Barua ya wazi kwa Shukuru Kawambwa

Barua ya wazi kwa Shukuru Kawambwa

KIRAMBA

Member
Joined
Aug 14, 2014
Posts
6
Reaction score
0
Kwa waheshimiwa



Dr. Shukuru Kawambwa


Hawa Ghasia


Jenista Mhagama


Agrey Mwandry


Kasim Majaliwa



YAH . KUMLALAMIKIA AFISA ELIMU WA SHULE ZA MSINGI MANISPAA YA MOSHI KWA JINA (D. BIMBALIRWA)

Kwa kweli imebidi sasa waalimu wa manispaa ya moshi tuanze kupaza sauti zetu kwa namna yeyote ile iwayo hadi hapo tume huru ya uchunguzi itakapokuja hapa moshi kumchunguza huyu afisa elimu msing wa manispaa ya moshi.

Sasa ni upendeleo kwa baadhi ya walimu anaowataka. Ana walimu wa mgongoni na wa tumboni. · Ngono mtindo mmoja njooni shule ya msiingi J. K nyerere, muoneni kwa macho. Shule za msing rau, na sokoine wakuu wa shule wanabadilishwa kama karata.

Ukaguzi ulifika shule ya msingi sokoine na waligundua mkuu wa shule hana uwezo wa kuongoza, kioja ni kwamba afisa elimu alimwamisha mkuu huyo wa sokoine ambaye shule yake ilikuwa inapumulia mashine akambadilisha na mkuu wa shule ya rau. Sasa sijui anataka shule ya msingi Rau nayo ikafe tena au?. · Afisa elimu amekuwa anachangisha waalimu wakuu michango ili ambayo anaitumia kujengea nyumba yake. nyumba anayoijenga ni kubwa sana na ipo maeneo ya msaranga (tume ichunguze kipato chake na kama ana mkopo benki ili ione maajabu ya nyumba hiyo/tumechoka kuchangishwa wakati sisi wengine hata kiwanja hatuna).

Mbadhirifu wa mali za umma. Amegeuza kituo cha walimu mawenzi kuwa tuitisheni center, kituo ni kwa ajili ya walimu kujiendeleza inakuwaje anafanya kituo tuitisheni center. · Ana upendeleo.bimbalirwa amekuwambaguzi na mpendeleaji wa walimu sana, hataki walimu wakasome,ila anawapa wengine upendeleo wanaenda kusoma wakiwa wanashikilia nafasi zao za ukuu wa shule au uratibi .fano hai ni mwaka juzi alimruhusu mratibu mmoja mwanamke jina tunalo akaenda kusoma kwa muda wa miaka miwili bila nafasi yake kupewa mtu hadi alipomaliza na kurudi kwenye nafasi ile ile na eneo lilile.

Huu ni upendeleo wa dhat mtu anakuwa nje ya kituo kwa miaka miwili na nafasi yake inabakia vilevile,angali wengine tukiomba tunakataliwa.hata evening program za waalimu kujiendeleza aezikataza na nakala ya barua za kukataza walimu wasisome tumeiweka kwenye mitandao ya kijamii ambayop ameisaini yeye nwenyewe kama mkuu wa idara. · Kituo cha walimu cha mawenzi kimekuwa kitega uchumi chake. Kimefanywa tuition center badala ya kituo cha walimu kujiendeleza.

Afisa elimu manispaa ya moshi idara ya msingi, upo usanii ambao huwa anautumiaga sana kipindi cha mitiani ya taifa ili manispaa ya moshi iendelee kuwa ya kwanza angali watoto hawana uwezo huo.anajua fika yakwamba manispaa ikishakuwa ya kwanza hataweza kuhamishwa.walimu wanaopangwa kusimamia mtihani huwa huwa wakifika kwenye kituo cha kusimamia wanapewa hela na mkuu wa shule husika ili awaachie wanafunzi wajadili na wawe huru kusaidiana wenyewe kwa wenyewe .ndio maana unakuta mkondo mzima unafaulu.

Anafanikiwa kufanya hili kwa kuwa amekuwa anawabakisha wakuu wa shule wabaki mashuleni siku ya mtihani ili waweze kuwapa wasimamizi hela mapema walegezee watoto uzi. Msimamizi anakuwa kazi yake ni kucheki doria nje na sio kusimamia watoto. · Amekuwa anatoa vitisho kwa wakuu wa shule na waratibu. ni hivi karibuni amekuwa na kikao cha kuwatishia waratibu na wakuu wa shule endapo manispaa itaanguka na kushindwa kuwa ya kwanza mwaka huu.

Amekuwa anajitamba mtaani kuwa hakuna mtu wa kuweza kumwamisha manispaa ya moshi labda apende yeye. anasema yeye amepewa uafisa elimu na mama mtukamanzima aliyekuwa wizarani, hivyo hakuna wa kuweza kumtoa. Ombi letu tunaomba kamati maalum ije kuchunguza malalamiko yetu. Huyu ni mbaguzi,mfanya kazi kwa kusikiliza maneno ya pembeni, asiye tenda haki, mla rushwa, mpenda ngono. KAMA HATUA HAZITACHUKULIWA STAHIKI TUTAMWANDIKIA WAZIRI WA ELIMU BARUA AFUATILIE YEYE

Nakala:
Katibu Mkuu/Wizara ya Elimu
Ofisi ya Waziri Mkuu na serikali za mitaa
Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro ·
Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi ·
TAKUKURU, Kilimanjaro
 
Ama kweli. Bora kuuawa na simba mwenye njaa maana anaweza akala nyama yako kuliko nyoka mwenye sumu ambaye baada ya kifo chako hatakufaidi kwa cho chote. Kiramba ni nyoka mwenye sumu. Hana tofauti na Kigagula kichawi kinachologa watoto wasio na makosa kwa sababu tu kimeona wivu kwa wazazi wa mtoto kumpata na kumlea mtoto mchanga mzuri asiyekuwa na makosa yo yote. Ewe Kiramba acha wivu wa kipumbavu.

Mwishoni mwa mwezi wa Mei na Juni mwaka huu ulikuwa ukituma msg kama hizi kwa Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro, Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Kilimanjaro, Mkaguzi wa Hesabu za Serikali Mkoa wa Kilimanjaro, Mkuu wa Wilaya ya Moshi na Mkurugenzi Manispaa ya Moshi, kwa kujifanya wewe ni mwalimu wa Manispaa ya Moshi kwa jina la bandia Jumanne Samson na namba ya TIGO 0654300539. Hii inathibitishwa na kufanana sana kwa mtindo wako wa uandishi katika msg za simu na ujumbe huu ulioutuma jf. Katika msg nyingi ulizokuwa ukizituma kwa viongozi hao na walimu mbalimbali wa Manispaa hii, ulionesha hasira zako za nyoka mwenye sumu kwa kumtuhumu Bw. D. A. Bimbalirwa (Afisaelimu na Utamaduni Manispaa ya Moshi) kwa masuala uliyoyarejea katika ujumbe wako hapa jf. Mbaya zaidi ni kuwa ulizituhumu Shule za Msingi Uhuru, Mawenzi, Muungano, Mwenge na Mwereni pamoja na Kituo cha Walimu Mawenzi kwa kutumika kukusanya fedha kwa njia mbalimbali, kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya afisa huyu, kama vile mshahara wake na wa mkewe hauwezi kufanya maendeleo kama hayo ama hawezi kukopa kwenye taasisi za fedha. Kwa faida ya wasomaji wa jf, hasira za Kiramba zilianza mara baada ya uteuzi wa mwalimu mkuu wa shule ya msingi J.K. Nyerere baada ya kustaafu kwa aliyekuwa mwalimu mkuu wa shule hiyo.

Ili kuthibitisha tuhuma hizo, Mkaguzi Mkuu wa Shule Kanda ya Kaskazini Mashariki aliunda timu ya wakaguzi watatu ili kuchunguza tuhuma hizo. Mkaguzi wa Mahesabu Mkoa alimteua mkaguzi mahiri wa hesabu za serikali kufanya ufuatiliaji wa kina. Mkurugenzi Manispaa ya Moshi alituma wataalamu wa fedha ili kujiridhisha kuhusu tuhuma hizo. Inasikitisha kuwa raslimali watu, muda na fedha za serikali zilitumika bure kwa kufanya ufuatiliaji wa tuhuma zako za kipumbavu kwani hakuna cho chote kilichothibitika. Hivi sasa umehamia jf baada ya kugundua kuwa ulemavu wa akili (utaahira) ulio nao haukuweza kuwaambukiza viongozi husika.

Tuhuma za ngono si rahisi kuzithibitisha kwani vitendo hivyo hufanyika faragha. Labda ututhibitishie kuwa na wewe, uwe mwanaume au mwanamke, ulishawahi kushughulikiwa na afisa huyu. Na kama ndivyo, basi hukumridhisha ipasavyo na hivyo wivu wa kuachwa ndio unaokusumbua. Wivu utakuua. Acha upumbavu. Tunahitaji maendeleo na sio tuhuma za kishenzi na za kijinga kama hizi.

Dhamira yako ni kuhujumu maendeleo ya kitaaluma ya muda mrefu ya manispaa hii. Kwa taarifa ya wana jf, manispaa hii ina hati miliki ya kushika nafasi za juu kitaifa katika kumi bora ya matokeo ya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi (PSLE) kwa zaidi ya miaka ishirini. Walimu wa Manispaa ya Moshi tokea enzi, wana asili ya kufanya kazi kwa ari na kujituma ipasavyo. Hivyo tuhuma kuwa Bimbalirwa huwataka walimu wawasaidie wanafunzi wakati wa PSLE hazina msingi kwani aliikuta manispaa hii ikiwa na utamaduni wa kushika nafasi za juu kitaifa.

Kiramba elewa kuwa wakati wa mitihani, licha ya Mkurugenzi Manispaa, Maafisaelimu Manispaa (MEO, Ukaguzi wa Shule na Idara ya Utumishi kwa Walimu) kuwajibika katika ufuatiliaji; mwakilishi wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), Usalama wa Taifa (TISS), Usalama wa Raia (POLISI) na Ofisi ya Elimu Mkoa huwajibika kwa asilimia mia moja katika kuhakikisha kuwa mitihani hiyo hufanyika kufuata sheria na taratibu zilizowekwa na Baraza la Mitihani la Tanzania. Hivyo Kiramba, kuhusu mitihani, usidhani unamtuhumu Bimbalirwa peke yake. Uongozi hautafutwi kwa uzushi, uzandiki, ulaghai ama uongo wenye visa na visasi kama huu wako. Jipange upya. Najua huchoki kutunga uongo wa kitoto. Unasubiriwa maana huna jipya zaidi ya rejea ya mwezi Mei na Juni 2014.

Nina wasiwasi wewe ni mpinzani si tu wa maendeleo, bali pia wa sera safi za Chama Cha Mapinduzi ambazo zimekuwa zikitekelezwa na watendaji wa Halmashauri hii licha ya kuwa chini ya upinzani.
 
Mleta mada ni mwalimu kweli? mwandiko kama wa baba yangu aliyekuwa mwalimu wa elimu ya watu wazima!
 
Ndugu yangu Ndebile hii ndio taabu tuliyo nayo katika nchi hii. Kama kweli ni mwalimu, basi hapa tuhesabu 0 kwenye hiyo BRN. Jamaa hata kupanga mawazo kwenye aya hawezi. Kufuata vituo hajui. Mtiririko wa mawazo ni matatizo. Alichojua yeye ni kutoa jakamoyo linalomsibu katika moyo wake.

Ushauri wa bure kwako KIRAMBA. Soma kwa makini majibu yaliyotolewa na HORACE. Angalia mpangilio wa mawazo yalivyojinasibu katika uandishi wake. Katika aya ya tano ya Horace anadhani huu ni wivu wa kimapenzi. Hata mimi naunga mkono. Katika aya ya sita Horace anatahadharisha kuhusu matokeo ya wivu wako kwa wanafunzi, walimu, wazazi na jamii ya manispaa hii kwa jumla. Anaona kuwa dhamira yako ni kuhujumu taaluma katika eneo hili. Ninasikitika kukuambia kuwa HUTAFANIKIWA.
 
Back
Top Bottom