Barua za maombi ya kazi kuchanwa maofisini

Dawa ni kujiajili lakini kujiajili kuna taka maandalizi ya kutosha,yaani kupata elimu inayopelekea huko,kunahitajika mitaji, huwezi kujiajili kama huna mtaji,sera za serikali na vyama vya siasa kutupeleka huko,kutenga maeneo maalum kwa ajili ya kuwekeza,vivutio vya watu kujiajili km kutenga maeneo na kupunguza kodi,upendeleo maalum km kukuza vipaji nk.
Mfumo wetu bado ni wa kurithi kutoka kwa wakoloni,ambao walikuwa wanaandaa waafrika kuwasaidia kazi za kiutawala.
 
Ni ofisi ya umma au ya binafsi?
Je kazi ilitangazwa?
Kama ni ofisi binafsi/private na kazi aikutangazwa,
ulitaka afuge karatasi za nini wakati watu wanataka paper-less offices?
 
nampa pole sana huyo dada kama hii stori ni kweli!
inawezekana ametumia hela kuandaa hiyo application alafu mpuuzi mwingine anamfanyia unyama
lakini hr kama alichana akijua kuwa nafasi tayari inamwenyewe yuko sahii
inawezekana kuna cv,ambayo si vizuri ionekane kwa kila mtu

nikirudi kwa mtoa thread ,sijambo jema kudisclose information za ofisini kwako
vingine vinafanywa kulinda maslahi ya ofisi
siku nyingine jitahidi kuleta thread za kutia matumaini sio za kutisha wadogo zetu
 
Duh! Tutatoboa kweli kwa mtindo huu
mimi kuna kipindi niliitwa kwenye interview nilivyoingia nikaulizwa "what is your good name?"nikajibu.nikaambiwa basi subiri nje tutakuita interview ya pili.baadae wakatoka wakaita watu watatu.sisi tuliobakia tukawa tumeshindwa interview.nilishangaa lakini pia nilicheka sana.
 
Duh!Aisee,inauma saana.Kwa mfano huyo Hr wenu nae ni member humu jamvini,na ktk fukua fukua zake akafanikiwa ku uona huo uzi uliou post huoni kua utakua umekiotesha nyasi kibarua chako?Cause,obvious atajua ni wewe.

Potelea mbali! Naweza fanya kazi popote cv yangu nzuri!
 
Ni ofisi ya umma au ya binafsi?
Je kazi ilitangazwa?
Kama ni ofisi binafsi/private na kazi aikutangazwa,
ulitaka afuge karatasi za nini wakati watu wanataka paper-less offices?

Hii ni public company, tena ni one of the leading in the industry. Sio kampuni ya kichochoroni!
 

Kipi bora kati ya kuishi kwa matumaini ya uongo na kufahamu ukweli unaouma?
 
Wala usivunjike moyo. Mie naamini in fate, kuna mahali Mungu akikupangia hata wazibe na wagaragaze watakuja kuachia tu. Usimsahau Yusufu, aliepangiwa kuwa mkuu na kusaidia familia yake. Wakamuuza na kuuahirisha mpango wa Mungu, lakini mwisho wa siku ikawa tu. Ndugu wale wale waliomtupa ili miganda yao isisujudie wa kwake, wakaja kumsujudu.
 
kama kuna uwezekano wa kujiajiri inakuwa bora zaidi kuliko kutafuta vibarua ofisini kwa watu

Nakubaliana na wewe. Watu wakitoka vyuoni sasa hivi waondoe mawazo ya kuajiriwa na wawe na mtazamo wa kujiajiri wenyewe, angalau hili linaweza likaondoa utegemezi wa kuzunguka na bahasha mjini. Badala ya kupoteza muda mwingi kuzunguka na barua, ukitumia huo muda angalau kutafuta kitu cha kufanya itasaidia zaidi ya kuyafanikisha maisha yako zaidi.
 
Watu wanachoka sana kutuma maombi ya kazi kutokana na ukweli kuwa inapofikia nafasi kza kazi zikatangazwa, basi ujue zimeshachukuliwa ila kinachofanyika hapo huwa ni kukamilisha logistics tu.
 
nipe mtaji nijiajiri

MZURI SANA;Tumia akili yako zaidi kubuni nini cha kufanya bdala ya kuwaza mtaji. Mtaji siyo mpaka ujazwe mahela. Kuna watu wana hela na hawajui hata wafanyie nini!!!! Ujasiriamali siyo kuwa na mtaji ni kuwa na wazo la kufanya kwanza. Ukisha kuwa na wazo la kufanya lazima hela itapatikana tu kwa vyovyote vile.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…