Barua ya wazi kwa Yanga management na Wanayanga wote' Timu inahitaji SOPs sahihi

Barua ya wazi kwa Yanga management na Wanayanga wote' Timu inahitaji SOPs sahihi

FRESHMAN

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2011
Posts
9,137
Reaction score
34,793
habari wanayanga wote.

huu ujumbe nitashukuru sana tukiutoa kwa pamoja kwa kuweka maoni yetu kwa timu yetu pendwa..

najua wengi tunaona yanayotokea kwa timu yetu.. mishahara ya wachezaji, gharama za usafiri na mengi yamekuwa kitendawili kisa tajiri wetu mpendwa.. mwanayanga mwenzetu manji amekaa pembeni..

Huwa nawaza sana hali hii ya kumtegemea mtu mmoja au kikundi cha watu wachache matajiri kuzamini na kuendesha timu itaisha lini ? nawaza tu siku manji akifariki, je tutaenda kumlilia mke wake kumuomba hela za mishahara hata kama yeye haipendi yanga au hapendi mpira?
ningependa sana kuona timu inaondoka huu mfumo wa kumtegemea mtu mmoja au wachache kiholela..


Maoni yangu mimi ni haya..

1. Yanga haifanikiwi na ni maskini sababu ya vipaumbele vya pesa na matumizi mabovu

hapa namaanisha timu ambayo haina kipato kikubwa imeajiri watu wengi sana ambao wanalipwa mishahara na posho ila role zao au majukumu yao hayana ulazima.. vyeo kama msemaji wa timu etc vingefutwa kupunguza gharama za mishahara msemaji wa timu anabaki kocha tu.. kama ulaya vile..

wangeitwa wataalamu , makampuni ya taaluma kama pwc, kpmg, delloite etc waje wathaminishe majukumu ya kila cheo.. kisha washauri role gani ziunganishwe na role gani zifutwe baada ya hapo kuwe na redundancy ya wasio na ulazima, na pia mishahara ipangwe kwa uhalisia..

2. Yanga haifanikiwi sababu ina poor marketing policy

hapa namaaisha yanga haijatangazi inavyotakiwa,, haitumii jina lake na mtaji wake wa mashabiki mamilioni kutengeneza pesa zake yenyewe.. mfano haina strong website, social network accounts, online tv etc... yanga ina uwezo wa kuwa na tv yake hata online tu kama millard hayo ambayo ingeendeshwa kisasa ingepata matangazo yake kama vodacom, tbl na makampuni binafsi, na bado kula hela za adsense ambazo zingeongeza mapato ya timu.. strong instagram accounts zingepost matangazo pia kama WCB wanavyofanya.. sitaki amini diamond ni smart than yanga management

3. ufatiliaji wa matumizi mabaya ya nembo na mauzo ya jezi feki ni mbovu

Hapa namaanisha mashabiki wengi wa yanga tunavaa jezi feki.. jezi zimejaa kariakoo na nchi nzima zina nembo za yanga ila ni feki... yanga haipati hata mia mauzo ya zile jezi feki.. unaenda taifa unakuta mashabiki wa yanga tumejaa kibao na njano na kijani zetu.. ila karibu wote tumevaa jezi feki ambazo club haijapata hata mia... kuwe na watu wa kufatilia wauzaji wa jezi feki na kuwashtaki na kwa kushirikiana na jeshi la polisi hii inawezekana kabisa ikiwekwa mfumo mzuri.. mauzo ya jezi yaifaidishe club..

4. Matumizi mabovu ya michango ya wanachama nayo ni sababu ya timu kulia ukata

wanachama tunalipia kadi kila mwaka, ila hela hizo hazieleweki zinaenda wapi... dunia ya sasa hela zinavunja uaminifu.. kuwe na mfumo rasmi wa kucontrol hela.. kila hela itoke kwa sababu.. hata kama ni 1000 tu au mia tano itoke kwa mbinde baada ya kuidhinishwa na ma signatories kibao...

hela ikiwa inatunzwa vizuri hii itashawishi hata mashabiki tukichangishwa tunatoa kwa moyo.. kuna wamachinga, wauza chips, boda boda, mama lishe wengi tu hawana kipato kikubwa ila wanaipenda sana yanga yetu,, kwamba ukimwambia arushe 1000 tigo pesa kuchangia timu yake yanga anatoa kwa amani kabisa.. ila sababu anajua kwa sasa hata nikitoa inaliwa na wezi viongozi na kulipana maposho hawezi kutoa kiurahisi...

mwenyekiti manji aliwahi kusema idadi ya mashabiki wa yanga ni kama milioni 35.. sina uhakika kama ni sahihi

Eti Yanga ina mashabiki 35 milioni!

sasa timu yenye mashabiki wengi hivyo inalia njaa.. si zaidi ya uchizi

timu yenye mashabiki wengi hivyo haijawai fika hata nusu fainali ya caf champions league.. kweli ujamaa umetulemaza.. yanga ni kubwa kuliko mazembe, kubwa kuliko enyimba, kubwa kuliko zanaco, kubwa kuliko APR sijui tumelogwa na nani


wanayanga wengine mnaruhusiwi kutoa maoni yenu.. Tunakosea wapi

Mimi yanga kwa jinsi navyoipenda hata kwa kukopa sishindwi ichangia buku buku kila mwezi.. kama tukiamua wanayanga tulipe mishahara ya wachezaji wenyewe kwa kuchanga.. ila sitachanga bila kuona mfumo rasmi wa kuzitunza hizi pesa za michango

by freshman aka Adam mwanayanga tawi la yanga Mabibo Hostel
 

Attachments

  • yanga.jpg
    yanga.jpg
    43.6 KB · Views: 51
Good maoni lakin utendaji na ufuatiliaji ni zero kabisa
 
kiukweli mimi ni simba lakini mleta mada umenipa changamoto ya kufikiri. Iwapo simba na yanga zingekuwa na viongozi waaminifu na wabunifu kwa kweli si Mo wala Manji wangehitajika. Simba na yanga zingeweza kabisa kuuza haki ya kutengeneza promotional materials kalamu, vikombe, scafu, stika, jezi n.k. jumlisha udhamini wa azam,vodacom, spoti pesa jumlisha matangazo ya makampuni mbalimbali kama mo sembe na quality group jumlisha viingilio milangoni jumlisha baba lao kadi na michango ya wanachama ya kila mwezi.

Kwa mfano viongozi wa yanga sasa wanahangaika kumbembeleza Manji na wanamuona kama mwarobaini najiuliza iwapo manji atagoma kurudi yanga hakika kwa aina ya viongozi waliopo yanga inaweza kabisa kushuka daraja. Nilitegemea kwanza wafungue akaunti ya dharura na watia saini wawe watu maarufu wanaoipenda yanga na wanaoamininka na uma wa watanzania kama akina Mkuchika, Mama Fatma Karume, Mzee Jabiri Katundu au Mwigulu na viongozi wote waliochaguliwa watoke dar makao makuu waende mikoani kwa kupitia viongozi wa matawi ya yanga wa kila mkoa waitishe harambee nina hakika zingepatikana pesa zaidi ya hata alizowekeza Mo simba. Lakini viongozi waliopo Yanga wao wanaota Manji tu arudi je asiporudi?

Kwa hali ilivyo sasa na aina ya viongozi waliopo unategemea kweli mpenzi wa Yanga atoe mchango wake wa 1,000? Mpenzi huyohuyo wa yanga akijua kuwa 1,000 atakayochanga Mwigulu atahakikisha inafika kwa uchezaji nina uhakika atakuwa analipa hiyo 1,000 kila wiki sasa tujiulize iwapo watatokea wapenzi 10,000,000 wakajitolea 1,000 kila wiki kwa mwezi ni kiasi gani kitakusanywa?. Ni wakati sasa wa kuchagua viongozi waaminifu wenye upeo mkubwa ambao wataweza kuorodhesha matawi yote Tanzania na kuangalia jinsi gani yanavyoweza kusaidia hivi vilabu. Pia kutengeneza mfumo mzuri ambao hata wapenzi wa hivi vilabu wasio wanachama waweze kuchangia kwenye hizi timu wanazozipenda. Kwa hili la kuchangia kila mwezi naamini wapenzi wengi wa Yanga wapo tayari lakini je pesa zao zitasimamiwa na nani?
 
nina maoni tofauti...ubinafsishwaji ndio muarubaini wa timu zetu Tanzania..wauze shares kwa matajiri kama watani walivyoanza...Yanga ni brand kubwa kuliko Simba...bingwa mara 27,makundi CAF mara tatu....
 
nina maoni tofauti...ubinafsishwaji ndio muarubaini wa timu zetu Tanzania..wauze shares kwa matajiri kama watani walivyoanza...Yanga ni brand kubwa kuliko Simba...bingwa mara 27,makundi CAF mara tatu....

una point ila kuleta mambo ya simba na yanga humu sio nafasi yake.. hapa ni kuishauri yanga tu.. sio mambo ya majungu kwa wapinzani... timu itabinafsishwa vipi bila kuthaminishwa kwanza.. je thamani ya yanga ni bei gan na kila share iuzwe bei gan?
 
una point ila kuleta mambo ya simba na yanga humu sio nafasi yake.. hapa ni kuishauri yanga tu.. sio mambo ya majungu kwa wapinzani... timu itabinafsishwa vipi bila kuthaminishwa kwanza.. je thamani ya yanga ni bei gan na kila share iuzwe bei gan?
Hakuna majungu thamani ya timu ni vikombe..Manji alisema thamani ya Yanga ni bilioni 40..ndio maana wakina mzee Dalali walipinga bilioni 20 Simba kubinafsishwa...natumia Simba kama case study...wataalamu Yanga tunao wengi tena wenye weredi mkubwa...toka 2006 katiba ilivyotaka Yanga kubinafsishwa muda huu tungekuwa kwenye levels za Mamelod Sundown,TP Mazembe,Zamalek nk...
 
Wakati Dismas Ten anaingia Yanga niliamini kabisa kwa maono yake atafanya kitu fulani kiwe mfano kwa hivi vilabu vikubwa viwili. Mwanzoni kweli alijaribu mambo mawili matatu hivi ya kuleta maendeleo ila sijui alikumbwa na nini au alikwamishwa na nini. Ila Dismas imani yangu kwako kuwa utafanya jambo kubwa bado ipo.

Hebu anza na hili la data base ya wanayanga wote Tanzania kwa kuanza kuorodhesha wanachama na baadaye wapenzi then tengeneza mkakati muwe mnaondoka makao makuu na kwenda mikoani kuchangisha fedha, kutoa kadi kwa wanachama wapya na kuhimiza wanachama kulipia kadi kila mwezi. Mnaweza hata kutumia redio, mitandao ya simu na magazeti kufanya kampeni hata wiki moja kabla hamjaenda mkoa husika na matawi yote ya mkoa husika yashirikishwe kikamilifu. Na kipindi ligi imesimama mnaweza kuwagawanya wachezaji wenu maarufu kila kanda wakacheze hata mabonanza haya ya uchangiaji na hata kuwaomba wasanii wanaoipenda yanga mkawalipa kidogo kama sehemu ya mchango wao mkaandamana nao huko mikoani. Jambo lingine hili zoezi liwe linafanywa na Yanga kila inapoenda kucheza mechi za ligi mikoani itangulie timu ya viongozi kutoka makao makuu hata siku tatu kabla ili iende kuuza brand ya timu yao na kutengeza pesa ambazo zitasaidia kupunguza gharama zilizotumika kuipeleka timu kwenye huo mkoa. Naamini mkifanya hivyo suala la mishahara na hata pesa ya kusajili wakati wa dirisha dogo disemba itakuwepo.

Haya yanaweza kufanyika kama mkakati wa muda mfupi wa kuiokoa yanga ili iweze kujiendesha kwa kipindi hiki cha mpito. Huko mbele ya safari akitokea mbia kama alivyo Mo kwa simba itakuwa vizuri lakini kwa kipindi hiki lazima lifanyike jambo la haraka kuitoa yanga hapa ilipo. Hivi viongozi wa Yanga wanajua jinsi gani wapenzi wao wanavyoumia huko mikoani kwa kushindwa kusajili wachezaji wa maana? Basi kwa maumivu hayo wanayoyapata wapo tayari kuchangia pesa kidogo hata 1,000 lakini kinachohitajika ni uwazi na watu wanaoaminika kwa uma kuwa pesa zao zitafanya matumizi sahihi.
 
Back
Top Bottom