Kwa hali hii mpira wa kibongo hauta kaa ubadilike na kuwa mafanikio,ni mpira wa majungu na ni mpira wa kufikirika.hakuna mafanikio yoyote katika kila jambo kama halitaoanishwa na mipango ya kimaendeleo na kisha kuwa na dhamira ya kweli ya kuitekeleza mipango hiyo.
siku zote watanzania kwenye soka tunawaza ni jambo la kufundishwa leo na kesho upate ushindi.haya mambo ndo yalipelekea kutokuendelea na Maximo kocha ambae alishaamsha ari ya soka kwa wachezaji na washabiki wa soka.lakini kwa sababu ya kufikirika tukaona hatufai.leo Besena kaharibu nini?au kama kipimo cha kujua soka ni kumfunga yanga tu?
Mambo ya kiswahili siku zote silaha yake ni majungu na matokeo ya majungu huwa ni kutokufanikiwa siku zote.nashukuru timu yangu ilishashuka daraja na nimeridhika kabisa,si nyingine ni PAMBA ya mwanza.
inategemea na malengo na perspective yako, angalia klabu kama chelsea au real madrid wao kocha akiboronga huwa wanafanya nini?au wao nao wamejaa majungu na umbea je na wao ni waswahili?
je, unajua basena wakati anaajiriwa alipewa mkataba wa muda gani?uliza ndio ujibiwe
sisi wapenzi wa simba tunaohudhuria mechi tunaiona timu yetu, timu hii ni nzuri sana katika miaka 3 au 4 iliyopita kwani kila eneo lina wachezaji wazuri, kipa ni mzuri, mabeki, viungo ndio usiseme na washambuliaji hali kadhalika, lakini ijapo kuwa timu ilikuwa inashinda timu haina coordination, ni sawa na man city enzi ya mark hughes au hata sasa kwa mancini, timu ni nzuri lakini kocha wa man city sio bora enough kwa ile timu, hilo ndilo lililopo Simba, kwani timu hii kwa ukamilifu wa wachezaji na angekuwa ni phiri, timu hii isingekuwa inashinda bao 1-0, maana ni kweli simba inaongoza ligi lakini ni juhudi zaidi za wachezaji kkwani wao hawachezi kitimu, sasa mwenye jukumu la kuunganisha timu ni nani kama sio kocha?
basena kwanza naamini hata viongozi wa simba wenyewe wanajua walilamba galasa, hana uzoefu wa kufundisha klabu kubwa huko kwao,yeye alikuwa kocha msaidizi uganda atafundishaje Simba klabu kubwa kuliko yoyote iliyopo kwao Uganda?mimi japokuwa siungi mkono maamuzi ya yeye kutimuliwa sasa lakini nafahamu kabisa Simba hatuna kocha, yule ni mchemfu, kwanza sisi tuna kawaida ya kujaza viungo wengi na kucheza pasi zaidi yeye juzi kapunguza viungo kwa kuwafanya waende winga na kuacha nafasi kati yanga wajitutumue, na ukitaka kujua kakariri hata sub zake kikianza kipindi cha pili tu, ndio anamwingiza haruna moshi kwenye mechi zote karibuni anafanya hivyo, ile na african lyon, ruvu na hii na yanga, sasa hapa ina maana ni wakati wa half time tu ndo anaona boban aingie au wakati upi?
basena bado hana hadhi ya kufundisha simba , na akiendelea si ajabu hata ubingwa tukakosa