Wakudadavuwa
JF-Expert Member
- Feb 17, 2016
- 17,506
- 16,003
Ndugu yangu Uhuru aka Kamwana,
Kuna mambo umeyafanya ambayo yameleta ghadhabu wa wakenya sasa unataka kutupia lawama mataifa jirani kama ambavyo Trump anavyolaumu China kwa matatizo yake ya ndani.
Ushauri wangu tulia jifunze kutatua matatizo wa wanakenya kwa kutumia mikakati ya kimagharibi. Hili limekuwa tatizo kwenye nchi nyingi Afrika na inatokana zaidi na ukakasi wa viongozi wengi kukariri mitaala (curriculum) iliyotengenezwa kutatua changamoto za ulaya na Amerika. Hii imesababisha wafanya maamuzi wengi hasa wakurugenzi, makatibu wakuu badala ya kupata elimu wao hukazana kuzungumza Kiingereza kwa lafudhi (accent) ya wazungu huku akitingisha kichwa na kushika nywele kichwani ili naye aonekane Mzungu hapa ndipo wazungu hutushangaa wanachofanya ni kukusifia huku wakikuzodoa (dharau).
Mtu akitumia mbinu nzuri ambayo inafaa kwa mazingira husika usimchukie bali soma taratibu uchanganye na akili zako ili uweze kutafuta suluhisho sahihi kwa mazingira yako ili usiwaumize wananchi. Nikupe mfano pamoja na utajiri wa nchi za magharibu na uwezo wa kulipa wananchi wao ''walfare payments'' au malipo kwa wasio na ajira hili jambo halitekelezeki (unsastainable) kwa muda wa kati (short term) na muda mrefu (long-term). tusitatue changamoto za Africa kwa kutumia ''blue print'' za IMF, WB, WHO na kadhalika bali tusome hizo ''blue prints'' tuchague yanayotufaa na tuite wataalamu wetu wa nyanja mbalimbali ili kutatua tatizo.
Kwa mfano; ili kukabiliana na janga la Covid-19 inapasa viongozi wa Africa kusoma muongozo wa WHO (ambao kimsingi umejikita kwenye afya), lakini yatupasa kushirikisha wataalamu wa uchumi, biashara, miradi, kilimo, jamii na kadhalika ili kuja na mkakati wa jumla (Holistic approach) ambao utatekelezwa bila kuleta machungu sana kwa wananchi. Leo hii Ndugu Kenyatta ukitumia watu wako wa usalama wachunguze wanakenya wangapi wanakufa usishangae kuambiwa waliokufa na maradhi yanayosababishwa na njaa ikiwemo unyanyasaji ni wengi kuliko wanaokufa na Covid-19.
Nimeshangaa kusikia mmoja wa mawaziri waandamizi (CS)kwenye wizara ya Kilimo Bw.Munga akitangaza kuagiza chakula kutoka Ethiopia. Kama baraza la mawaziri lina waziri amabye hajui hali ya mavuno na chakula kwa nchi jirani lazima kuna tatizo la msingi. Ethipia hii ambayo miaka na mikaka ina tatizo la njaa, nzige, siasa zisizotulia (political instability leo wauie Kenya Chakula? Mh. Kenyatta hivi waziri wako hajui kuwa umoja wa ulaya umeahidi kuchangisha mamilioni ya euro kuisadia Ethiopia kupambana na baa la njaa (hunger)?
Kuhusu suala la madereva kusafirisha vitu mipakani linahitaji busara kubwa sana ili kuepuka malalamiko ya wananchi wa Afrika ya Mashariki. Ili kuepuka lawama kwamba madereva wa Tanzania ''wanaingiza Covid-19'' Kenya, Mkuu wa Mkoa wa Kilimajaro aliagiza kuwa mizigo yote inayoingia Kenya kupitia mipakani ishushwe kutoka magari ya Tanzania na kupakiwa kwenye magari ya Kenya yenye madereva wa Kenya ''wasioa na Covid-19'' ili kuzuia maambukizi na vilevile ile inayotoka Kenya ishushwe mpakan na kupakiwa kwenye magari yenye madereva wa Tanzania; mantiki ya hoja hii ni kama ifuatavyo;
Ningependa nikutaarifu tu ya kwamba nimeona taarifa kupitia television ya CNN kuwa baada ya kudhibiti hali ya ugonjwa wa Covid-19 Marekani wataanza uchunguzi wa kina (scuitiny) kwa taasisi zake kwasababu inaonekana ni kama kuna mchezo unaendelea kwa sababu za siasa, biashara na uchumi wa kimataifa.
Nimeona kwa mfano; licha ya Northen coridor ya nchi nne za jumuiya ya Afrika Mashariki kukutana bila Tanzania na Burundi kumekuwa na ''billateral arrangements'' baina ya Uganda, Rwanda na Tanzania ili kuruhusu mambo yaende. Bado kuna nafasi ya Tanzania na Kenya kufanya ''billateral arrangements''. Kumbuka Bandari ya Mombasa inapitisha baadhi ya shehena za DRC na baadhi ya nchi nyingine ikiwamo Tanzania hususani maeneo ya kanda ya ziwa Victoria. Kama kutakuwa na usumbufu hii biashara ndogo utaikosa, kwani shehena kubwa ya nchi hizi hupitia Tanzania. Ndio maana nimesema ili kukabiliana na Covid-19, unapaswa kusoma muongozo wa WHO huku ukishirikisha wataalamu wa biashara, sheria, miradi, uchumi na kadhalika ili kupata suluishi la jumla (holistic approach. Kuna msemo wa kiswahili unasema ''la kuambiwa changanya na za kwako''
Mwisho nikukumbushe; Covid-19 bado ipo sana, haitaisha kwa kufungia watu ndani au kufunga biashara bali kwa kutoa elimu ya afya, kuondo hofu na kujifunza jinsi ya kuishi nayo huku jitihada za ugunduzi wa kinga na tiba ukiendelea.
Tusipuuze dawa zetu za asili hasa ikizingatia ugonjwa huu umeonekana kuwa wanaopona ni wengi sana huku asimilia ndogo inakufa (si jambo jema). Tungeweza kuwatenga wazee na wenye maradhi sugu ingesaidia kupunguza vifo. Zaidi ya yote Kenyatta, Mungu yupo! sisi ni waja wake tusichoke kumsihi atupe mbinu ya kupambana na maradhi haya ambayo madhara yake yamekuzwa (overrated) kuliko uhalisia.
Ni malize kwa kukutakia kazi njema Mh. Rais
Wakudadavuwa
Mwanajumuiya ya Afrika Mashariki Mwandamizi.

- Ni jambo lisilowezakana madereva kuwa kila siku hauumwi unapimwa mfano kwa dereva anayeingia Kenya/Tanzania mara tano kwa mwezi atalazimika kupimwa mara kumi kwa mwezi, yaani mara tano 5 na mara tano Tanzania. Ni nani anaweza kuvumilia?
- Ucheleweshaji wa mizigo kusubiri vipimo umeharibu thamani ya bidhaa na mazao na pia kuongeza gharama ya biashara bila ulazima.
- Hii itapunguza lawama kuwa nchi fulani inapeleka magonjwa kwenye nchi nyigine.