Rijali jandoni
JF-Expert Member
- Apr 5, 2018
- 1,936
- 1,972
Habari wanajamii napenda kumshukuru MWENYEZI MUNGU mwingi wa rehema kwa kutupa neema hii ya pumzi mpaka muda huu
Barua yangu hii fupi naomba niweke mahususi kwa viongozi wa nchi wakiongozwa na Mheshmiwa Raisi na wasaidizi wake wote katika kila taasisi naimani ni wenye afya na mko salama kabisa.
Kwa dunia ya sasa yenye kasi ya maendeleo kwenye kila nyanja, Tanzania kama nchi moja wapo hatuwezi kukwepa hii hali. Kwa kutambua hilo naimani viongozi mlishaweka utayari wenu juu ya haya mambo muhimu kwa taifa letu lenye idadi kubwa ya vijana wa rika la kati (17-40 years), tukiwapuuzia ama kuwaacha tuna uwezekano wa kutengeneza taifa lenye watu waliokosa maadili na misingi ya kijamii itakayo pelekea vijana wasio na aibu wala utu hasa kwenye kuharibu, kuiba hata kutokuwa na huruma na mali za watanzania na za nchi yetu kwa ujumla.
Kuzuia haya mambo tunaweza endeleza hizi sera na kisha kuyafanyia kazi kwa kipindi cha (5-10 years)
1. UJENZI WA VYUO VIKUU KATIKA MAENEO YAFUATAYO
Viongozi hasa wabunge maana wao ndio waendeleza sera na sheria za nchi yetu wakiwa ndani ya bunge, wajitahidi kuweka mikakati itakayo saidia miji yenye shule kubwa za sekondari hasa kidato cha sita kuwa na vyuo vikuu hii itachangia uendelezwaji wa mikoa ilio na watu wengi yaani vijana na italeta maendeleo katika eneo husika kwenye upande wa ajira na shughuli tofauti.
Nimependekeza hili kwa sababu zifuatazo :
Nina uhakika viongozi wamekuwa wakisafiri na mara nyingi huona nchi za wenzetu kila mji wanaopelekwa kwenye nchi husika una kila hitaji la kijamii na umechangamka, hii hali huonekana hasa kwa nchi za ulaya na sasa imekuwa trend kwa nchi za bara la Asia hasa China, Korea, Malaysia na nyingine, hii imetokana na kupeleka maendeleo kwa kila mkoa na walilenga mno mikoa ilio na shule ili kuweka vyuo vikuu vitakavyo weza kutumika kama sehemu maendeleo ya kiuchumi kwa wananchi wa eneo husika na hata muda mwingine husaidia kuleta vijana na watu wapya, huu mchakato hutengeza fursa nyingi kwa wananchi wa maeneo husika na watu watakao enda huo mkoa (province).
Na hili hawakuanza na ujenzi wa vyuo kamili katika mikoa husika huenda walianza hata na vitivo yaani colleges na idara za utafiti (institutions) zilizo jiendesha na kusimamiwa vizuri vikiwa chini ya vyuo tofauti na kupelekea kupata vyuo kamili hapo baadae hii imetumika hata kwetu kwa upande wa chuo cha dar es salaam kuzaa muhimbili na idara nyingine.
Kwa namna hii tutaweza jengaa nchi katika kila kona si tuu kiuchumi wa fedha ya mkononi au kiusalama na siasa bali itakuwa kwa vitendo zaidi maana itapelekea uwekezaji wa eneo husika kuongezeka kwenye upande barabara, hospital, majengo ya biashara pamoja na mambo mengine.
Na itapunguza wingi wa vijana kwenye miji mikubwa Tanzania kama dar es salaam kwa sababu za kusoma na kutafuta maisha.
2. KUTENGENEZA BUSINESS HARBORS, YAANI BANDARI AU MAENEO MAALUM NA YA KIMAKAKATI KWA AJILI YA BIASHARA.
Katika nchi zilizo endelea na zinazozidi kuendelea bila shaka kila msafiri kutoka Tanzania anae enda nchi husika hufikia eneo fulani lenye pirika nyingi za biashara. Ndugu viongozi hili jambo kwa wenzetu sio bahati mbaya waliweza kutenga miji yao kwa shughuli husika.
Kuna baadhi ya nchi ukienda miji fulani ni maalum kwa ajili ya shughuli za kisiasa huko kuonana na pirika za biashara ni kwa upande fulani tena mdogo pembeni kidogo ya mji. Lakini likija swala la biashara kubwa na zenye kipato kwa taifa na hata zinazo wasaidia wananchi wao basi kuna mikoa imetengwa maalum kwa ajili hiyo.
Sisi kama Tanzania tunaweza fanya hili tuweke mfano hapa mikoa inayo husika na rasilimali za madini yawekwe na kuundwa kimkakati ili hata mtu akihitaji kito anajua kabisa hili linapatikana sehemu hii shinyanga.
Na wananchi wa eneo hilo waandaliwe kukabiliana na changamoto hata maendeleo ya sekta husika walio saidiwa kutangaziwa serikali na viongozi wake.
Tukija miji kama Tanga,Mtwara, Mbeya, kagera, Kigoma, Arusha, Moshi, dar es salaam imekaa strategically kwenye biashara kuna nyingine ni special kwa kupokea mizigo na kutoa kwa sababu ya kuwa na vyanzo vya usafirishaji kama Bahari. Na hii mingine imepakana na nchi tunazo shirikiana nazo kwa ukaribu kwenye masuala ya biashara. Katika haya maeneo tunaweza kuanzisha viwanda mbali mbali kwa bidhaa zinazo uzika nnje ya nchi, kwenye hili swala hatuna budi kukaa na sekta binafsi na wamiliki wa viwnada ila hii pia itapendwa zaidi kama eneo husika likiwa na idadi kubwa ya watu.
Kwa sababu kwenye kila nchi ilio endelea wakijenga na kufanya jambo wanawaza mnunuzi wa kwanza awe mzaliwa wa nchi husika, ndio maana upandishwaji wa kodi kwa bidhaa zinazotoka hata kuingia (tariffs) na maswala mengine ya kiuchumi yakitokea bado wanapona sababu soko la ndani ni zuri pia.
(wanajamii mkiweza pendekezeni na mengine mengi hapo chini na nini kifanyike sehemu fulani ili kuleta maendeleo)
3.. itaendelea....
NOTE: hizi zinaweza tumika kama sera za viongozi kwenye uchaguzi na zisitumike kulaghai watu, kazi ifanywe na kama imefanyika basi iendelezwe ila kwa nidhamu viongozi wetu, ili kuiokoa na kuilinda Tanzania yetu