BASATA yasajili makumi ya Wasanii Dodoma

BASATA yasajili makumi ya Wasanii Dodoma

mchumihalisi

Member
Joined
Oct 8, 2015
Posts
28
Reaction score
98
Baraza la sanaa Tanzania BASATA limeendelea na uhamasishaji wa Wasanii Kujisajili kwenye mfumo wa Usimamizi Taarifa za Msanii 'Amis' pamoja na kuwasaidia Washiriki kujisajili kwenye Tuzo za Muziki Tanzania (TMA) waliokua na changamoto za Kimtandao.

Akizungumza na Wasanii wa Dodoma Kwanza Afisa Sanaa Mwandamizi wa Basata Agustino Makame amewaambia faida za kujisajili BASATA ni nyingi lakini muhimu zaidi mfumo unasaidia kulinda haki zao za Sanaa kuvamiwa na Watu wengine, Pamoja na kutambulika rasmi na Serikali.

Wasanii walipata nafasi ya kuuliza Maswali na kushauri juu ya tuzo na mfumo wa Basata kwa ujumla ambapo Majibu yote yalijibiwa na Afisa Sanaa Makame papo hapo.

Zoezi la Wasanii kujisajili na kupata elimu ya Sanaa Dodoma limefanyika vizuri ndani ya siku mbili Februari 19 na 20 2022 kwa mafanikio Makubwa kwenye ukumbi wa Dodoma kwanza ulioko
IMG_9547.jpg

Jijini Dodoma.
IMG_9534.jpg

IMG_9521.jpg

IMG_9526.jpg
 
Back
Top Bottom