BASATA yamfungulia msanii Ney Wa Mitego

BASATA yamfungulia msanii Ney Wa Mitego

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,621
Reaction score
8,411
BASATA imemfungulia Nay wa mitego kuendelea na shughuli za sanaa baada ya kutekeleza maagizo aliyopewa.

Nay wa Mitego atakuwa kwenye uangalizi maalumu wa BASATA ili kuhakikisha anazingatia sheria, kanuni na taratibu sambamba na maadili.

Pamoja na marekebisho mara mbili ya wimbo wa 'pale kati', BASATA bado haijaridhishwa hivyo inaendelea kuufungia wimbo huo.

Nay wa Mitego atakiwa kuufanyia marekebisho kama anauhitaji, vyombo vya habari vyapigwa marufuku kuucheza. Kuhusu Nay wa mitego kupanda jukwaani huku akiwa ktk adhabu, BASATA imesema inafikiria hatua za kuchukua kwa waandaaji wa tamasha.

===============
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Katibu Mtendaji wa BASATA Godfrey Mngereza amesema kuwa wamemfungulia msanii Nay wa Mitego kuendelea na sanaa baada ya kutekeleza maagizo aliyopewa ikiwa pamoja na kuomba msamaha kwa jamii, kukiri kubadilika ila bado wameendelea kuufungia wimbo wake wa 'Pale kati' kwani bado hauna maadili kwa jamii licha ya msanii huyo kuufanyia marekebisho mara mbili.

"Tumemfungulia Msanii Nay wa Mitego kwa kutekeleza maagizo aliyopewa, kujutia na kukiri kubadilika. Wimbo wa 'Pale Kati' bado haukidhi. Pamoja na kuufanyia marekebisho mara mbili wimbo wa Pale Kati bado haukidhi. Tunaendelea kuufungia hadi itakapoelekezwa vinginevyo, tunatoa maelekezo kwa vyombo vya habari kutocheza wimbo wa 'Pale Kati'. Hatua na adhabu za kisheria zitachukuliwa kwa atakayekaidi" Amesema Mngereza

Mbali na hilo msanii Nay wa Mitego ametangaza kuachia wimbo mwingine mpya ambao unaweza kutoka wiki hii.
 
Hivi BASATA na TCRA ni ndugu? Maana wote menoless
 
Back
Top Bottom