Bashe iga mfano wa Mwigulu. Jitokeze ujibu kashfa ya sukari

Stuka

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
282
Reaction score
906
WAZIRI wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba amejitokeza hadharani kwenye mitandao mbalimbali ya Kijamii kujibu tuhuma za kwamba Serikali imefilisika kama walivyodai baadhi ya watu na akatoa ufafanuzi wa kina wa kila hoja.

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe unakabiliwa na tuhuma mbalimbali kwenye utoaji wa vibali vya sukari kwa zaidi ya miezi miwili sasa kashfa inakulilia, umeona wazalishaji wa sukari wanakulilia, wakulima wa miwa wanakulilia na tuhuma lukuki za rushwa kwenye biashara ya utoaji vibali vya sukari.

Kwanini na wewe usitoke hadharani ukaeleza unayojajua kuhusu kashfa hii kubwa ya sukari inayoendelea kuibuka upya kila siku?

Bashe iga MFANO wa Mwigulu utakuja kunikumbuka, ukimya wako haukusaidii chochote na hicho cheo ni dhamana lolote linaweza kutokea kwako.
 
Hata zakayo na yeye ni bwabwa kifupi asilimia kubwa ya viongozi wa tz hawana upeo na maarifa ya uongozi
 
Tena ajitokeze JF na X tumsute mpaka akimbie jukwaa kama walivomfanyia mpina
 
yani mtu anamiliki mabilioni ajitokeze kujibu maswali yanyie kenge?🤣🤣🤣🤣

mwigulu mwenyewe anawainjoitu kujisumbua kuwajibu
Atuenjoy asituenjoy Mungu ANAMUONA hata kama hana hofu naye.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…