Luqman mohamedy
JF-Expert Member
- Jul 24, 2016
- 899
- 1,231
Utangulizi: Kuna udumavu wa maendeleo na ongezeko wa deni la taifa linaloletwa na mikopo ya nje sababu ya uchache wa kodi zinazokusanywa.
Mamlaka ya ukusanyaji mapato inapaswa kutumia njia chanja kuliko hasi katika uhamasishaji wa kulipa kodi na ukusanyaji wa kodi zenyewe.
Kwa muda mrefu mamlaka zimekuwa zikitumia njia hasi maarufu kama 'Task force' kufunga biashara za wanaoshindwa kulipa kodi na kuwakamata watu wasiodai risiti baada ya manunuzi,njia hii haijaongeza mapato hata kidogo.
Kutatua hili mamlaka inapaswa itumie njia chanja kama ifuatavyo;
1. Kila mlipa kodi anapaswa kurudishiwa 5% ya kodi aliyolipa mwishoni mwa mwaka wa kifedha,hii itashawishi wanunuzi kudai risiti zao pindi wanapofanya manunuzi.
Hakutakuwa na haja ya kukamata watu wasiodai risiti.
Hili litawezekana kwa kila mwananchi kuwa na TIN yake.
2. Kurudisha uwajibikaji kwa wezi wa pesa umma na mafisadi wanaoainishwa kwenye ripoti za CAG.
Wananchi wengi wamekuwa wakikwepa kodi wakiamini kodi zao haziendi kuleta maendeleo bali zinaenda kutajirisha watu wengine jambo ambalo linapunguza utayari wa kulipa kodi.
Uwajibishwaji wa hawa watu na usimamizi mzuri wa pesa za walipa kodi utaongeza hamasa na utayari wa kulipa kodi.
3. Kutoa misamaha ya kodi kwa biashara ndogo na za kati miezi 3-6 baada ya kuanzisha biashara. Upendeleo unaopewa makampuni ya nje wa kipindi za majaribio 'trial' bila kulipa kodi unapaswa uhamishiwe kwa biashara ndogo ndogo pia.
Msururu wa kodi kwa biashara mpya unadumaza ukuaji wa biashara hizo,iwapo wafanyabiashara hawa watapewa nafasi ya kukuza biashara zao kwa miezi kadhaa kisha ndio waingie kwenye mfumo wa kulipa kodi utaongeza idadi ya biashara mpya.
4. Kuongeza urasimishaji wa biashara ndogondogo.
Tunapoteza mapato mengi kwa kuwa na biashara nyingi ambazo sio rasmi.
Biashara kama bodaboda,madalali wa nyumba (mitaani),mama ntilie nk haea watu tunapaswa kuwatambua kama wachangiaji wa pato la taifa na wanapaswa kupewa leseni bure kabisa za kufanya biashara zao.
Kila mwisho wa mwaka wakilazimika kulipia 1% ya makadirio ya pato lao la mwaka utaongeza wingi wa kodi.
5. Ufatiliaji duni wa mikataba ya waajiriwa kwenye sekta binafsi.
Idadi kubwa ya wafanyakazi kwenye sekta binafsi hawana mikataba inayotambulika kisheria,wengi wao hulipwa kama vibarua tu.
Kwa namna hii hawa hawaingizwi kwenye mfumo wa kulipa PAYE kama walivyo wafanyakazi wengine.
Mamlaka zinapaswa zifanye ukaguzi wa mara kwa mara kwenye sekta hizi ili kupata walipa kodi wapya,waajiri watakaokiuka biashara zao zifungwe au kupigwa faini.
6. Kuongeza ajira na kutoa mikopo,
Tunapoteza idadi kubwa ya walipa kodi ambao wengi ni wahitimu wa vyuo vikuu kwa wao kukosa ajira na mitaji ya kujiajiri.
Ni uwekezaji mbovu sana kutumia mapato ya serikali kwa kumsomesha watu kwa miaka 14 kisha kuja kumuachilia mtaani bila kumpa fursa ya kujiajiri na ajira.
Mikopo ya mtu mmoja mmoja inapaswa kutolewa kwa wahitimu hawa.
Mazingira ya kujiajiri pia yanapaswa kuwekwa vizuri ili tupate walipa kodi wapya.
Hitimisho: Tunapaswa kutengeneza mazingira ya kuwa na walipa kodi wadogo wadogo wengi wanaolipa kodi na sio walipa kodi wakubwa wachache wanaokwepa kodi.

Upvote
3