Kwa Tume hii ya Uchaguzi ?Mwisho wa siku na yeye anatamani kugonga meza pale Dodoma ale Zabibu.
Mambo ya mali za waislamu yamepitwa na wakati
Kwa Tume hii ya Uchaguzi ?
Yaani unatarajia ashinde ?
Ushindi kwa mtu yoyote wa upinzani ni mpaka CCM waruhusu Hilo jimbo liende...lakini sio kwa
Kwani waliowahi kushinda ilikuwajeKwa Tume hii ya Uchaguzi ?
Yaani unatarajia ashinde ?
Ushindi kwa mtu yoyote wa upinzani ni mpaka CCM waruhusu Hilo jimbo liende...lakini sio kwa kura za wananchi
Labda kama huna macho ya kuona,Kwani waliowahi kushinda ilikuwaje
Kwa lugha rahisi unamsihi Mzee Ponda asiende kuwa mwakilishi wa wananchi wa Temeke na kutetea maslahi yao kuptia bunge, bunge ni jukwaa kubwa zaidi la kusikika hata kama ni kibogoyo, ni jukwaa jingine kuendeleza maono yake.Hata hivyo, kwa masikitiko na tahadhari kubwa, napenda kukuomba kwa dhati kabisa usigombee ubunge wa Jimbo la Temeke, iwe kwa tiketi ya ACT-Wazalendo au chama kingine chochote cha siasa.
Watu wanacheza kete zao, naona Mzee Ponda akipewa jimbo labda si na wananchi ila na washika funguo.Iwapo utachukua uamuzi wa kugombea, kuna uwezekano mkubwa wa kushindwa kwa tofauti kubwa, jambo ambalo linaweza kusababisha madhara makubwa kwa heshima yako kama kiongozi wa kitaifa wa dini.
KweliSheikh Ponda uwe na sikio lenye usikivu isipokuwa "Hiari ya shari, heri ni kufa" au "Hiyari hulenga pabaya."
Basi Ponda tunampa ili muaibike wasusiajiLabda kama huna macho ya kuona,
Kwa miaka ya hivi karibuni..hasa mifumo aliyoanzisha Jiwe kura za wananchi hazina umuhimu
Sio kama nabahatisha.. wengine tuna ndugu waliowahi kusimamia chaguzi hizi ..wanatupa kinachoendelea ndani ya chaguzi hizi
Mpe hata mwiliBasi Ponda tunampa ili muaibike wasusiaji
Umechelewa Malaria 2Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu
Mpendwa Sheikh Ponda,
Assalaamu alaykum warahmatullah wabarakatuh,
Kwa heshima na unyenyekevu mkubwa, ninakuandikia barua hii kama ndugu yako na Mtanzania ninayekuheshimu sana kwa mchango wako wa muda mrefu katika kupigania haki, kutetea jamii ya Kiislamu, na kuwa sauti ya wanyonge katika taifa hili.
Sheikh, kwa zaidi ya miongo miwili, umekuwa kiongozi mashuhuri katika harakati za kudai haki za Waislamu, kurejesha mali za Waislamu, na kutoa mwongozo wa kiroho na kijamii kwa jamii pana ya Watanzania. Umesimama kidete wakati ambapo wengine walinyamaza. Ulikuwa bega kwa bega na viongozi mbalimbali wa Kiislamu kama Sheikh Mbukuzi, Sheikh Omar Bashiri (marehemu), Sheikh Basaleh (marehemu), Sheikh Mazinge, Sheikh Kassim bin Juma, Sheikh Khalifa, na Masheikh wengine ambao ama wametangulia mbele ya haki au wamepumzika katika majukumu yao.
Katika historia yako, umetumia majukwaa ya dini kwa ajili ya maslahi ya Umma, umehimiza mshikamano, umepigania haki za Wapalestina, na umepaza sauti dhidi ya dhulma katika jamii. Heshima yako imejengwa juu ya misingi hiyo ya uadilifu usioegemea upande wowote wa kisiasa.
Hata hivyo, kwa masikitiko na tahadhari kubwa, napenda kukuomba kwa dhati kabisa usigombee ubunge wa Jimbo la Temeke, iwe kwa tiketi ya ACT-Wazalendo au chama kingine chochote cha siasa.
Ni kweli kwamba, kama Mtanzania mwingine yeyote, Sheikh Ponda una haki ya kushiriki katika siasa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977. Haki hiyo imo katika Ibara ya 20(1), inayosema:
Hata hivyo, pamoja na haki hiyo ya kikatiba, kwa kuzingatia hali ya sasa ya kisiasa nchini, ni wazi kuwa mazingira ya ushindani wa haki bado ni changamoto kubwa, hasa katika majimbo yenye mvutano mkubwa kama Temeke. Si kwamba huna uwezo, wala hauna wafuasi — bali hali halisi inaonesha kuwa vyama vya upinzani bado vina nguvu ndogo ukilinganisha na chama tawala ambacho kina mtandao mpana wa kiutawala na rasilimali nyingi, jambo linalowapa nafasi ya ushawishi mkubwa katika mchakato mzima wa uchaguzi.
Iwapo utachukua uamuzi wa kugombea, kuna uwezekano mkubwa wa kushindwa kwa tofauti kubwa, jambo ambalo linaweza kusababisha madhara makubwa kwa heshima yako kama kiongozi wa kitaifa wa dini. Utaonekana umeingia kwenye siasa kwa maslahi binafsi, na wapinzani wako wataitumia nafasi hiyo kuhoji uhalali wa msimamo wako wa kidini na kijamii.
Sheikh, pindi utakapokuwa mwanasiasa wa chama, hata kama ni chama chenye sera nzuri kiasi gani, utaonekana umeegemea upande mmoja. Watu wengi hawatakusikiliza kama Sheikh wa jamii nzima, bali kama mwakilishi wa chama fulani. Sauti yako ya sasa ina nguvu kwa sababu inasikika na kuheshimika kutoka pande zote — usiipunguze kwa kuigeuza kuwa ya chama kimoja.
Hutoweza tena kusimama na kusema “nawakilisha Waislamu wote,” bali utaonekana kuwa msemaji wa chama chako. Hutaonekana tena kama Katibu wa kutetea haki za Waislamu, bali kama mpiga debe wa chama — hata kama dhamira yako ni njema.
Kwa hiyo, kwa heshima na mapenzi makubwa, naomba utazame wito huu si kama upinzani, bali kama sauti ya tahadhari ya kidugu. Tunaamini bado unaweza kuendelea kuwa taa ya jamii, mshauri wa viongozi, mtetezi wa wanyonge, na sauti ya haki kwa wote — ukiwa nje ya Bunge, lakini ukiathiri taifa zima kwa hekima, ushauri, na msimamo wa ukweli.
Uongozi si lazima uwe ndani ya Bunge. Uongozi wa kweli uko katika uthubutu wa kusimama na kusema kweli hata bila vyeo. Hilo umelithibitisha kwa miaka mingi. Tafadhali, endelea kuwa hivyo, Sheikh wetu.
Wassalaamu alaykum warahmatullah wabarakatuh,
DKT. MALARIA 2
Mwananchi, Mfuasi wa Haki, na Ndugu Yako wa Taifa
Huyo huenda ni Yule hawara ya bibi Yake wa lambo wa adrizWatia nia ya ubunge wengi wao hudanganywa na wapambe wao, ila mwisho wa siku hata bila hujuma za serikali kuu wanakua tayari wameangukia pua huku wapambe wakila pesa zao tu.
Kuna jamaa alisoma ughaibuni na kufanya kazi kwa muda huko, aliporudi bongo akajiingiza kwenye siasa muda mfupu tu baada ya kufika.
Sasa kile kibunda kilishawishi baadhi ya wajumbe na kuanza kumnadi ili ashike nyadhfa fulani chama tawala.
Na cheo cha kiwilaya tu, alimwaga pesa kwa wapambe huku mtaani hata hafahamiki, akidhani pesa itanunua kila kitu.
Watu waliishia kunywa bia tu.
Hakuna tatizoKwani Kuna shida gani tukiwa na wabunge mashekhe
Acha kumpangiaSheikh ponda atulie
Kweli ukistaajabu ya Musa utayaona ya Farao. Kama katiba inasema kila mtu anauhuru wa kushiriki uchaguzi why kuna waozunguka kushawishi watu wasishiriki uchaguzi!Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu