Ibrahim300
JF-Expert Member
- Nov 29, 2010
- 390
- 68
Hii Bongo Movies siku hizi imekuwa kama laana kwa kizazi cha siku hizi nchini Tanzania. Ni jambo la kusikitisha kuwa kila siku kila wakati utasikia mwigizaji huyu ama yule amepiga picha za ufuska na kuzianika kwa mtandao.
Jambo lililoniudhi zaidi ni hivi majuzi nilipoingia katika blog fulani ya udaku ya Jambo Tanzanian na kuona stori na picha za wasanii wa Bongo Movies wamepiga picha wakiwa uchi. Tatizo ni kuwa picha hizo hazikuwa fumanizi wala nini bali zilikuwa ni picha zilizopigwa kwa zamu. Wamejipanga matumbo yao huku wakitabasamu mbele ya kamera bila haya wala uoga wowote.
Utamaduni wa kiafrika umeenda wapi jamaa?
Nimepongeza hatua ya BASATA kumfungia Snura video yake ya 'kimajanga' na nawaomba kama wana uwezo wa kuwafungia hawa wasanii wengine wanaochukua advantage ya miili yao ili kudhania watapata umaarufu ingekuwa vyema.
Tatizo hili naliona limeanza kuenea hadi shule za sekondari na hivi karibuni nahofia shule za misingi wanashika mkondo. Kuna blogs nyingi zinazoonyesha wanafunzi nao wakipiga picha za uchi.
Serikali kama inaweza kuingiza mkono wake kwa janga hili naona itakuwa ni bora kwani itaokoa jahazi kutozama.
Kuna ule msemo wa kiswahili unaosema 'samaki mkunje angali bado mbichi.'