Mwanza: Bashungwa atembelea shule walipotekwa watoto, atoa onyo kwa wahalifu

Mwanza: Bashungwa atembelea shule walipotekwa watoto, atoa onyo kwa wahalifu

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa ametoa onyo kwa wahalifu baada ya jeshi la polisi kufanikiwa kuwapata watoto wawili waliotekwa Februari pili 2025 jijini Mwanza na kupatikana Februari saba 2025 wakiwa salama.

Soma Pia:

“Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Vyombo vya Ulinzi na Usalama liko imara kitaaluma na lina vifaa vya kisasa na vingine havionekani hivyo msifanye mchezo na weledi na utayari wa jeshi hili na niwaonye wahalifu kuwa popote mlipo tutawafikia tena bila kelele yoyote” amesema Bashungwa.
 

BASHUNGWA APONGEZA POLISI KUPATIKANA WANAFUNZI WALIOTEKWA MWANZA.

“Wahalifu msijaribu uwezo wa Polisi, tutawafikia popote”

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa amelipongeza Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Wazazi na Wananchi kwa kufanikisha Operesheni ya msako mkali na kuwapata Wanafunzi wawili wa Shule ya Msingi Blessing Medium iliyopo Mwanza waliotekwa na kupatikana wakiwa salama.

Aidha, Bashungwa ametoa onyo kali kwa watu wote wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu na uvunjifu wa amani na usalama na kueleza kuwa Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Vyombo vya Usalama limejipanga na lina uwezo na weledi wa kukomesha na kupambana na vitendo vyote vya kiuhalifu.

Bashungwa amesema hayo leo tarehe 11 Februari 2025 mkoani Mwanza mara baada ya kufika katika Shule ya Msingi Blessing Medium kuzungumza na Walimu na Wazazi pamoja na Askari na Maafisa waliofanikisha zoezi la kupatika kwa Wanafunzi waliotekwa tarehe 05/02/2025 na kupatikana tarehe 07/02/2025 wakiwa salama.

“Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Vyombo vya Ulinzi na Usalama, liko imara kitaaluma na lina vifaa vya kisasa na vingine havionekani na ndio maana linapokuja suala lolote linakuwa lipo imara, msifanye mchezo na weledi na utayari wa Jeshi la Polisi, mhalifu popote ulipo tuna uwezo wa kukufikia, tena bila kelele yoyote” amesema Bashungwa.

Kadhalika, Bashungwa ametoa wito kwa Wamiliki wa Shule kuanza utaratibu wa kufunga Kamera kwenye Mabasi na mazingira ya shule ili kuongeza ufuatiliaji na kuimarisha usalama wa wanafunzi kuanzia wanapotoka nyumbani hadi wanapokuwa katika mazingira ya shuleni.

Vile vile, Bashungwa amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Camillus Wambura kupitia upya utaratibu wa kusajili kampuni binafsi za ulinzi pamoja kufuatilia mwenendo na weledi wao katika utendaji kazi.

Kwa Upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, DCP Wilbrod Muitafungwa amesema kuwa tukio la Utekaji wa Wanafunzi wawili lilitokea tarehe 05/02/2025 ambapo Jeshi la Polisi lilitimiza wajibu wake kwa kudhibiti uhalifu na kufanikiwa kuwapata Wanafunzi wakiwa salama.

Naye, Mzazi wa mmoja wa Mwanafunzi, Anumie Mtweve ameishukuru Serikali kupitia Jeshi la Polisi kwa kuonesha ushirikiano mkubwa kwa wazazi na uongozi wa shule na kuhakikisha watoto wao wanapatikana wakiwa salama na bila shida yoyote.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2025-02-11 at 19.06.02.jpeg
    WhatsApp Image 2025-02-11 at 19.06.02.jpeg
    338.2 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2025-02-11 at 19.06.04.jpeg
    WhatsApp Image 2025-02-11 at 19.06.04.jpeg
    554.2 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2025-02-11 at 19.06.05.jpeg
    WhatsApp Image 2025-02-11 at 19.06.05.jpeg
    710.7 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2025-02-11 at 19.06.06.jpeg
    WhatsApp Image 2025-02-11 at 19.06.06.jpeg
    336.8 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2025-02-11 at 19.06.07.jpeg
    WhatsApp Image 2025-02-11 at 19.06.07.jpeg
    417.1 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2025-02-11 at 19.06.08.jpeg
    WhatsApp Image 2025-02-11 at 19.06.08.jpeg
    597.4 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2025-02-11 at 19.06.09.jpeg
    WhatsApp Image 2025-02-11 at 19.06.09.jpeg
    463.1 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2025-02-11 at 19.06.10.jpeg
    WhatsApp Image 2025-02-11 at 19.06.10.jpeg
    725.9 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2025-02-11 at 19.06.11.jpeg
    WhatsApp Image 2025-02-11 at 19.06.11.jpeg
    422.9 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2025-02-11 at 19.06.12.jpeg
    WhatsApp Image 2025-02-11 at 19.06.12.jpeg
    570 KB · Views: 1
Wale watoto wametekwa na watekaji wameuawa.

Hili nadhani ndio Mdude Nyagali alikuwa ana comment, anasema wale watekaji wawili walikuwa na mapanga tu,Polisi imeshindwa vipi kuwakamata?

Halafu karibu kila mtu pale alikuwa anampinga Mdude.

Yule jamaa mmoja anasema,"Mi hapa niko Marekani,mhalifu akiwa na wembe tu,Polisi inakuja na SWAT team."
Lakini hii incident inafanana na Ile incident iliyotokea Arusha five or ten years ago.

Huyu mtekaji alikuwa in police custody,usiku anaenda kuwaonyesha Polisi mahali ilipokuwa maiti ya mtoto, halafu yule akauawa na Polisi " kwa sababu alitaka kutoroka".

Sasa mtu kateka mtoto,labda katumwa na mteja,halafu mhalifu anauawa.

Inasikitisha,to say the least.

Kwa sababu wale wahalifu wangeweza kusaidia katika uchunguzi.
 
Back
Top Bottom