BASHE : SERIKALI ITAWALINDA WAKULIMA KWA GHARAMA ZOTE
Tanganyika, Katavi.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe ameweka wazi msimamo wa serikali juu ya kuwalinda wakulima nchini kufuatia muingiliano wa kisekta wa mara kwa mara ambao husababisha wakulima kubeba mzigo mkubwa zaidi wa gharama za uzalishaji.
Naibu Waziri Bashe ameyasema hayo kufuatia taarifa ya wilaya ya Tanganyika juu ya Mamlaka ya Wanayapori nchini (TAWA) kuweka alama za mipaka Kwenye maeneo ya misitu ya Tongwe ambayo hapo awali maeneo hayo yalikuwa yamekwishagawiwa kwa wakulima wadogo na wawekezaji wa kilimo huku maamuzi ya kurasimisha maeneo hayo kwa TAWA yakiwa yamefanywa pasipo vikao kushirikisha wadau wa pande zote pamoja na halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika.
Naibu Waziri Bashe amesema “Haiwezekani TAWA kutumia vibaya Mamlaka waliyinayo, waliwezaje kuingia na kuweka alama bila kushirikisha uongozi wa vijiji, kata au wilaya? Vitendo vya namna ni kumgombanisha Rais pamoja na wananchi ambao wamekwishakupatiwa mashamba Kwa ajili uwekezaji kwenye sekta ya kilimo”
Bashe ameongeza ya kuwa “Masuala ya namna hii yanahitaji mashauriano zaidi baina ya Wizara ya Kilimo na Wizara ya Mali Asili na Utalii ili kuhakikisha tunalinda maslahi ya pande zote bila kuwapa mzigo wananchi ambao sehemu kubwa ya maisha yao wamekuwa wakitegemea kilimo”
Aidha Mhe. Bashe ameongeza ya kuwa “Kama taifa tumekuwa na mipango ya kuwa na maeneo ya viwanda, maeneo ya wanyamapori, na maeneo ya usafirishaji lakini hakuna Mpango wa kutenga maeneo kwa ajili ya uwekezaji wa kilimo. Kwa dunia ya sasa ili kila jambo lifanikiwe lazima liwekewe utararibu rasmi ambao utatoa mwanga Kwa wawekezaji na taifa Kwa ujumla”
Katika kuhitimisha ziara yake kwenye wilaya hiyo ya Tanganyika, Mhe. Bashe ameitaka kutenga eneo la ekari 1,000 kwa ajili ya Kilimo cha mbegu kufuatia mkoa wa Katavi kuwa kitovu cha uzalishaji wa mbegu ambapo watafiti wa Taasisi za TARI na ASA wamepewa jukumu la kufanikisha zoezi hilo Kwa haraka ili kufikia malengo ya kitaifa kwenye uzalishaji na upatikanaji wa mbegu nchini.
#SamiaKaziIendele
#KilimoTanzania