Bashungwa Aitaka Idara ya Uhamiaji Kutoa Huduma Nzuri kwa Wageni, Kuchochea Utalii

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa ameitaka Idara ya Uhamiaji kuendelea kuwa mstari wa mbele kuchochea na kukuza utalii nchini kwa kutoa huduma bora na nzuri kwa wageni wanaokuja nchini kwa shughuli mbalimbali.

Ameeleza hayo Januari 10, 2025 Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba, Zanzibar wakati alipotembelea ujenzi wa Bandari ya Shumba Mjini ambapo awali ilikuwa bandari bubu iliyotumiwa wananchi wageni kwenda bandari ya Mombasa, Kenya

“Tuendelee kujipanga na kuhakikisha tunakuwa na huduma nzuri ya kuwapokea wageni ili wakija wakafanya utalii watachangia utalii lakini wakipata huduma nzuri, wao pia wanaenda kuwa wasemaji wetu wazuri huko wanakotoka”

Bashungwa amesisitiza kuwa Idara ya Uhamiaji ikitoa huduma nzuri kwa wageni na watalii wanaaoingia nchini, hali hiyo itaendelea kuitangaza nchini yetu kwa Mataifa wanapotoka.

Aidha, Bashungwa ametoa pongezi kwa Mhe. Dkt Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa kazi kubwa ya maendeleo anayoendelea kuifanya kwa kuifungua Zanzibar kiuchumi.

Kadhalika, Bashungwa ameeleza kukamilika kwa ujenzi wa Bandari ya Shumba Mjini itasaidia kukuza uchumi na kuwawezesha Wananchi na wageni kuingia na kutoka Zanzibar.

Awali, Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Hassan Ali Hassan ameeleza kabla ya kuanza ujenzi wa Bandari hiyo wananchi wa Kisiwa cha Pemba walitumia eneo hilo kwenda Mombasa Kenya bila utaratibu ambapo kukamilika kwa bandari hiyo itawezesha kusafiri kufuata sheria na taratibu.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2025-01-11 at 09.02.38.jpeg
    773.7 KB · Views: 3
Tushachoka hizi ngonjera

Atakuja waziri mwingine atarudia maneno hayo hayo

Kupata tu passport bila kuhonga hupati kwa wakati

Kwenye NIDA mambo ni hayo hayo miaka na miaka ,

Walau kipindi cha JPM mambo yalianza kubadilika

Sasa hivi kwenye maofisi ya serikali ni ovyo ,
 
Mnachekesha sana,unadhani kwa nini watu wengi wanahangaika watoto wao waende uhamiaji.
 
Na wanafanya kazi hapa,wahindi kibao,pita kwenye makampuni makubwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…