Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa amesema kuwa Serikali inaendelea kuliimarisha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa kulipatia vitendea kazi ambapo sasa inatekeleza mradi wa ununuzi vifaa mbalimbali vya kuzima moto na uokoaji pamoja na magari 150 ya kuzima moto na uokoaji.
Bashungwa ameeleza hayo tarehe 03 Februari 2025 wakati akijibu swali la Mbunge wa Ngorongoro, Emmanuel Shangai aliyetaka kujua Je, lini Serikali itanunua gari la Zimamoto Wilaya ya Ngorongoro.
“Kwa sasa Serikali inatekeleza mradi wa ununuzi vifaa mbalimbali vya kuzima moto na uokoaji pamoja na magari 150 ya kuzima moto na uokoaji” amesema Bashungwa
Amesema pindi magari 150 ya kuzima moto na uokoaji yatakapofika nchini, yatakayosambazwa nchi nzima ikiwemo Wilaya ya Ngorongoro.
Bashungwa amesema Serikali ipo mbioni kununua helikopta moja maalum kwa ajili ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ambayo yataenda sambamba na kuwapatia Mafunzo Maafisa, Wakaguzi na Askari wa Jeshi hilo.
Soma, Pia: Bunge la 12 Mkutano wa 18 Kikao cha Tano, Februari 3, 2025 asubuhi