BAS UTEREIJK: Fundi wa picha aliyetengeza picha ya Yesu na Pharaoh

BAS UTEREIJK: Fundi wa picha aliyetengeza picha ya Yesu na Pharaoh

Da Vinci XV

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2019
Posts
3,862
Reaction score
6,438
Wasalaam




Kuzaliwa katika zama hizi za maendeleo ya sayansi na teknolojia ,mara nyingi tunasahau jinsi mambo tofauti yalivyokuwa kabla yetu.
Watu wangeweza kujua tu mtu anaonekanaje kulingana na mtazamo wa msanii (mchoraji) au zile picha za black and white

Licha ya juhudi za wasanii katika kuchora, uchoraji hauwezi kufikia kiwango cha uhalisi ambacho picha zinaweza kuwa nazo.
Na kwa hivyo, watu mara nyingi hushangaa ni vipi baadhi ya watu mashuhuri wa kihistoria walionekana kwa kweli na ujinga wote wa zamani umeondolewa kwasababu ya maendeleo (picha)

Bas Uterwijk, mpiga picha kutoka Amsterdam, Uholanzi mtaalam kwenye maswala ya picha za kompyuta, michoro kwa 3D, na Special Effects , anajaribu kutoa jibu la swali hili linaloumiza vichwa vya watu wengi

Uterwijk ni maarufu kwa kutumia GAN (Generative Adversarial Network) kubadilisha michoro na picha za zamani za watu haswa watu maarufu kuwa picha. mfano wa picha halisi.


GANs ni darasa la mifumo ya ujifunzaji wa mashine ambayo ina uwezo wa kutengeneza picha za wanadamu zinazoonekana kama za kweli, na zenye mfanano kabisa na mtu halisi juu ya vipimo na muonekano



Yeye hutumia mchoro unaojulikana kubadilisha kuwa picha kama mtu halisi

Hizi ni baadhi ya kazi zake zipo nyingine nyingi (waweza mfatilia kwenye social net zake)



NEFRITI na PHARAO


Kutumia kwake akili na program ya bandia, mpiga picha wa Uholanzi Bas Uterwijk alitoa picha za kisasa za Mfalme Pharao Akhenaten wa Misri (Amenhotep IV) na Malkia Nefertiti.

Screenshot_20210401-010637.png



Screenshot_20210401-010116.png




JESUS (yesu)

Mpiga picha huyo wa Uholanzi bwana Bas Uterwijk ametoa mfululizo wa picha za watu maarufu, pamoja na Yesu Kristo pia, kama kawaida akitumia akili na programm bandia.

Picha ya mnazareth huyo ,kwanza inamwonyesha Yesu na ngozi ya kahawia, macho ya kahawia, na ndevu fupi.

Screenshot_20210401-010747.png


Screenshot_20210401-011040.png



STATUE OF LIBERTY

Hii Sanamu iko pale USA iliundwa tena na msanii Bas Uterwijk akitumia programu ya bandia...kutengenezea picha yake
Screenshot_20210401-011401.png


Screenshot_20210401-011542.png





GEORGE WASHNGTON

Raisi wa kwanza wa marekani, basi mtaalam Bas akamtengenezea picha yake nae iwe iliyofanana na picha halisi

Screenshot_20210401-012454.png




MONA LISA

Huu ulikuwa mchoro wa mwanasayansi nguli LEORNADO DA VINCI wenye sifa kedekede nao si haba bwana Bas akautengenezea picha halisi kuuleta katika muonekano halisi sa picha

Screenshot_20210401-012923.png





JULIO CAESAR

Wengi wetu haswa wanamtambua huyu bwana kutoka pale Roma Italy, basi bwana BAS hakuwa nyuma , akatengeneza namna anavyoweza kuwa anafanana naye katika picha halisi


Screenshot_20210401-013018.png
 
Nataka kusema waliochora picha kwa mfano ya Yesu si wamebuni tu hakuna anaeifahamu sura halisi ya Yesu.
Ni kweli hata DaVinci , aliwahi kufanya hivyo hii huwa wanafanya kutokana na masimulizi ya muonekano na vipimo

Ushawahi kusikia picha iliyotengenezwa kutokana na vipimo kwenye nguo aliyovikwa Yesu alipokufa kabla hajafufuka iliyohifadhiwa Italy????
 
Hiyo ya Jesus jamaa aliijuaje
Kwa kuhusu picha ya Bwana yesu jamaa alitoa tofauti tofauti kama tatu hivi

na kutoka kwa Teller Report‘s ambao walitafsiri makala moja ya Uterwijk kuhusu picha za yesu

Jamaa anasema

“For one of the images, I added a little historical truth,” anaeleza “In one of the three versions, Jesus has shorter hair because historians do not believe that at that time, in the region of Galilee, in Israel, a man could have had hair so long.” …


“Sometimes I try to be as realistic as possible and sometimes I try to give a representation of how we perceive a character in history,”

Alimalizia hivyo Bas utewrjk
 
Mafarao wengi walikuwa ni weusi ila wazungu hawataki waafrika tujue hilo sababu wanajua litaboost saikolojia yetu. Hatua yoyote ya mtu kujikwamua na kijiheshimu inaanza na saikolojia ya kusema "kumbe naweza"
Sio wengi ni kama wote walikuwa Blacks mapaharao watawala walioteteresha dunia zamani hizo

Na hio ndiyo silaha aliyotupiga nayo mzungu ,katuacha mbali sana saivi twajiona dhalili
 
Ni kweli hata DaVinci , aliwahi kufanya hivyo hii huwa wanafanya kutokana na masimulizi ya muonekano na vipimo

Ushawahi kusikia picha iliyotengenezwa kutokana na vipimo kwenye nguo aliyovikwa yesu alipokufa kabla hajafufuka iliyohifadhiwa Italy????
Hii ni mpya kidogo kwangu hebu lete hii simulizi mkuu tuone iliwezekanaje.
NB: Nakukumbusha jina Yesu ni nomino kwahiyo unapoliandika jitahidi uwe unaanza na herufi kubwa. Asante.
 
Back
Top Bottom