Bashungwa: Tozo imekuwa mwarobaini wa matatizo sugu

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2021
Posts
577
Reaction score
2,595
Waziri wa TAMISEMI Mhe. Innocent Bashungwa amesema kuwa baadhi ya sekta muhimu nchini mfano ile ya afya isingeweza kupitia mabadiliko makubwa kama yaliyopo sasa kama tozo sizingekuwepo.

Ametolea mfano wa ujenzi wa vituo vipya vya afya 234 ambayo vimekamilishwa kupitia tozo ya miamala ya simu, sasa Serikali inajipanga kupeleka dawa na vifaa tiba ili vianze kuhudumia watanzania.

Aidha, ujenzi wa majengo ya wagonjwa wa nje, maabara, majengo ya wazazi pamoja na huduma zingine muhimu zimefanikisha kusogeza huduma hizi karibu na wananchi. Pia, watumishi wa afya 7612 wameajiriwa.

Sehemu zingine zilizonufanika ni sekta ya afya ambayo imeweza kuruhusu watoto wasome bure kuanzia elimu ya msingi hadi kidato cha sita.
 
Tozo zitaleta uzalendo sana Nchini kwa kuwa Raia wataanza kujitambua na kutambuliwa kama Tax payers badala ya Voters ( uchungu wa jambo lazima uugharimie kwanza) ndio sababu una uzalendo na familia yako kuliko ya Jirani

ushawahi kusikia Marekani au Ulaya unatambua Raia kwa jina la kebehi la wapiga kura ( wateja wa biashara ya Siasa)?

fyoko fyoko …wapiga kura wangu wa jimboni badala ya Walipa kodi…

…ntakuja kupiga kura pale tu nitapokuwa na uhakika kuwa kura yangu itahesabiwa na itajumuishwa kwny matokeo…' -Prof Mussa Assad
 
Waziri wa TAMISEMI Mhe. Innocent Bashungwa amesema kuwa baadhi ya sekta muhimu nchini mfano ile ya afya isingeweza kupitia mabadiliko makubwa kama yaliyopo sasa kama tozo sizingekuwepo.

Ametolea mfano wa ujenzi wa vituo vipya vya afya 234 ambayo vimekamilishwa kupitia tozo ya miamala ya simu, sasa Serikali inajipanga kupeleka dawa na vifaa tiba ili vianze kuhudumia watanzania.

Aidha, ujenzi wa ,majengo ya wagonjwa wa nje, maabara, majengo ya wazazi pamoja na huduma zingine muhimu zimefanikisha kusogeza huduma hizi karibu na wananchi. Pia, watumishi wa afya 7612 wameajiriwa.

Sehemu zingine zilizonufanika ni sekta ya afya ambayo imeweza kuruhusu watoto wasome bure kuanzia elimu ya msingi hadi kidato cha sita.
Huu ndio ukweli ambao tumekuwa tunasema siku zote lakini majitu yenye chuki binafsi yanapinga daily sasa sijui mnataka nini..

Kila Siku uzushi wa kijinga.
 
Huyu ameanza kuota mbawa
Mnaumiza wananchi kipi ambacho hamuelewi? Tukiweka pesa nyumbani kwenye magunia naona tutakuwa sawa heshima itarudi
Swala tozo kelele zipigwe kwa nguvuuuu IG Twitter etc
Mmegeuza wananchi vitega uchumi
 
Hivyo vituo vya afya Huwa haviishi? Kila siku idadi inaongezeka
 
Waziri wa TAMISEMI Mhe. Innocent Bashungwa amesema kuwa baadhi ya sekta muhimu nchini mfano ile ya afya isingeweza kupitia mabadiliko makubwa kama yaliyopo sasa kama tozo sizingekuwepo.

Ametolea mfano wa ujenzi wa vituo vipya vya afya 234 ambayo vimekamilishwa kupitia tozo ya miamala ya simu, sasa Serikali inajipanga kupeleka dawa na vifaa tiba ili vianze kuhudumia watanzania.

Aidha, ujenzi wa majengo ya wagonjwa wa nje, maabara, majengo ya wazazi pamoja na huduma zingine muhimu zimefanikisha kusogeza huduma hizi karibu na wananchi. Pia, watumishi wa afya 7612 wameajiriwa.

Sehemu zingine zilizonufanika ni sekta ya afya ambayo imeweza kuruhusu watoto wasome bure kuanzia elimu ya msingi hadi kidato cha sita.
Bashungwa wewe kweli mTanzania na ulikuwepo mlipoanza kuvaa baraka na kuomba pesa ya COVID 19?! Je unakumbuka zile pesa Ilifanya Nini na hili unalosema ni Nini.!?? Mnawafanya waTanzania mazuzu !?
 
Hili boga linaongea tuu kutetea kazi yake, waziri kama chawa, ovyo kabisa bora lingekaa kimya tuu
 
Huyu jamaa kashiba matoke, tatizo ubunge walipata kirahosi safari hii jasho la mgongo litawatoka.
 
Back
Top Bottom