Bashungwa: Mwananchi Kupata Kitambulisho cha NIDA Ndani ya Siku 14

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

BASHUNGWA: MWANANCHI KUPATA KITAMBULISHO CHA NIDA NDANI YA SIKU 14

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa ameeleza mkakati wa Serikali ni kuhakikisha Mwananchi anapata Kitambulisho cha Taifa ndani ya siku 14 mara baada ya kukamilisha usajili katika Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

Ameeleza hayo, tarehe 28 Februari 2025 katika hafla ya Jubilei ya miaka 25 ya huduma ya Kolping Hotel, Bukoba Kagera ambapo alitumia nafasi hiyo kueleza mikakati ya Serikali katika kuboresha utoaji wa huduma za NIDA kwa wananchi.

“Mkakati uliokuwepo kwa sasa, mwananchi atakapojisajili ndani ya siku 7 atapokea namba yake ya NIDA (NIN) katika namba ya simu aliyoijaza kwenye fomu na baada ya siku 14, atapokea ujumbe mwingine wa kumtaarifu kufuata kitambulisho chake katika ofisi za NIDA” amesisitiza Bashungwa

Bashungwa amewaagiza viongozi wa NIDA ngazi za Wilaya na Mikoa kutoa elimu kwa Wananchi juu ya mpango mpya wa utoaji huduma ambao umelenga kuondoa kero zote zilizokuwa zinalalamikiwa na wananchi kuhusu usajili, uzalilshaji na
usambazaji wa vitambulisho hivyo.

Aidha, Bashungwa ameielekeza NIDA na Idara ya Uhamiaji kukaa pamoja katika kila ofisi za wilaya, ili kuhakikisha huduma za usajili na utambuzi zinawafikia
wananchi bila usumbufu.

Ametoa rai kwa wananchi wenye changamoto ya kukosa namba na kitambulisho, kujitokeza wakati NIDA na Idara ya Uhamiaji wanapofanya zoezi la uhakiki au usajili katika maeneo yao ili kupata huduma na kutatua changamoto hizo.

Katika Mkoa Kagera, Bashungwa amemuagia Afisa Msajili NIDA kuweka kambi wilaya zote ili kuwasajili wananchi ambao wametimiza miaka 18, ambapo zoezi hilo litaanza tarehe 10 Machi 2025 katika Wilaya ya Kyerwa.

Bashungwa amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutenga fedha kwa ajili ya kuwasajili wananchi 269,177 katika Mkoa wa Kagera ambao wametimiza miaka 18 ambao awali waliokosa nafasi ya kujisajili.
 
Attachments

  • Gk842XoXoAAOrSt.jpg
    Gk842XoXoAAOrSt.jpg
    354.9 KB · Views: 2
  • Gk842XpXsAAXYF1.jpg
    Gk842XpXsAAXYF1.jpg
    410.3 KB · Views: 2
  • Gk842XnXgAAiNpR.jpg
    Gk842XnXgAAiNpR.jpg
    720.9 KB · Views: 2
  • Gk842XqXwAAZu6H.jpg
    Gk842XqXwAAZu6H.jpg
    352.1 KB · Views: 2
NIDA mmesitisha matumizi ya namba za kitambulisho vya wananchi ambao hawakufika kwa wakati mliowapa wa mwezi mmoja kutokana na umbali mmefanya sio vema. mgetoa notisi ya miezi angalau mitatu. Mnajua kabisa namba hizo hutumika kwa matumizi ya shughuli mbalimbali ila mmezifungia bure namba za wananchi wapo hai na vitambulisho hivyo watachukua hata kama vipo mbali
 
BASHUNGWA: MWANANCHI KUPATA KITAMBULISHO CHA NIDA NDANI YA SIKU 14

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa ameeleza mkakati wa Serikali ni kuhakikisha Mwananchi anapata Kitambulisho cha Taifa ndani ya siku 14 mara baada ya kukamilisha usajili katika Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

Ameeleza hayo, tarehe 28 Februari 2025 katika hafla ya Jubilei ya miaka 25 ya huduma ya Kolping Hotel, Bukoba Kagera ambapo alitumia nafasi hiyo kueleza mikakati ya Serikali katika kuboresha utoaji wa huduma za NIDA kwa wananchi.

“Mkakati uliokuwepo kwa sasa, mwananchi atakapojisajili ndani ya siku 7 atapokea namba yake ya NIDA (NIN) katika namba ya simu aliyoijaza kwenye fomu na baada ya siku 14, atapokea ujumbe mwingine wa kumtaarifu kufuata kitambulisho chake katika ofisi za NIDA” amesisitiza Bashungwa

Bashungwa amewaagiza viongozi wa NIDA ngazi za Wilaya na Mikoa kutoa elimu kwa Wananchi juu ya mpango mpya wa utoaji huduma ambao umelenga kuondoa kero zote zilizokuwa zinalalamikiwa na wananchi kuhusu usajili, uzalilshaji na
usambazaji wa vitambulisho hivyo.

Aidha, Bashungwa ameielekeza NIDA na Idara ya Uhamiaji kukaa pamoja katika kila ofisi za wilaya, ili kuhakikisha huduma za usajili na utambuzi zinawafikia
wananchi bila usumbufu.

Ametoa rai kwa wananchi wenye changamoto ya kukosa namba na kitambulisho, kujitokeza wakati NIDA na Idara ya Uhamiaji wanapofanya zoezi la uhakiki au usajili katika maeneo yao ili kupata huduma na kutatua changamoto hizo.

Katika Mkoa Kagera, Bashungwa amemuagia Afisa Msajili NIDA kuweka kambi wilaya zote ili kuwasajili wananchi ambao wametimiza miaka 18, ambapo zoezi hilo litaanza tarehe 10 Machi 2025 katika Wilaya ya Kyerwa.

Bashungwa amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutenga fedha kwa ajili ya kuwasajili wananchi 269,177 katika Mkoa wa Kagera ambao wametimiza miaka 18 ambao awali waliokosa nafasi ya kujisajili.
sound to hizo!
 
NIDA mmesitisha matumizi ya namba za kitambulisho vya wananchi ambao hawakufika kwa wakati mliowapa wa mwezi mmoja kutokana na umbali mmefanya sio vema. mgetoa notisi ya miezi angalau mitatu. Mnajua kabisa namba hizo hutumika kwa matumizi ya shughuli mbalimbali ila mmezifungia bure namba za wananchi wapo hai na vitambulisho hivyo watachukua hata kama vipo mbali
utaratibu uliwekwa hata kwa asiekua muhusika kuweza kumchukulia mtu iwapo atakidhi vigezo vinavotakiwa nafikiri
 
Kitambulisho cha taifa mpaka sasa kimenajisiwa kiufupi.Kwa USA ID CARD kama hii uwezi kupata kwa mtindo watanzania na mfumo huu.Ukiwa na Id kwa wenzetu mpaka bunduki unamiliki pale pale supermarket lakini usiwe na akili ya sabaya tu.
 
tatizo muda uliwekwa wa mwezi mmoja ni mfupi mno, tayari wameishafungia namba za watu walio hai
muda wa siku 30 ulikua unatosha mkuu ukisema hautoshi hata miezi 3 bado haitatosha, nafikiri wange ongeza njia zaidi hata kutumia anuani za makazi kwa eneo uliopo kuweza kufika ofisi za NIDA makazi mapya uliopo kisha kujaza fomu malumu kuomba kitambulisho kikufikie kwa posta na kulipia gharama husika
 
wangeanisha hizo njia ingekuwa bora zaidi. Sasa wamefungia namba za kitambulisho hadi mtu atakapoenda huko mbali alikojiandikisha ndio wafungue
 
utaratibu uliwekwa hata kwa asiekua muhusika kuweza kumchukulia mtu iwapo atakidhi vigezo vinavotakiwa nafikiri
Hili utawalaumu bure NIDA, waliweka utaratibu wa kuchukuliana na walitoa karibu mwezi mzima, binafsi nimechukuliwa pia kwahiyo hapa mkuu ukubali tu wewe mwenyewe ndio ulizembea
 
mimi sio muhanga wa hilo mkuu bali nilimweleza huyo alie lalamika kwamba upo huo utaratibu wa kuchukuliwa meku
 
Back
Top Bottom