. Ni ukimya ambao unaendelea kutoa kibali kwa Utawala haramu wa Robert Mugabe kuendelea kutesa wananchi wa nchi hiyo. Je sisi Tanzania ambao tuliwahi kukiri katika imani zetu kuwa "binadamu wote ni sawa, na Afrika ni moja" leo hii tuko wapi?
Mch. Martin Luther King alipoandika barua yake kutoka Jela ya Alabama alisema wazi kuwa "udhalimu mahali fulani, ni udhalimu mahali pote" Je tunaweza vipi kukaa katika "kisiwa cha amani" wakati ndugu zetu wanateseka na kufanywa wakimbizi katika nchi yao wenyewe. Kwanini kina Morgan na wenzao waonekane si wananchi wa Zimbabwe kweli kwa sababu tu wanataka kuiokoa nchi yao?
Nini ambacho utawala wako unaogopa kusema na kufanya mbele ya Robert Mugabe? Hivi tukimtolea uvivu na kumuita kwa jina lake kuwa ni dikteta na kusema kuwa yanayofanyika Zimbabwe hayana nafasi katika bara la Afrika Mugabe atasema nini? Atatufanya nini? Hii heshima ya wazee ni heshima kweli wakati mzee anasimamia ubakaji na utesaji wa watu wake?
Naomba kutoa wito wa wazi, wa moja kwa moja na usio na utata kwako uwa Mhe. Kikwete kama Rais wa Tanzania, nchi ambayo imetoa na kulipa kwa damu ili nchi hizi za kusini mwa Afrika ziwe huru, asimame sasa na kusema "kama kutosha inatosha". Rais Kikwete ukiwakilisha mawazo ya kizazi kipya uungane na Botswana kwa kumwita Balozi wa Zimbabwe nchini na kuonesha kutokufurahishwa na yanayoendelea Zimbabwe.
Zaidi ya yote, Rais Kikwete akiwa ni Mwenyekiti wa AU aitishe mkutano wa haraka kati ya Morgan na Mugabe Jijini Dar (na si mtu mwingine nje yao) ili kujadiliana na kukubaliana jinsi uchaguzi wa marudio utakavyokuwa na kupata uhakika kuwa kila mmoja wao ataheshimu matokeo ya uchaguzi huo. Kikwete anaweza kufanya hivyo kwa kutumia kivuli cha NEPAD ambamo ndani yake kuna "African Peer Review Mechanism". Huu ni wakati wa kuonesha uongozi.
Na endapo Mugabe hatokuwa tayari kusikiliza ushauri wa rafiki, basi wakati umefika wa kuvunja uhusiano wetu wa kidiplomasia na Zimbabwe. Itauma, lakini inabidi.
Nikukumbushe maneno ya Rais Nyerere kwenye mkutano wa Jumuiya ya Madola mwanzoni mwa miaka ya sitini ambapo hoja ya kukubali kuiingiza Afrika ya Kusini katika jumuiya hiyo. Nyerere alisema wazi kuwa kwa kadiri ya kwamba siasa za kibaguzi zilikuwepo Afrika ya Kusini basi Afrika ya Kusini haiwezi kuwa mwanachama. Na akatamka yale maneno mashuhuri ya msimamo wa kiongozi mbele ya Malkia "Mkiwapigia kura kuwaingiza Afrika ya Kusini, mtakuwa mmepika kura kututoa sisi". Na hoja ya Mwalimu ikashinda.
Na ni Mwalimu huyo huyo ambaye alizungumzia suala la "uraia" baada ya Idi Amin kuanza kuhoji uraia wa waasia wa Uganda na kuanza sera zake za kibaguzi kule. Mwalimu alizungumza siku ile August 21, 1972 pale Chuo cha Ualimu Chang'ombe, Mwalimu alisema hivi "Afrika lazima ikatae kudhalilishwa, kunyonywa, na kusukumwa sukumwa. Na kwa moyo huo huo ni lazima tukatae kuwadhalilisha, kuwanyonya, na kuwasukuma sukuma wengine. Ni lazima tutende siyo maneno tu".
Mhe. Rais, Afrika inadhalilishwa na vitendo vya Mugabe na mashabiki wake. Afrika inafanywa duni kwa viongozi kama yeye. Ni kweli tuna matatizo yetu Tanzania, nafahamu tuna kashfa zetu za mambo ya fedha nchini na uongozi wa kishkaji; nafahamu wazi kabisa ndani ya CCM na serikali kuna kubebana na kulindana. Lakini ukweli ni wazi kuwa hatujafikia walipofikia Zimbabwe, hatujafikia mahali pa kufanyana vibaya kiasi cha Zimbabwe. Ni kweli tuna matatizo yetu lakini tukiyaweka ya Zimbabwe upande wa pili, ya kwetu yanaonekana ni kheri tupu!
Sisemi upuuzie matatizo yetu, sitoi ushauri kuwa ya kwetu kwa vile ni madogo basi usiyafuatilie. La hasha, ninachosema ni kuwa chukua msimamo kama kiongozi na kwa niaba ya wale waliotangulia mbele ya haki, kwa niaba ya wale waliomwaga damu yao kukomboa bara letu, usimame na kumwambia Mugabe inatosha na saa na wakati wake umepita aamue kujiuzulu na kustaafu kwani yeye kama wanadamu wengine, atakufa tu, na Zimbabwe itatawaliwa na mwingine. Mugabe hana ubavu wa kuzuia hatima ya nchi hiyo, na siku moja wengine watasimama mahali pake.
Akiamua kuachia ngazi sasa na kufanya mapatano ya kisiasa na wale walioumia chini yake, labda historia itamuonea huruma. Lakini Zimbabwe haiwezi kuendelea jinsi ilivyo, huku sisi rafiki zao na ndugu zao tukikaa nje kuangalia. Mhe. Rais, onesha msimamo sasa, na uliongoze Taifa letu kuchukua msimamo dhidi ya Mugabe ili tuwape nafasi ya ndugu zetu wa Zimbabwe ya kuishi katika nchi ya amani, utulivu, na mshikamano.
Sijaomba vingi, lakini hilo nakuomba kwa machozi.
Nimalizie kwa kukumbusha maneno haya ya baba wa Taifa tena alipozungumza mwaka 1959 kwenye mkutano ule uliofanyika Uingereza Juni 26 (karibu miaka 50 kamili iliyopita). Katika mkutano huo uliokuwa unazungumzia Afrika ya Kusini na utawala wa Makaburu Mwalimu alisema maneno haya "Serikali ya Afrika ya Kusini inapigana na historia, ni wao watakaoshindwa. Tunafahamu harakati za ukombozi zitafanikiwa katika Afrika ya Kusini. Kama tunajiamini tutashinda".
Mheshimiwa, Mugabe anashindana na historia na kwa hakika atashindwa; harakati za mabadiliko ya kisiasa yanayoendelea yatafanikiwa, na kama sisi sote tunajiamini kwamba tuko sahihi basi tutashinda. Tuongoze katika hili kwani bwana mdogo kutoka Botswana ameshaonesha njia.
Wasalaam katika Kuliinua Bara letu
M. M. M.