Barua ya wazi kwa Rais Samia Suluhu Hassan: Umenena vyema suala la PF-3

field marshall1

JF-Expert Member
Joined
Sep 17, 2017
Posts
1,171
Reaction score
2,732
Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, Kwanza napenda kukupongeza kwa hotuba yako nzuri wakati wa ufunguzi wa kiwanda cha kutengeneza au kushona nguo cha jeshi la polisi.

Nilivutiwa na jinsi ulivyosema kuhusu matumizi ya PF-3 kwa wagonjwa wanaoumia au kupata ajali za barabarani na ni ukweli usiopingika kuwa wengi wa wananchi wanapoteza maisha kutokana na urasimu (bureaucracy) ya system ya kijinga ambayo sijui ilikopiwa wapi.

Kweli mtu anaumia kwenye ajali, anaumizwa na majambazi kwa kupigwa risasi au kuchomwa kisu au ajali yoyote ile iwe ya moto au majanga mengine halafu anapelekwa hospitali anaambiwa hadi apate form ya PF-3? Hivi huu ujinga umetoka wapi?

Tumechelewa sana, wananchi wengi wamepoteza maisha kama ulivyosema mheshimiwa rais, na kama ni sehemu nyingine, ndugu zao walipaswa walipwe fidia kwa uzembe wa hali ya juu wa serikali yetu.

Kwa mapendekezo kama mwananchi, ningeshauri hospitali zote nchini hadi vituo vya afya viwe na sehemu ya EMERGENCY CARE kwa ajili ya kuwakimbiza wanaoumia au wenye shida ya magonjwa hatari ili maisha yao yaweze kuokolewa, tofauti na sasa ambako hospitali zetu hazina hizo huduma za dharura, hivyo unakuta mgonjwa anaambiwa asubiri kitanda hata awe na maumivu kiasi gani au awe mahututi kiasi gani.

Mara nyingi tunasikia mwananchi amekimbizwa hospitali lakini kabla hajaanza kushughulikiwa akapoteza maisha, sababu ni hizo kuwa hatuna hizo huduma muhimu ambazo zipo duniani kote hata hapo Kenya zipo lakini sisi hatuna.

Kwa vile umeona hayo mheshimiwa rais, tunaomba utamke kuwa hayo mambo ya PF-3 yaishe, kwani polisi wana uwezo wa kwenda kumhoji mhanga wa tatizo hata akiwa hospitalini akipokea matibabu.

Pili kuhusu polisi na IGP wao, ni wazi kuwa hili jeshi bado lina tatizo kubwa, kwa mawazo yao ni kwamba wapo kudhibiti wananchi ikiwa ni pamoja na kupiga, kuumiza na kuua ovyo. Bado mindsets zao zina shida na hazijabadilika hadi sasa, mfano halisi ni jinsi walivyokuambia kuwa wamepata faini kiasi cha Billioni 50.

Jeshi hili lipo kwa ajili ya kuumiza na siyo kutoa huduma, mfano halisi ni kuwa ukiwa na tatizo inabidi uende polisi uwatafutie usafiri na uwalipe posho (rushwa), sasa hapo haki itapatikana vipi?

Tunaamini ni hatua nzuri kwa kuanzia, tunaomba mheshimiwa rais uwe very BOLD, usiongee kinyonge nyonge, kama suala la PF-3, mheshimiwa lifute kwa madaraka uliyonayo, hakuna haja ya kuwaomba polisi waliaangalie. Kwao litachukua muda kama si miaka wakati wananchi wetu wakiendelea kupoteza maisha.

Suala la haki na kesi za kubambikiziwa, mheshimiwa rais Samia, tunaomba wahusika wote waliofanya hayo madudu wawajibishwe na wafikishwe kwenye mikono ya sheria, kwani suala hilo limeumiza watanzania wasio na hatia na ikiwezekana wapewe compensation kwa yote waliyoyapitia.

Ahsante sana

R. Milla
 
Hii ni barua ya wazi ama risala, kipi kipya ambacho rais au wasaidizi wake wakichukue km changamoto ya kufanyia kazi? Naamn ilikua unataka kusema maneno haya "NAUNGA JUHUDI HATUA ZA MAMA "
 
Kweli tatizo la mama anaomba badala ya kutoa amri kwenye mambo ya msingi. Suala la PF3 ilikuwa atoe kauli thabiti ya kuifuta kabisa.
 
Yaani mpaka Rais aseme, wangapi wamekufa? Tanzania hovyo kabisa
 
Kweli tatizo la mama anaomba badala ya kutoa amri kwenye mambo ya msingi. Suala la PF3 ilikuwa atoe kauli thabiti ya kuifuta kabisa.
Hivi tumekua taifa la watu wasioweza kuelekezwa kistaarabu? Mpaka Raisi ashike fimbo?
 
Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, Kwanza napenda kukupongeza kwa hotuba yako nzuri wakati wa ufunguzi wa kiwanda cha kutengeneza au kushona nguo cha jeshi la polisi.

Nilivutiwa na jinsi ulivyosema kuhusu matumizi ya PF-3 kwa wagonjwa wanaoumia au kupata ajali za barabarani na ni ukweli usiopingika kuwa wengi wa wananchi wanapoteza maisha kutokana na urasimu (bureaucracy) ya system ya kijinga ambayo sijui ilikopiwa wapi.

Kweli mtu anaumia kwenye ajali, anaumizwa na majambazi kwa kupigwa risasi au kuchomwa kisu au ajali yoyote ile iwe ya moto au majanga mengine halafu anapelekwa hospitali anaambiwa hadi apate form ya PF-3? Hivi huu ujinga umetoka wapi?

Tumechelewa sana, wananchi wengi wamepoteza maisha kama ulivyosema mheshimiwa rais, na kama ni sehemu nyingine, ndugu zao walipaswa walipwe fidia kwa uzembe wa hali ya juu wa serikali yetu.

Kwa mapendekezo kama mwananchi, ningeshauri hospitali zote nchini hadi vituo vya afya viwe na sehemu ya EMERGENCY CARE kwa ajili ya kuwakimbiza wanaoumia au wenye shida ya magonjwa hatari ili maisha yao yaweze kuokolewa, tofauti na sasa ambako hospitali zetu hazina hizo huduma za dharura, hivyo unakuta mgonjwa anaambiwa asubiri kitanda hata awe na maumivu kiasi gani au awe mahututi kiasi gani.

Mara nyingi tunasikia mwananchi amekimbizwa hospitali lakini kabla hajaanza kushughulikiwa akapoteza maisha, sababu ni hizo kuwa hatuna hizo huduma muhimu ambazo zipo duniani kote hata hapo Kenya zipo lakini sisi hatuna.

Kwa vile umeona hayo mheshimiwa rais, tunaomba utamke kuwa hayo mambo ya PF-3 yaishe, kwani polisi wana uwezo wa kwenda kumhoji mhanga wa tatizo hata akiwa hospitalini akipokea matibabu.

Pili kuhusu polisi na IGP wao, ni wazi kuwa hili jeshi bado lina tatizo kubwa, kwa mawazo yao ni kwamba wapo kudhibiti wananchi ikiwa ni pamoja na kupiga, kuumiza na kuua ovyo. Bado mindsets zao zina shida na hazijabadilika hadi sasa, mfano halisi ni jinsi walivyokuambia kuwa wamepata faini kiasi cha Billioni 50.

Jeshi hili lipo kwa ajili ya kuumiza na siyo kutoa huduma, mfano halisi ni kuwa ukiwa na tatizo inabidi uende polisi uwatafutie usafiri na uwalipe posho (rushwa), sasa hapo haki itapatikana vipi?

Tunaamini ni hatua nzuri kwa kuanzia, tunaomba mheshimiwa rais uwe very BOLD, usiongee kinyonge nyonge, kama suala la PF-3, mheshimiwa lifute kwa madaraka uliyonayo, hakuna haja ya kuwaomba polisi waliaangalie. Kwao litachukua muda kama si miaka wakati wananchi wetu wakiendelea kupoteza maisha.

Suala la haki na kesi za kubambikiziwa, mheshimiwa rais Samia, tunaomba wahusika wote waliofanya hayo madudu wawajibishwe na wafikishwe kwenye mikono ya sheria, kwani suala hilo limeumiza watanzania wasio na hatia na ikiwezekana wapewe compensation kwa yote waliyoyapitia.

Ahsante sana

R. Milla
View attachment 1790978
Hata mimi namuunga mkono Mhe. Raisi Mama Samia Suluhu Hassan a.k.a Mama SASHA lakini jambo la msingi zaidi ni kwenda kurekebisha sheria inayohusiana na PF-3.
 
Back
Top Bottom