BASHUNGWA AFIKA SOMANGA KUKAGUA ATHARI ZA MVUA BARABARA YA DAR - LINDI
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amefika katika eneo la Somanga - Mtama mkoani Lindi kuungana na Timu ya Watalaamu wa Wakala ya Barabara (TANROADS) na Makandarasi kuratibu kazi ya kurejesha mawasiliano ya Barabara ya Lindi – Dar- es Salaam ambayo imeharibiwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha zilizobatana na kimbunga Hidaya, leo tatehe 05 Mei 2024