Bashungwa atoa angalizo kwa Maafisa wa Uhamiaji wanaoingiza Wahamiaji Haramu Nchini

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
WhatsApp Image 2025-03-04 at 17.15.56_a88b0cbd.jpg
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa amewataka Maafisa na Askari wa Idara ya Uhamiaji kutekeleza majukumu yao kwa uzalendo, uadilifu na kujiepusha na vitendo vya rushwa ambavyo vinaweza kupelekea uingiaji wa wahamiaji haramu nchini.

Bashungwa ameeleza hayo, leo Machi 04, 2025 katika kikao kazi na Maafisa na Askari wa Jeshi la Polisi, Magereza, Zimamoto na Uokoaji, Idara ya Uhamiaji na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) katika wilaya ya Karagwe, Mkoa wa Kagera.

“Wizara itawasimamia kikamilifu maafisa Uhamiaji katika kutekeleza majukumu yao. Wale ambao watakosa uzalendo na uadilifu, na kuwa sehemu ya chanzo cha kuchochea uingiaji wa wahamiaji haramu kwa lengo la kujipatia fedha au rushwa, tutawachukulia hatua kali za kisheria na za kiutumishi,” amesema Bashungwa.
WhatsApp Image 2025-03-04 at 17.15.58_af988780.jpg

WhatsApp Image 2025-03-04 at 17.15.59_54c6ce04.jpg

WhatsApp Image 2025-03-04 at 17.15.59_b0876860.jpg
Bashungwa amesema Mkoa wa Kagera ni miongoni mwa Mikoa ambayo iko mipakani, ambao umekuwa ukikumbwa na changamoto ya baadhi ya wageni kutoka nchi jirani kuingia kinyume na taratibu kutokana na ukubwa wa mpaka.

Aidha, Bashungwa ametoa wito kwa viongozi wa vijiji na kata, kuwa mstari wa mbele kusimamia ili kukomesha suala la uhamiaji haramu bila kumuonea au kumkomoa mtu kwa kutoa taarifa kwa maafisa wa uhamiaji pale zinapohitajika.

Amewahimiza wananchi kutoa taarifa pindi watakapoona Askari wa Idara ya Uhamiaji anafanya vitendo ambavyo ni kinyume na maadili, sheria na taaluma yake ili kuhakikisha kila mgeni anayeingia nchini anaingia kwa mujibu wa sheria.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Julius Laiser ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuviwezesha Vyombo vya Ulinzi na Usalama ikiwemo Idara ya Uhamiaji Wilaya ya Karagwe kupewa gari jipya.
WhatsApp Image 2025-03-04 at 17.16.01_f040004f.jpg
 
BASHUNGWA ATOA ANGALIZO MAAFISA UHAMIAJI, UINGIAJI WA WAHAMIAJI HARAMU.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa amewataka Maafisa na Askari wa Idara ya Uhamiaji kutekeleza majukumu yao kwa uzalendo, uadilifu na kujiepusha na vitendo vya rushwa ambavyo vinaweza kupelekea uingiaji wa wahamiaji haramu nchini.

Bashungwa ameeleza hayo, leo Machi 04, 2025 katika kikao kazi na Maafisa na Askari wa Jeshi la Polisi, Magereza, Zimamoto na Uokoaji, Idara ya Uhamiaji na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) katika wilaya ya Karagwe, Mkoa wa Kagera.

“Wizara itawasimamia kikamilifu maafisa Uhamiaji katika kutekeleza majukumu yao. Wale ambao watakosa uzalendo na uadilifu, na kuwa sehemu ya chanzo cha kuchochea uingiaji wa wahamiaji haramu kwa lengo la kujipatia fedha au rushwa, tutawachukulia hatua kali za kisheria na za kiutumishi” amesema Bashungwa

Bashungwa amesema Mkoa wa Kagera ni miongoni mwa Mikoa ambayo iko mipakani, ambao umekuwa ukikumbwa na changamoto ya baadhi ya wageni kutoka nchi jirani kuingia kinyume na taratibu kutokana na ukubwa wa mpaka.

Aidha, Bashungwa ametoa wito kwa viongozi wa vijiji na kata, kuwa mstari wa mbele kusimamia ili kukomesha suala la uhamiaji haramu bila kumuonea au kumkomoa mtu kwa kutoa taarifa kwa maafisa wa uhamiaji pale zinapohitajika.

Amewahimiza wananchi kutoa taarifa pindi watakapoona Askari wa Idara ya Uhamiaji anafanya vitendo ambavyo ni kinyume na maadili, sheria na taaluma yake ili kuhakikisha kila mgeni anayeingia nchini anaingia kwa mujibu wa sheria.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Julius Laiser ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuviwezesha Vyombo vya Ulinzi na Usalama ikiwemo Idara ya Uhamiaji Wilaya ya Karagwe kupewa gari jipya.
 
Attachments

  • GlNFvBnXcAAh9QC.jpg
    GlNFvBnXcAAh9QC.jpg
    96.6 KB · Views: 1
  • GlNFvBoXMAAWTUn.jpg
    GlNFvBoXMAAWTUn.jpg
    92.1 KB · Views: 1
  • GlNFvB5XwAA8gEa.jpg
    GlNFvB5XwAA8gEa.jpg
    118.6 KB · Views: 1
  • GlNFvBmWcAAE6cZ.jpg
    GlNFvBmWcAAE6cZ.jpg
    102.9 KB · Views: 1
Hivi hilo ni la kutoa angalizo? Au kilikuwa ni kitendo cha kuwabaini, kuwafukuza kazi kisha hatua za kisheria kuchukuliwa dhidi yao.
 
Waanze na yeye kwanza. Kabla ya hao wengine.
 
Back
Top Bottom