Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Wakuu,
Hadi nimecheka
oyaa napita hapo dk 0 kwenye gari aina fulani, fanya kunipiga mkono

.
=====
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa akizungumza na askari wa usalama barabara katika eneo la Magugu wilayani Babati mkoani Manyara wakati akiwa safari mara baada ya kushudia askari hao wakitekeleza majukumu yao kwa weledi na uadilifu, leo tarehe 04 Januari 2024
Bashungwa akiwa kwenye gari lenye namba za usajili binafsi, direva wake alisimamishwa na kuanza kukaguliwa wakati Waziri huyo akiwa ndani ya gari ambapo baada ya kuruhusiwa, aliwaita askari hapo na kuwapongeza kwa kutekeleza majukumu yao kwa weledi.
Kwa vimbwanga na vituko vingine kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ruka hapa: Uzi Maalum wa Vibweka na Hekaheka za wanasiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
“Nimeshamwambia IGP, barabarani sio machinjio ya watu, kwahiyo mnaposimamia majukumu yenu kwa weledi tunafurahi. Hakuna ambaye yupo juu ya sheria, mtu yeyote anayetumia chombo cha moto anapokuwa barabarani lazima azingatie sheria za usalama barabarani” Bashungwa akizungumza na Askari .
Aidha, Bashungwa amempongeza Kamishna Mwandamizi wa Jeshi la Polisi (SACP) William Mkonda, Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani, Maafisa na Askari wote wa Usalama Barabarani na kuwataka kuendelea kushughulika na madereva wazembe.

.=====