Hadi nimecheka oyaa napita hapo dk 0 kwenye gari aina fulani, fanya kunipiga mkono.
=====
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa akizungumza na askari wa usalama barabara katika eneo la Magugu wilayani Babati mkoani Manyara wakati akiwa safari mara baada ya kushudia askari hao wakitekeleza majukumu yao kwa weledi na uadilifu, leo tarehe 04 Januari 2024
Bashungwa akiwa kwenye gari lenye namba za usajili binafsi, direva wake alisimamishwa na kuanza kukaguliwa wakati Waziri huyo akiwa ndani ya gari ambapo baada ya kuruhusiwa, aliwaita askari hapo na kuwapongeza kwa kutekeleza majukumu yao kwa weledi.
“Nimeshamwambia IGP, barabarani sio machinjio ya watu, kwahiyo mnaposimamia majukumu yenu kwa weledi tunafurahi. Hakuna ambaye yupo juu ya sheria, mtu yeyote anayetumia chombo cha moto anapokuwa barabarani lazima azingatie sheria za usalama barabarani” Bashungwa akizungumza na Askari .
Aidha, Bashungwa amempongeza Kamishna Mwandamizi wa Jeshi la Polisi (SACP) William Mkonda, Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani, Maafisa na Askari wote wa Usalama Barabarani na kuwataka kuendelea kushughulika na madereva wazembe.

Askari wa barabarani ni kero tu. Binafsi sijawahi kuamini kama wana msaada kivile kwenye kupunguza hizo ajali za barabarani! Maana muda mwingi wako busy kukusanya hela tu za rushwa, na pia zile za hesabu kwa ajili ya mapato ya serikali ya CCM.
Kwakweli huyu jamaa yupo vizuri, juzi kapita kazini kwangu hata hakutaka kujulikana kama yupo.
Nilikuja kushangaa msaidizi wake anakuja kuniomba password ya wi-fi kwamba mh anataka kufanya issue kwenye mfumo.
Kwenda ndo namkuta kwenye gari yupo busy na pc yake.
Mbona Ile road Haina traffic wa kutosha ukitoka kisongo hapo mpaka Minjingu utakutana nao wachache labda kipande cha minjingu magugu hadi babati mjini ndo kipengele