Bashungwa: Wakulima wa Kahawa Kagera ni Shangwe Tupu, Bei ya Kahawa Imepanda

Bashungwa: Wakulima wa Kahawa Kagera ni Shangwe Tupu, Bei ya Kahawa Imepanda

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

WAKULIMA WA KAHAWA KAGERA NI SHANGWE TUPU, BEI YA KAHAWA IMEPANDA: BASHUNGWA

Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa Jimbo la Karagwe, Innocent Bashungwa ameipongeza Wizara ya Kilimo kwa kusimamia vyema Maono ya Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwainua Wakulima wa Kahawa na kuwezesha bei ya Kahawa kuongezeka kutoka shilingi 1,100 hadi Shilingi 4,100 kwa kilo moja ya maganda ya Kahawa aina ya Arabika.

Bashungwa ametoa pongezi hizo kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii kwa kuweka risiti ya Mauzo yake ya Kahawa yaliyofanyika leo tarehe 05 Juni 2024.

“Pongezi nyingi kwa Waziri Mhe. Bashe Hussein na timu yako ya Wizara ya Kilimo kwa kusimamia vyema maono ya Mhe. Rais kuinua wakulima wa kahawa nchini. Tunashukuru kwa jitihada za kusambaza miche ya kahawa ili vijana walime kwani kilimo kinalipa kwa kwa mikakati hii makini ya utekelezaji wa Ilani ya CCM”

Bashungwa ameeleza kuwa “Mimi ni mkulima na mwanachama wa Chama cha Msingi (AMCOS) ya Bweranyange. Namshukuru Mungu kwa mavuno ya kahawa na leo nimepeleka kahawa kwenye Chama cha msingi kuuza. Kilo ya kahawa aina ya Arabika kwa mnada wa leo Juni 5 nimeuza kwa Tsh. 4,100 kwa kilo ya maganda ya Arabika.”

“Sisi wakulima wa Kagera hii ni shangwe tupu na haijapata kutokea. Kwa miaka mingi kahawa iligota kwenye Tsh. 1,100 kwa kilo hadi Mhe. Rais alipoingia madarakani na kuingilia kati kuhusu kuzorota kwa bei ya kahawa kwa muda mrefu. Tunamshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa sera nzuri za kuinua zao la kahawa.”
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2024-06-05 at 14.24.42.jpeg
    WhatsApp Image 2024-06-05 at 14.24.42.jpeg
    164.2 KB · Views: 13
  • WhatsApp Image 2024-06-05 at 14.24.42(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-06-05 at 14.24.42(1).jpeg
    169.1 KB · Views: 10
  • WhatsApp Image 2024-06-05 at 14.24.43.jpeg
    WhatsApp Image 2024-06-05 at 14.24.43.jpeg
    171.2 KB · Views: 11
Mnajua kudanganya kitoto sana, kilichofanyika ni wazalishaji wakubwa wa kahawa mavuno hayakua mazuri kwao hivo kahawa chache imevamiwa na mabepari wa kidunia, hebu muulize Kwa nini mahindi hayapandi?
 
Rais hana uwezo wa kucontrol soko la kahawa, pamba, korosho, mbaazi, hayo mazao yana wenyewe huko duniani
 
Wanaoshangilia ni wale madalali/ wezi waliorasimishwa: AMKOSI
 
Back
Top Bottom