Dr leader
JF-Expert Member
- Jun 28, 2016
- 893
- 1,021
BARUA YA WAZI
1 Nawasalimu kwa jina, jinale la jamhuri
Kwako wewe kamishina, uigongae mihuri
Wasimamizi wa shina, msome pasi kiburi
Hii barua ya wazi, kwenu nyinyi viongozi
2 Upapo mwingi uhaba, wa ajira hapa nchini
Sisi twajaza vibaba, viwango vyetu vichini
Hatutaki vya kukaba, licha ya nguvu mwilini

3 Nasi tumejiajiri, kwayo midogo mitaji
Nimesikia habari, kwamba hamtuhitaji
Kwa maneno ya kejeri, na wala tusiyahoji

4 Kweli tubarabarani, na turadhi kuondoka
Yako wapi masikani, yaliyotoshelezeka
Kutuweka ndani ndani, watu wasieze fika

5 Hamtaki ushauri, tuamue kwa pamoja
Na mazingira mazuri, hiyo ndio yetu hoja
Wamachinga tuko furi, na bado twajikongoja

6 Hapa niitie nanga, ujumbe uwafikie
Tuendelee kupanga, ridhiki tujipatie
Wapenda manga na shanga, karibu mjitwalie

[emoji2399]Abuuabdillah [emoji3578]
0744883353
jumaomari5@gmail.com
Kilimanjaro Tanzania