Based on true story:Jana ilibaki kidogo nife ndege john

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642
Jana mida ya asubuhi hata chai sijanywa nikapita shop nikanunua pombe Kali yenye alcohol 35% nikawa nakunywa mdogomdogo naelekea kazini baadae mida ya saa tano nkatoka kazini nikarudi kijiweni kuendeleza ligi nikanunua kijini (gen) kingine ikumbukwe pombe zangu sii gharama sana buku 2500 tu au 3000 huwa sikweri.kufika mchana si ndio pombe ikapanda nikaanza kujisikia kuchemka nikanunua ubwabwa kwa mama ntilie nikaonja kidogo nikajisikia kichefuchefu ghafla mwili ukachemka ni kinyama.nikaanza kuona dunia inaranda nikaanza kuona mapigo ya moyo yanaenda Kasi ya ajabu pressure ya moyo mpaka nasikia nimelegea.nikajisemea moyoni Leo mjanja nimenaswa Leo nakufa.nikachukua simu yangu Nika uninstall fasta app ya Jf maana sikutaka nikifa wanandugu waje kuona thread nilizokuwa naanzisha.nikafuta na picha za ngono zote nilizokuwa nazo.simu ikabaki clear nikaenda sehemu nikalala hapo nasikia joto la ajabu na jasho usipime.nikapagawa mpaka nikajinyea kidogo nikaona Leo naaga dunia akapita jamaa mmoja nikamwachia wosia Nika mwambia kama nikifa naomba mpigie simu mama angu umwambie nikampa password ya simu nikamwambia nikifa ai restart simu yote.nikamtuma jamaa aniletee maji ya kunywa nilivyokunywa maji nikatulia kidogo kama usingizi ukanipitia dakika tano nikajikuta nimeamka na ile homa ikaisha nikagundua kumbe ilikuwa ni dehydration tu nikapona nikalia kwa Mungu nikamuomba msamaha kuanzia jana sirudii tena kunywa pombe
Moral of the story:kuweni makini sana wanywa pombe na wavuta sigara kwani zinaua sana Jana ndo nimegundua jinsi zinavoua.
 
Jana umegundua jinsi zinavyoua wakati hujafa? Ungekufa kwanza ndio ungejua jinsi zinavyoua.
 
Pole leo inabidi ukashinde sehemu ya kufanyia ibada kulingana na imani yako.
Jana hiyo hiyo niliamua ku download tena app ya Bible nisome upya bibla na kanisani niende nafikiria kujiunga na kwaya ya vijana kanisani kwetu
 
Jana umegundua jinsi zinavyoua wakati hujafa? Ungekufa kwanza ndio ungejua jinsi zinavyoua.
Jana ndege nilinaswa kwenye tundu bovu..Kama ni kufa process nilikuwa 60%..yaani ilibaki kidogo ni shutdown mazima
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…