DOKEZO Barua ya wazi kwa Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi

DOKEZO Barua ya wazi kwa Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Leo tarehe 11, July 2024. Umealikwa kuwa mgeni Rasmi katika maadhimisho ya siku ya kupambana na rushwa Afrika.

Hongera Dr. Hussein Mwinyi, kwa nia yako thabiti ya kuzuia na kupambana na rushwa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla, licha ya wasaidizi wako wachache wanaokuangusha.

lengo la barua hii ya wazi kwako ni kukutaarifu kuwa, tume ya utumishi Serikalini Zanzibar ina mikono mingi ya rushwa hususwan, katika mchakato mzima wa ajira.

Kumekuwa hakuna haki na usawa kwenye ajira za Zanzibar hali inayopelekea kuajiriwa kwa wasio na vigezo na kuachwa wenye vigezo kwa sababu tu ya rushwa iliyokithiri na ujamaa.

Mara nyengine wanaajiriwa watu ambao hawakufanya interview hata moja kwa sababu tu ya connection na kuachwa wenye ujuzi hata awe na elimu kama bahari, kwa sababu tu ni watoto wa kimaskini wasio na uwezo wa kutoa chochote kitu.

Hali hii inachangiwa pia na kuchelewa kuwaita watu kazini na wanaoitwa huitwa kimya kimya bila ya kutoa list kwa umma kama ilivyo kwa upande wa Tanzania Bara.

Hitimisho, tunaomba ofisi hii ya utumishi serikalini iwe ni starting point ya kufanyiwa kazi baada ya maadhimisho yaliyofanyika leo kwa sababu wananchi wanalalamika sana mitaani.
 
mkuu achana na CCM, hao watu hawawezi kutengenea tena, suluhisho ni kuwang'oa tu.
 
Back
Top Bottom