Per Diem
JF-Expert Member
- Mar 28, 2018
- 2,189
- 3,724
Kuna nguvu ilitumika sana kwenye suala la mbolea mwaka jana, nyimbo zilitungwa na sifa ziliimbwa kwa waziri bashe kuhusu mbolea ya ruzuku.
Bashe akasema anataka kumuinua mkulima ndio maana anasaidia wakulima wote wapate mbolea ya ruzuku.
Hafla ya mbolea ya ruzuku kwa wakulima ilifanyika mbeya siku ya nanenane na mgeni rasmi alikua raisi samia. Karibu nusu ya mawaziri walihudhuria ile hafla ya ugawaji mbolea ya ruzuku.
Bajeti ikasifiwa kuwa ni ya kihistoria haijawahi kutokea. Sasa leo mwaka wa bajeti umeisha turudi kwenye uhalisia kuhusu hayo yaliyofanyika mwaka jana, tuone ukweli na uongo ulipo.
Lengo ilikuwa ni kusajili wakulima milioni 7, waliofanikiwa kusajiliwa ni wakulima milioni 2, waliofanikiwa kupata mbolea ni wakulima laki 8.
Haya waziri alipaswa kuyasema na sio kuyamezea. lengo ni kuwajuza kama ilivyofanyika wakati wa uzinduzi, huo ndo utakua msema ukweli na utasaidia watu wajue mapungufu yapo wapi na kukusaidia kuyatatua.
Chini ni idadi ya wakulima kila mkoa waliopata mbolea ya ruzuku. Mkoa kama rukwa na katavi ambao unasifika kwa kilimo, waliopata mbolea ni 10,000 tu. Mkoa ambao una wakulima zaidi ya laki 5 (sensa). Hapo tafsiri yake wakulima zaidi ya laki 490,000 hawakupata hiyo mbolea.
Bado tunataka tusubiri mwaka ujao?