Bashe tuletee majina ya wakulima waliouza mchele Tsh 3,500 kwa kilo tukupongeze kwa kumlinda mkulima

Bashe tuletee majina ya wakulima waliouza mchele Tsh 3,500 kwa kilo tukupongeze kwa kumlinda mkulima

saidoo25

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2022
Posts
624
Reaction score
1,456
Nimekuwa nikimsikia Bashe akijipata kuwa anawatetea wakulima wauze wanavyotaka kwani kilimo ni biashara.

Kwa heshima na unyenyekevu mkubwa naomba unitajie angalau majina ya wakulima 10 wwaliofanikiwa kuuza mchele sh 3,500 kwa kilo ili tuwafahamu twende tukajifunze kwao walivyotajirika kwa kilimo.
 
Tuna waziri kiazi si wengine ndugu zetu wakulima,yaani hapo anapiga kelele ila wakulima washauza chakula tokea mwaka jana.

Sasa hivi wenye hizo bidhaa ni walanguzi, eti anadai awamu yake wakulima ndio wanapiga pesa tatizo lake hana hata data,wakulima hali zao zipo vilevile wanaopiga pesa ni walanguzi
 
Kwani huu mchele wa mbeya tunanunua kutoka nje? Si kutoka kwa wakulima wa ndani?
 
Ngoja kwanza njaa iwatie adabu ili siku nyingine wajifunze kuweka akiba ya chakula.

Hivi mtu unalima mahindi unavuna magunia 50 unauza yote bila kuacha angalau magunia 6 ya akiba kwa ajili ya chakula hali yakuwa unajua kuwa una familia.
Na mbaya zaidi huwa wakiuza hayo mazao wengi wao huwa jawafanyi mambo ya maana zaidi ya kunywa pombe na kuhonga malaya walio toka mjini huku wakiacha familia zao zikiteseka.

Mm sikuwa muumini ya sera za kibabe za jiwe lakini kuna sehemu nilikuwa namkubali maana waafrika tumekuwa masikini kwa sababu ya kuendekaza kubembelezana.
 
Tuna waziri kiazi si wengine ndugu zetu wakulima,yaani hapo anapiga kelele ila wakulima washauza chakula tokea mwaka jana.

Sasa hivi wenye hizo bidhaa ni walanguzi, eti anadai awamu yake wakulima ndio wanapiga pesa tatizo lake hana hata data,wakulime hali zao zipo vilevile wanaopiga pesa walanguzi
Hata MO ni mkulima mjue infact 90% ya watanznaia ni wakulima; sasa bahati mbaya hili group kubwa lipo katika nodes mbalimbali za supply chain maana nikisema "value chain" nitakuwa nime exaggerate maana hakuna value addition ya maana hapa nchini kwakua hakuna viwanda vya maana zaidi ya hivi vyaku kusaga unga na kukoboa mchele...Then waziri anashindwa kuelewa hii diversity ya wakulima anatumia simplicity kusema eti wakulima wanafaidika, this is a tragedy, somebody has to help these people na ni watendaji ndiyo wanampotosha bila kujali welfare ya watanzania...
 
Nimekuwa nikimsikia Bashe akijipata kuwa anawatetea wakulima wauze wanavyotaka kwani kilimo ni biashara.

Kwa heshima na unyenyekevu mkubwa naomba unitajie angalau majina ya wakulima 10 wwaliofanikiwa kuuza mchele sh 3,500 kwa kilo ili tuwafahamu twende tukajifunze kwao walivyotajirika kwa kilimo.
wafanya biashara ndo wanauza kwa Bei hiyo na zaidi, wakulima watakuwa wanauza 1000-1800/ haiwezi kuzidi

Nnachoona wanachanganya mkulima na mfanyabiasha

ama mkulima na mkulima biasha (kilimo biashara)

Watanzania wengi ambao ni wakulima, ni wakulima perse na siyo wafanya biashara! huuza mazao yao kwasababu wanahitaji fedha wakati huo na hakuna mbadala!
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Back
Top Bottom