Bashe jiuzulu kulinda heshima yako; wanaokuhujumu wanatumwa na mahasimu wako

Bashe jiuzulu kulinda heshima yako; wanaokuhujumu wanatumwa na mahasimu wako

Resilience

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2023
Posts
1,096
Reaction score
4,948
Njombe yametokea matukio mawili ya kujumu wakulima katika eneo la Mbolea. Wasambazaji wa Mbolea badala ya kupeleka Mbolea wanasambaza maelfu ya magunia ya mchanga na vitu vinavyofanana na mchanga.

Polisi wanaambiwa wachunguze wanasema sample zinasubiri majibu maana yake pamoja na Waziri kuambiwa huu mchanga, mwenye ghala kukiri kwamba magunia yamejaa mchanga lakini polisi wao wanasema hapana wanasubiri uchunguzi wa maabara.

NI kweli kabisa kwamba uchunguzi wa kitaalamu unahitajika lakini je, kuchunguza mchanga nakusema siyo mbolewa maabara zetu zinatumia muda gani?

Wakati huo katika kuzimaliza kesi hizi wanaotakiwa kukamatwa wanasema wahusika wametoroka na wanadai kwamba wameripoti polisi means wanajua mchezo mzima.

Lakini pia Mbolea inatoka Arusha Minjingu means kuna nyaraka za mauzoano, je ukaguzi WA nyaraka baina ya hawa watu na kampuni inayouza haikuwepo? Lakini pia TBS wanakuwa wapi wakati haya mambo yanafanyika?

Maafisa kilimo wanashindwaje kutofautisha mchangaa na Mbolea?

Haya yote yanaleta maswali kwamba Mhe. Waziri upo kwenye exit nikusihi jiandae. Hawa watu wanaoweza kufanya hii hujuma maanayake kwenye tenda walibebwa na niwatoto WA wakubwa hivyo ukitaka kuwakamata lazima wakubwa wakukamate wewe.

Hakuna namna mnaweza mkapeana pesa za Mbolea Kwa kusajili makampuni ya wanasiasa mtegemee integrity; hii deal imeshikwa na vigogo jiandaeni.

Pesa ya Mbolea lazima mmezigawa Kwa watu wasio na integrity na untachable, la sivyo tuoni publically makampuni yaliyopewa tenda na wamiliki wake, wasimamizi wake na wasambazaji wanaofanya kazi.

Mbolea ni jipu jingine, wakulima amkeni.
 
Mbolea zimekamatwa ndani ya ghala sasa hapo una uhakika gani kama sio mchezo unaofanywa hapo hapo kwenye ghala na wasimamizi wa ghala pasipo kuhusika kiwanda?
 
Back
Top Bottom