Bashiri mtu/watu kwa mujibu wa thread zake jinsi alivyo.

Shida na raha

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2014
Posts
3,773
Reaction score
3,471
Habari za majukumu wakubwa na wadogo.
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu.

* Ushimen: ni mtu wa kawaida hapendi kujaa hasira sana.
* Mshana Jr: huyu nilishakunywa nae soda sina haja ya kubashiri.
* Bujibuji: hapendi kucheka cheka lakini hata hivyo hana hasira za karibu mpaka umkere.
* Daby: hapendi kukera ila ukimkera uvumilivu hana anaweza kukuvuruga mbavu.
* Kasie: huyu mama ni mzee lakini anapenda sifa sifa ukimsifia umemdaka.
Gentamycine: hana shida na mtu anapenda kuficha hasira zake lakini zenyewe zinafika kipindi zinamzidia.
Shunie: ni mcheshi mcheshi kidogo sio sana na pia hana tabia ya kuzira ovyo ila anaweza kukupeleka kuzimu ukipitiliza.
Emmyta: Ana wivu sana sema anaficha kidogo ila anaweza kukuuwa kwa wivu.

Wangu ni hao kama unawajua wengine ongezea...
 
Kiranga= mtata na mbishi kupindukia japokuwa ni muelewa wa mambo mengi.

Faiza Foxy=mbishi na mgomvi mgomvi fulani hivi ila ana uelewa wa hali ya juu.

Mshana jnr = huyu ni mtaalam wa ku-google vitu na kuvichanganua kwa faida ya wengi pia ana busara.

Wapo wengi ambao kwa uandishi wao utawajua tabia zao kirahisi tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…