Barua ya wazi mamlaka husika

MANYASANI

Member
Joined
Jun 15, 2013
Posts
46
Reaction score
13
BARUA YA WAZI KWA MAMLAKA HUSIKA ZOTE, JUU YA SWALA LILILOMKUTA SHILOLE KWA KITENDO CHAKE CHA KUONEKANA AKIWA ANATUMBUIZA NCHINI BELGIUM HUKU SEHEMU ZAKE ZA MWILI ZIKIWA NJE MIEZI KADHAA ILIYOPITA,,HALI AMBAYO KISHERIA NI KOSA NANIUKIUKAJI WA MAADILI YA SANAA YA TAIFA LA TANZANIA,JAMBO AMBALO LIMEPELEKEA MWANAMAMA SHILOLE AFUNGIWE KUFANYA KAZI YA MUSIC NDANI NA NJE YA NCHI KWA MUDA WA MWAKA MMOJA NA MTU ATAKAEMPA ULISHIRIKIANO ATAADHIBIWA VILE VILE….

KABLA SIJAENDA MBELE NAPENDA NISEME YAFUATAYO;

Ø Moja kabisa naipenda Tanzania maana ndio nchi yangu na ndio mahala pekee ambapo najivuna kwa kusema am a Tanzanian.
Ø Pili ninaieshimu katiba yetu ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kama ilivyo na maudhui yake
Ø Tatu naheshimu sana utawala wa sheria.
Ø Nne naheshimu mihimili yote ya dola yaani mahakama,serikali kuu,bunge,,, ukijumlisha vyombo vya habari na vyombo vya ulinzi na usalama.
Ø Tano ninaamini sana katika kumshauri mtu kuliko kumuadhibu kunakompoteza zaidi.
Ø Sita naiogopa sana sheria ya makosa ya mitandaoni.
Ø Saba mimi si funs wa shilole na wala sijawahi kuingia hata show yake mo
ja.




PIA KABLA SIJATOA MAONI YANGU NA MAPENDEKEZO YANGU I HAVE TO DECLARE MY INTEREST;
Kwanza ifahamike kabisa mimi si mtaalam wa maswala yakisheria ila ni mtaalamu katika maswala ya social protection/social security kwa lugha rahisi hifadhi ya jamii ambayo kazi yake kubwa nikuhakikisha binadamu yeyote yule anapata huduma muhimu kama chakula,mavazi,makazi,huduma ya afya,elimu bora,ama misaada ya dharula,,pia kuhakikisha haki yakuishi na haki za msingi za binadamu zinalindwa,,,ukiachilia mbali social protection ya formal yenye mifuko ya hifadhi ya jamii ambayo hutoa mafao kadhalika kwa members wake.

KWANINI IMENILADHIMU KULIONGELEA SWALA LA SHILOLE;

Ø Kiukweli nimeguswa sana na adhabu aliyopewa kwa maana rahisi shilole atakuwa ni kama unemployed person,kwa kuwa ajira yake imefungwa kwa muda wa mwaka mzima, ikizingatiwa hajaajiriwa ila amejiajiri mwenyewe hivyo maana ake atakuwa ni jobless for one year,,je mmewahi kusikia unemployment benefit hapa Tanzania kifupi haipo maana ake shilole kama hana kazi nyingine yakumuingizia kipato sijui ni vipi atayamudu maisha.

Ø Lakini pia nimetafakari kwa kina sana je kwenye ajira yake hiyo shilole alikuwa ametengeneza ajira kwa watu wengine kama wangapi vile nikasema wenda ni wengi je hawa watu wanaathirika vipi kiuchumi jibu ni sana, kazi kubwa ya social protection ni kuhakikisha ubora wa maisha ya binadamu unakua kila siku,hivyo baada yakuona vile nikajiuliza pia je katika sheria husika hakuna adhabu mbadala ambayo athari zake zisiwe kubwa hivyo,
Ø Swala lingine lililonipa hamasa yakuandika nikuwa shilole anategemezi wangapi,nikasikia ni mama mwenye watoto pia,je sasa kwa huu muda wa mwaka bila kushughulika na kazi yake ya muziki je atamudu gharama jibu likawa inatia shaka,hapa social protection imeguswa moja kwa moja kwenye wajibu wa mzazi kulea watoto,hapa watoto wataathirika ambapo wajibu wa hifadhi ya jamii nikuhahakisha watoto wanapata elimu bora,maisha bora nakuishi katika mazingira salama.

Ø Je kisaikolojia Shilole atakuwa katika hali gani kwa ufupi bila hata kuficha mbaya sana ,kwa utafiti mdogo wa chini tu nikuwa huu mwaka ndio mwaka wa shilole yaaani kama ameanza kupenya kimataifa kwa kasi,ni kama vile kapokonywa Tanzanite,hivyo itamuathiri sana nainaweza kuharibu maisha yake kwa ujumla maana hata reaction inaweza kumuumiza,pia hapa hifadhi ya jamii inaguswa kwa kuwa inawajibika katika kuhakikisha kila binadamu anakuwa certain to life and not uncertain ambayo inamfanya awe vulnerable to risk,hivyo akiwa kama mama kisaikolojia akiumia ni pigo sana kwa watoto wake na familia inayomtegemea.

Ø Vipi kuhusu mapato yanatakayopotea kuingia kwa serikali sio mengi sana lakini yapo yatayopotea kutokana na shilole kufungiwa muziki kwa mwaka mzima,,japo ni asilimia 0.0 zisizo na mwisho lakini kuna kitu kwenye uchumi kitaguswa.

Ø Kingine nilichojiuliza sana je ni kweli adhabu hii ambayo wenda ni kama nyundo itakuwa imemrekebisha shilole kwa kipindi hicho au wenda ikampeleka kubaya zaidi hata baada ya adhabu hiyo akapotea kwenye industry ya fani yake,maswali juu ya shaka yangu hii yanakuwa makubwa sana.

Ø Nini hatima yakipaji cha mwanadada huyo shilole katika kipindi cha adhabu chote,,,je sanaa yake itaweza kusubiri mwaka kisha aje arudi kwenye chati na ajijengee jina kama alilonalo sasaa au ndio inakuwa haifahamiki,,kwangu mimi kama mtaalam wa hifadhi ya jamii naguswa maana natambua sana tatizo la ajira ambalo linagusa vijana walio wengi hivyo kwa mtu aliejiajiri akipoteza nyenzo ni tatizo sana.


MAPENDEKEZO YANGU;
Ø Kwa wale wanaoijua sheria hiyo ambayo inaipa nguvu BASATA kumuadhibu msanii au mwanachama wao pale anapokiuka maadili ya sanaa Tanzania,haswa wanasheria ninatoa rai ya dhati kabisa kama uwezekano wakumuokoa Shilole atoke kwenye janga hilo msaidieni kwa uwezo wenu wote mtakuwa mmeliokoa taifa kuwa na vijana wengi wasio na ajira.

Ø Ninaiomba BASATA kama kuna adhabu mbadala yeyote ambayo itamjenga shilole si kumbomoa basi wampatie ila hii yakumfungia asifanye kazi yake waifikilie sana, Yule ni kijana pia ni mwanamke,,pia mama mwenye watoto anaowalea,,tunasema wanawake wakiwezesha wanaweza tumwezeshe shilole madhaifu yake yasitukatishe tamaa katika harakati zakumkomboa mwanamke tanzania.

Ø Wanaharakati wanawake na asasi zote zenye kutetea wanawake msikae kimya msaidieni najua kuwa mtadai aliwadhalilisha kwa kitendo na matendo yake, lakini jikazeni msameheni katika hili mpeni ushirikiano wakutosha mumuokoe kuliko kumuacha peke ake maana mazara yaake nimakubwa sana.Obama mwenyewe akiwa Kenya amekiri kuwa mwanamke akiwezeshwa ni jambo jema katika Taifa na pia ni kulikoa bara la afrika kuondokana na umasikini.

Ø Mheshimiwa waziri wa wizara husika nakuomba sana kama kuna sheria ambayo inakupa mamlaka yakutengua maamuzi hayo yaliyofanywa na chombo kilicho ndani ya wizara yako,nakuomba kwa moyo wakizalendo nahekima muokoe kijana mwenzetu Shilole,msaidie naimani zipo adhabu hata kijamii ambazo zinaweza kumrekebisha ila kufungia kazi yake nisawa nakumkaribishia njaa na umasikini,,,mheshimiwa waziri kama watu wangejua dada zetu waliokata tamaa kazi wanazofanya usiku ni kheri hata mumuadhibu kwa adhabu hata yakufagia barabara au hata kufyeka bustani ya ikulu au hata kupikia uji wanafunzi wa jangwani kwa muda flani.

Ø Mwisho ni ombi kwa raisi jamhuri wa muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kama mamlaka zote zinashindwa kumsamehe ama kutengua adhabu hiyo ,aliyopewa mwanachi wako ambae ni mwanamuziki Shilole,,wewe ndie mlezi wa taifa hili, wewe ndie unaweza kutoa msamaha,Nakuomba sana tumia nafasi yako umwezeshe kuepuka mtihani huo ambalo ni pigo kubwa sana kwake.muombee hata apewe adhabu nyingine yeyote lakini sio kufungiwa muziki ambayo ndio kazi ake,,ni ombi hili langu binafsi ambae najua adha na changamoto ambazo dada zetu na mama zetu zinawakumba katika harakati za maisha.

MAONI YANGU
Ø Simtetei shilole kuwa alitenda mema hapana la hasha,hata kama katenda mara ngapi inabaki pale pale kila mwanadamu anamapungufu yake na binadamu hupokea mabadiliko kwa muda mrefu sana,,pia ikumbukwe kabisa katika maisha yetu historia zetu huja kututesa sana baadae ndio maana bado inatupasa tumpe muda apokee mabadiliko ambayo yatamjenga kuliko kumpa adhabu ile inayommaliza kabisa.

Ø Ninatambua ishu ile ya Shilole ni kweli ilidhua mjadala bungeni nakuleta sintofahamu,lakini kwa tetesi shilole aliomba radhi kwa yaliyotokea hata yeye hayakumpa amani.katika hili la wabunge kuliijia juu ni haki na ni wajibu wao kabisa kikatiba kulinda hadhi ya taifa letu, je ikitokea kwao wamerekodiwa katika maficho ama kupigwa picha pasipo hiari yao, je ni kweli watafukuzwa ubunge moja kwa moja nakusitishiwa haki zao za msingi?

Ø Nashauri sana sheria hii ambayo inaipa mamlaka Basata kufungia Msanii kwa kipindi mpaka mwaka ni kheri kabisa ifanyiwe marekebisho kutegemea na makosa menyewe, ni bora ikaweka adhabu kubwa za faini ama adhabu za kuhudumia jamii kuliko kufungiaa kwa vipindi virefu ambavyo vinaathari kali na ambazo hazibebeki kabisa kwa wasanii wetu wachanga ambao wanatoka katika maisha yetu magumu.

Ø Naamini sana taifa letu linapitia changamoto nyingi na sote tukubaliane tulipokubali capitalism sytem,tulikubali soko huria ambalo ndilo limeleta utandawazi ambao ndio unatutafuna,hivyo turekebishane,tushauriane pasipo kuvunjika moyo,tusimtenge shilole sote tuna mapungufu,ukiangalia alieopost zile picha hakua nania nzuri kabisa.

Ø Shilole popote ulipo fuata taratibu kama zipo,jipaganie usikate tama nausikubali kushindwa,wewe ni mtanzania na Tanzania ni nchi yako,na haki yako sehemu ya mwisho kuipata ni mahakamani kama italadhimu ufike huko nenda,naamini mahakama zetu zinasimamia haki na usawa kwa wote,,mungu akuongoze.


HITIMISHO
Ø Ninaamini nimetumia haki yangu kikatiba ya uhuru wakutoa maoni pasipo kuvunja sheria wala kutumia lugha ya kuudhi,nimetimiza wajibu kwa kuangalia hali halisi ya mama zetu na dada zetu ikiwa ndio wanaotuzaa nakutulea pia, na ndio wanaotuzalia watoto pia,nimeshindwa kukaa kimya kwa kuangalia uhalisia wa maisha yakitanzania kanda zote haswa mijini nayajua, naamini mawazo yangu yatapata kufanyiwa kazi hata kama si leo naamini kizazi kinachokuja.

Ø Napenda ieleweke kabisa nimeandika ujumbe huu kwa dhumuni moja tu kuwa Shilole apewe adhabu yoyote itayomfunza kulingana na kosa lake lakini sio itayomtia umasikini na njaa .sote tunajua kwanini vijana wengi wanafanya biashara zisizo halali ni kwasababu ajira hamna.
 
huyu lowasa..pipo zilokua zinamkandia...leo hii kila.mtu team lowasa....maniner!!!
 
Unapowasilisha mada rasmi kama hii jifunze matumizi sahihi ya alama kwenye uandishi.
Umeanza aya kwa kutumia irabu 'ø' jambo ambalo sio sahihi. Kwa muktadha huo alama kama vile '-' '.' Nukta kubwa zingeliweza kutumika. Kumbuka vijana wetu wanajifunza kupitia maandishi rasmi kama haya. Tumia lugha rasmi kuwasilisha mada rasmi.
 
Upo na lowasa hapa umeitwa usome???
Hao basata nao wamezidisha lol.... wakaa uchi wapo kibao insta, watukanaji matusi ya ndani wapo why shilole?? kama ni matiti kuwa wazi haikua makusudi ni ajali kazini na aliomba msamaha imekuaje wamfungie
 
Tasnia ya sanaa lazima iheshimiwe! Usitetee uchafu! Sitti Mtemvu amesababisha MISS TANZANIA ifungiwe na BASATA sembuse huyu mpuuzi mmoja, mjinga mmoja: kama alikuwa anategemea sanaa basi angekuwa na heshima na kazi yake!
 
Mrembo by nature asante sana. Nimekupenda tangu uhamie chadema
 
Kama vipi Shilole nae ahamie Ukawa. Wakimwaga mboga unamwaga ugali tu
 
huyo shilole alishaonywa kipindi cha nyuma akaahidi kutorudia makosa, kwa hili sakata la pili aliitwa kutoa maelezo hakujitokeza pamoja na ajira anayotengeneza madhara kwa jamii ni makubwa sana hasa kwa sisi wenye familia adhabu aliyopewa ni ndogo sana inabidi nyinyi manaojiita wataalamu wa mambo ya jamii muwe mnawaonya hao watu kwanza na sio kusubiri wakifanya makosa ndio waadhibiwe ndio mnajitokeza mwisho hata wauza unga nao wanatengeneza ajira kubwa lakini madhara kwa jamii ni makubwa kuliko hata faida ya ajira wanazotengeneza
 
MTOA mada Nadhan HUENDA umetumwa.Hivi unataka mtu afanye kitu gani Nje ya Nchi cha kudharirisha taifa ndipo use me hapo Sawa?HUYO Dada hana maadili na nadhani BASATA wamechelewa kumpa adhabu na pia wamempa ndogo.Kuhusu watoto,mtu anapofanya kosa huwa hategemei familia yake iwe defence yake Bali kutotenda kosa,HIVO kuwa na watoto haina maana asiadhibiwe.Pia ajira alizotengeneza so hoja kwani angekufa nao watu wangetegemea wapi ajira? Mwisho ni kuwa Angalia rekodi yake kwenye mitandao ikoje??
 
Hamna la maana zaidi ya kutukana?
 
Ungetumia mda huu kushauri wengine wanaoanika duduz zao,halafu Shilole akaongezewa adhabu kama mfano.nyie si mnanufaika na hizo tupu ndo maana mnatetea
 
Hebu tupieni hizo picha kwanza ili na sisi tushauri kihalali!!
 

Sio bure, unatafuta kiki nini ya kutokea na we mada zako vilevile zitupiwe macho😉😲? Hebu tafakari mada nyingine
 
Humu ushabiki mwingi unawapofusha Watu kwenye Mambo ya Msingi, Afande sele alivua nguo jukwaani aliadhibiwa? Bongo movie ngapi Wanawake wanavaa Uchi tofauti kabisa na maadili ya kitanzania hao basata wana video hadi majumbani mwao.

Stupid Decision!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…