BASATA watishia kufungia Wasafi festival

brave one

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
4,879
Reaction score
7,386
BASATA wametaka Diamond na Rayvanny kufuta wimbo wa Mwanza kwenye platform zote huku wao wakiwalisiliana na mamlaka nyinginge.
Katika hatua nyingine BASATA wamesema iwapo wasafi watatumia nyimbo zilizofungiwa kwenye tamasha lao la wasafi festival hawatasita kulifungia tamasha hilo. Ikumbukwe nyimbo zilizofungiwa ni WakaWaka, Hallelujah na ya Sasa hivi Mwanza
 
Wamejifurahisha tu lakini hawawezi kuzuia tamasha hata kidogo,wewe huijui nchi yako siasa kila sehemu.Wema yule si unamuona wanasema kafungiwa muda usiojulikana,ngojea baadaye CCM wawe na event alafu Wema ashiriki kesho utasikia amefunguliwa.Tamasha litakuwepo na litafanyika ktk viwanja hivyo hivyo vya CCM au umesahau Chura ya Snura ilifungiwa lakini wakati wa kampeni za CCM ikapigwa mbele ya waheshimiwa na msambwanda akawatingishia.
 
wema kafanya hayo madudu kwa kuya rudia rudia... hatimae wana ishia kumuonya... Ila amber nan ßijui wana mgonga lungu... hahahahahaha
 
Basata wanatumika na clouds!

Comments zijazo!!
 
[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]
.................wewe huijui nchi yako siasa kila sehemu............................... au umesahau Chura ya Snura ilifungiwa lakini wakati wa kampeni za CCM ikapigwa mbele ya waheshimiwa na msambwanda akawatingishia.
 
Hii nchi ishakuwa ya kiislam sasa.
 
Hivi Hallelujah ilifungiwa kumbe? Huu ni wivu sasa[emoji849][emoji849]
 
Mkuu Nyani Ngabu alipost hili shairi juzi hapa Jf



Shairi la yule gwiji mshairi, si mwingine yule bali Amiri Abdalah Sudi almaaruf kama Andanega, lijulikanalo kama ‘Nyege ni Kunyegezana, nalo liliwahi fungiwa na hawa mgambo wetu wa maadili ya Kitanzania?
Kama hujawahi lisikia au kulisoma hilo shairi, nakuwekea hapa.
Furahia utunzi murua kabisa wa gwiji Andanenga:




Peni yangu Andanenga, uwino unapotona,
Mantiki huzilenga, na balagha na bayana,
Hufaidika malenga, huvurugika akina,
Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili.
Msemo wa Kiswahili, nyege ni kunyegezana,
Maana yaki kamili, wema ni kutendeana,
Wasiojua fasili, hunamba nimetukana,
Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili.
Ni msemo maarufu, ambao shaka hauna,
Kwenye kamusi sanifu, funueni mtaona,
Niwezeje kukashifu, nami mwana muungwana!
Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili.
Ninataja ukurasa, wazi hapa naunena,
Soma mbili moja tisa, soma bila ya fitina,
Msemo siyo wa sasa, si juzi licha wa jana,
Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili.
Ushairi kubwa fani, mithili yake haina,
Kujua zake bayani, yataka kikubwa kina
Muoneni mwafulani, hata kuku wamguna,
Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili.
Ulipotamkwa mlo, kaja akitunatuna,
Akakabwa koromelo, akabaki kugunaguna,
Kabakia lolololo, uzamani umechina,
Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili.
Alhaji Jitukali, pokea pongezi tena,
Kikubwa chako kilili, hapandi yule mtwana,
Atuache tule wali, yeye ugali wa dona,
Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili.
Kaditama wa Busara, na Mbwezi heko kijana,
Pongezi ndugu Kagera, Yobu has ante sana,
Ndimi Mshairi Bora, kipofu ninaeona,
Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili.
(Mshairi Bora)
Amiri A. S. Andanenga (Sauti ya Kiza)
SLP 4775,
Kinondoni Shamba
Dar es salaam.
 
Huyo jamaa anaongea kama ni personal issue. Anapaswa kuelezea kosa, sheria na kanuni zilizokiukwa, hatua zinazopaswa kuchukulia kwa kukiuka hizo kanuni na hatua walizochukua kiutekelezaji. Ukimsikiliza unaona kabisa kuwa analenga kabisa kuwachamba wasanii na lebo yao, ili wadharaulike katika jamii. Na adhabu waliyotoa ipo Kisheria au wanajipangia tu kwa sababu ni WCB?

Inawezekana kabisa kuwa wasanii walilenga ny*ge, lakini wao mametamka Nyegezi. Mengine ni tafsiri yao Basata na msikilizaji wa wimbo huwezi kumshika uchawi msanii kwa akili mbovu ya mtafsiri.

Hivi WCB hawawezi kuwashtaki Basata? Binafsi naona kama Basata watapata tabu sana kuprove kuwa kuna matusi kwenye huo wimbo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…