Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
“Namjua Dkt. Msonde nimefanya nae kazi nikiwa TAMISEMI, ni mzee wa kunyooka na mwenye kufuata utaratibu, kwa hiyo naomba mnipe miezi mitatu nimkabidhi Taasisi hizi Naibu Katibu Mkuu ili kufanya mabadiliko katika taasisi hizi”, amesema Bashungwa.
Waziri Bashungwa ameeleza kuwa Dkt. Msonde atamsaidia Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Balozi Mhandisi Aisha Amour kuongeza ufanisi wa utendaji kazi na kufanya maboresho katika Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo.
Soma Pia:
~ Waziri wa Ujenzi awaondoa Watendaji wa TEMESA Kivukoni Dar kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao
~ Huduma za Uvushaji wa MV Kigamboni zasitishwa
Aidha, Bashungwa ametumia fursa hiyo kumshukuru Mhe. Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa uteuzi wa Niabu Katibu Mkuu huyo pamoja na kumpongeza Naibu Katibu Mkuu aliyepita Bw. Ludovick Nduhiye ambaye kwa sasa ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi kwa utendaji mzuri wakati akiwa Wizara ya Ujenzi.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumumu ya Bunge ya Miundombinu, Mheshimiwa Selemani Kakoso amesisitiza umuhimu wa Wizara ya Ujenzi kusimamia TEMESA na TBA ziweze kukusanya madeni wanayodai kwa Taasisi za Serikali ili kuisaidia Wakala hizo kujiendesha pamoja na kutoa gawio kwa Serikali.