BARUA YA WAZI KWA WIZARA YA ELIMU (Kamishena wa Elimu)

wanguwangu

New Member
Joined
Jun 5, 2008
Posts
4
Reaction score
0
KWA KAMISHENA WA ELIMU
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI,
MAKAO MAKUU DAR-ES-SALAAM.

Yah: WARAKA WA ELIMU NAMBA 5 WA MWAKA 2012 KUHUSU MAREKABISHO YA MIHULA YA SHULE ZA SEKONDARI NA VYUO VYA WALIMU.

Rejea Waraka mpya wa Elimu namba 5 wa Mwaka 2012 kuhusu marekabisho ya mihula ya shule za Sekondari na vyuo vya walimu wahusika.
Sisi wazazi na wadau wa elimu tunapenda kuchukua nafasi hii kuipongeza Wizara kwa kazi nzuri inayofanya . Aidha tunapenda kuishukuru Wizara kwa kuanzisha utaratibu wa mihula mipya ya shule hasa ile ya Kidato cha Tano na Sita. Tunaamini kabisa kwamba mihula hii mipya italeta ufanisi mkubwa hasa kwa Walimu ambao kwa sasa watapata muda wa kutosha kufanya majukumu yao huko mashuleni.
Pia kwa mujibu wa Waraka huu, mpango huu utaanza rasmi mwaka huu 2013, na utawahushisha Kidato cha Tano waliopo mashuleni sasa, ambao kwa mpango wa zamani walipaswa kumaliza Kidato cha Sita mwaka 2014 mwezi wa Februari, ila kwa sasa itabidi wamalize kidato cha Sita mwezi wa May 2014.
Licha ya utaratibu huu mpya kuonyesha kwamba utaleta ufanisi mkubwa, sisi kama Wazazi na Wadau wa elimu tumeona mpango huu ukianza ghafla hivi utasababisha matatizo makubwa hasa kwetu sisi tunaosomesha watoto wetu kwenye shule binafsi hata kwa Serikali pia.
Shule binafsi zinawafanyakazi walioajiriwa ambao mishahara yao, marupurupu yao, na michango ya mifuko ya Hifadhi hutegemea ada za wanafunzi kwa asilimia kubwa.
Bajeti ya uendeshaji wa shule hizi hupangwa sambamba na mwaka wa masomo kwa kuzingatia siku za kuwepo shuleni.
Kidato cha Sita wakimaliza mitihani yao mwezi wa Februari 2013 wataondoka na hawa wa Kidato cha Tano sasa nao watakuwa wamemaliza mwaka wa masomo na itabidi nao waende likizo ndefu ya miezi minne kabla hawajarudi shuleni mwezi July 2013 kujiunga na kidato cha Sita.
Kipindi hiki cha miezi menne ambacho wanafunzi wa kidato cha Tano wakiwa likizoni, shule zitaingia katika gharama za uendeshaji na kuwalipa walimu na watendaji wa shule bila utendaji halisi, kulipia miundombinu kama maji umeme, na kwa wale wanaokodi hosteli inabidi wazilipie.
Tatizo jingine ni la kiaadili, kwani wanafunzi hawa wakiwa majumbani kwetu kwa kipindi cha miezi MINNE, hawatakuwa salama kimaadili, maana wazazi tunakwenda kazini na kuwaacha majumbani peke yao.
Tatizo linguine ni la kitaalumu, kwani hawa wanafunzi kwa mujibu wa mpango wa zamani wa mihula walitakiwa wakae likizo ya mwezi mmoja tuu kabla ya kurudi shuleni, na kwa mpango mpya watalazimika kukaa nyumbani miezi minne ambayo tunahakika itashusha viwango vyao vya taaluma. Sisi wazazi tunapo kuwa hatupo majumbani watoto hawa wanaweza kufanya mambo mabaya.
Hata kama shule hazitafungwa kwa miezi minne, bado wazazi watalazimika kuongeza ada ya ziada kwa muda ambao haukuwepo kwenye bajeti.
Matatizo kwa Wanafunzi wanao husika ambao wapo katika Kidato cha Tano sasa ni kwamba kisaikolojia wataadhirika kwani badala ya kumaliza Kidato cha Sita mwezi wa Pili watamaliza mwezi wa Tano.
Mitihani yao itakuwa migumu zaidi kwani muda wa kujisomea bila walimu utakuwa mkubwa zaidi.

Mapendekezo:-
Tunaomba Wizara ya Elimu itekeleze mihula mipya kwa awamu kama ifuatavyo:-
Badiliko hili lisiwahusu wanafunzi ambao wapo mashuleni katika Kidato cha Tano sasa. Wao waendelee na utaratibu wa mihula wa zamani. Hii itaepusha matatizo tuliyo baini kwa shule, wazazi na wanafunzi.
Zoezi hili lilenge wanafunzi wapya kabisa watakao chaguliwa kuingia au kuomba kuingia Kidata cha Tano cha mwaka huu 2013. Wao wajiunge na masomo mwezi wa July 2013 na kumaliza Kidato cha Sita May 2015.
Tunatanguliza shukrani zetu kwa Wizara kwa uelewa wenu makini na hatuna shaka maoni yetu yatazingatiwa kwa manufaa ya kujenga Taifa kwa kuboresha ELIMU
Sisi ni wazazi tunawakilisha wenzetu ambao tuna watoto katika Kidato cha Tano kwa kipindi hiki.

Tunawasilisha.
 
Mawazo mazuri lakin mkuu ungeyafikisha baraza penyewe ingekuwa vyema zaidi.
 
Hapo mmepatia wazazi wenzangu tukumbuke huko wizarani watendaji wametulia tu so hatuna budi kuwakumbusha mara kwa mara
 
Mtoto kukaa nyumbani muda mrefu hakuwezi muharibu kama wazazi hamna malezi na hamjawafundisha malezi mazuri watoto wenu msitegemee sana shule kuwafunda. Pili suala la bajeti ya shule za binafsi haliusiani na serikali wao wana wahisani. Tatu kukaa kwa mtoto miezi 4 si tatizo kwani akirudi shule bado kuna muda wa kutosha kufanya vizuri hadi 2014. Nne walezi na wazazi malezi ya watoto wenu msiipe mzigo serikali kama vipi mkiondoka kwenda kazini wafungieni ndani hadi mtakapo rudi. Tano mbona hao wa kidato cha nne toka wamalize hadi matokeo yatoke ni miezi6 je wameharibika? Na watakao kuwa wanasubiri kujiunga na chuo je wataharibika? Sijaona pointi ya maana katika barua yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…