Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 577
- 2,595
Ziara ya Rais Samia Suluh Hassan Mkoani Njombe, kijiji cha Mtwango.
Waziri wa Kilimo Mh. Hussein Bashe ametoa uhakika wa upatikanaji wa mbolea kwa bei ya ruzuku hata kwa wakulima ambao hawatakuwa wamesajiliwa baada ya muda huo kufika. Hii inatoa ahueni kwa wakulima waliokuwa na wasiwasi juu ya utaratibu huu mpya wa kujisajili ili kuwa mnufaika wa nafuu ya punguzo ya bei ya mbolea iliyotangazwa na serikali.
Waziri Bashe amewataka wakulima wote, hata wale wasiosajiliwa kufika kwa mawakala watakao orodheshwa hapo baadae ili kupata mbolea kwa bei ya ruzuku kwani serikali itaweka utaratibu wa kuwasajili hapohapo pasipo usumbufu. Katika kuhitimisha hotuba hii fupi, Rais amewaomba viongozi wa serikali kukusanya mapato vizuri kwa ajili ya maslahi mapana ya taifa.